Jina....TABASAMU LA UCHUNGU
Mtunzi......... Official Dully
Mkasa....wa...kusisismua
Sehemu Ya {19}
ILIPOISHIA..
Alipata njia kuingia ndani na taratibu alianza kujongea huku akiifunga bastora yake kiwambo cha kuzuia sauti pindi akifyatua risasi na siku hiyo naweza kusema ilikuwa siku mbaya kwa Ochu ambae alikuwa busy kunywa na kuwatumia watoto wa kike kadri awezavyo.....ENDEIA.....
Ulikuwa ni usiku wenye furaha kwa Ochu lakini usiku huo ulibadilika ghafla na kuwa mbaya kwake, uliojaa majonzi na wenye kuogopesha sana ama kwa hakika hakuna anaeijua kesho yake au baadae yake.
Chumba kizima mabinti walianza kukimbizana kutoka nnje baada ya kumuona Stephan ameingia huku akiwa na bastora mkononi, lakini pia hata Ochu kitendo hicho kilimuogopesha sio kidogo.
"We...we..wewe ni nani na umefuata nini kwenye hiyama yangu, naomba uende kabla hayajakukuta makubwa tafadhali.!!"
Ochu alizungumza kwa kutetemeka huku mkononi akiwa amekamata chupa kwaajili ya kujihami.
"Sasa unauliza kuhusu mimi wakati mimi ndiye yule jamaa ulienipiga na chupa kisha ukajiona umeshinda mbele za watu, lakini leo nimekuja tuoneshane ubabe tukiwa wawili na hii nafasi nakupa ya kujitetea kama ukinipiga nakuacha lakini kama hutaki basi utakufa kizembe"
Stephan alizungumza kwa kujiamini sana na Ochu alipovuta kumbukumbu alimkumbuka Stephan hivyo aliona kama ndiye mtu aliempiga chupa basi leo hatotoka salama.
"Hey mlinziiiiii.!!!"
"Unajua unafurahisha sana wewe, sasa mlinzi wa nini mbona unakuwa kama mwanamke wewe wakati hapa nimekuja tucheze au unataka nianze kukumaliza taratibu"
Stephan aliikoki bunduki yake vyema lakini wakati huo Ochu alishika chupa nyingine na kitendo cha haraka alimrushia Stephan ambae ilimpata mkononi na ile bastora kuanguka chini.
Wakati anainama ili kuiokota Ochu alimrukia na kuanguka nae chini sasa ikawa ni patashika ya watu wawili huku kila mmoja akitaka kuiwahi ile bastora ampige mwenzake.
Virugu zilizozuka hapo hazikuwa ndogo, hazikuwa za kitoto lakini mwisho Ochu aliipata ile bastora na bila kuchelewa alimpiga nayo Stephan mguuni na kupelekea ahisi maumivu makali sana huku damu nyingi zikimvuja.
Uzuri wa Ochu alikuwa ni mwanaume aliejazia mwili na mwenye nguvu ila kwa Stephan hakuwa na mwili mkubwa na hata nguvu alizokuwa nazo hazikuweza kutosha kumzuia Ochu mwenye miraba minne iliyojijenga kwa mazoezi.
Hiyo ilikuwa ni vita ya tatu ya dunia mwisho Ochu alifyatua risasi nyingine iliyopenya vyema begani kwa Stephan na kumfanya sasa azidiwe na kicheko kikali kikasikika kutoka kwa Ochu.
"Hahaha unajua mimi mtu wa mchezo sio, yaani wewe bado mtoto kwangu kwahiyo umezaliwa umetukuta na acha uondoke leo utuache na dunia yetu hahaha"
Ochu alizungumza kwa kejeli na kujiamini maana aliona Stephan hatofanya lolote ukizingatia amemzidi nguvu.
Katika purukushani hizo Stephan alitazama pembeni kwenye sakafu aliona kuna kipande kikubwa cha chupa kilichovunjika hivyo alikichukua na kukikamata vyema bila hata Ochu kushtuka.
"Sasa nikwambie tu wewe ndiye utakaekwenda kuzimu alafu mimi utaniacha kwahiyo nikuage ndugu yangu kwaheri pia hata uko uendapo ujifunze kuto jiona mbabe mbele za watu la sivyo utakufa tena"
Ilikuwa ni kauli ya Stephan iliyomfanya Ochu acheke sana maana akitazama bastora alikuwa ameimiliki yeye kwa asilimia kubwa lakini hakujua Stephan alikuwa amekamata kipande cha chupa ambacho ndicho kilichompa jeuri.
Wakati Ochu anazumza na kucheka kwa kujiamini ghafla alihisi kitu kimechoma shingoni mwake na aliposhika kisha kutazama alistaajabu kuona damu zikimtoka kama maji hivyo alijikuta akizuia lakini damu zilizotoka zilikuwa ni nyingi sana ambazo zilimmaliza nguvu.
Stepha hiyo ikawa ni nafuu kwake lakini damu za Ochu zilikuwa zikimrukia mwilini mwake hivyo ilibidi amsukume pembeni, alichukua bastora na kujiinua taratubu kutoka nnje ila wakati anaufikia mrango alisikia gari za polisi zikiwa zimewasili hapo.
Haikujulikana polisi hao walipataje taarifa au huenda ni wale mabinti ndio walitoa taarifa polisi hivyo polisi walifika na kutanda nnje ya nyumha ya Ochu huku wakiwa na siraha kali za moto.
"Mungu wangu sasa hapa nitatokaje jamani.!?"
Stephan sasa akili ilimpata moto lakini mwisho alipata wazo na aliona wazo hilo afanye huenda likamsaidia kutoka hapo salama.
Polisi wakiwa nnje wametulia wakipanga mbinu za kuingia ndani ghafla waliona gari nyeusi ikitoka kwa kasi sana hivyo iliwabidi warudi kwenye gari zao na kuanza kuifukuza.
Waliifukuzia mwisho waliweza kuzuia ila walipotazaa ndani hapakuwa na mtu kwa maana Stephana alikuwa amewachezea mchezo, hata waliporudi tena nyumbani kwa Ochu walikuta maiti tu Stephan hayupo na ushahidi wote umetolewa.
Tresha alikuwa ni mtu wa mawazo kwa upande wake pia alikuwa mtu wa kujiuliza kuhusu Stephan anaendeleaje lakini akiwa kwenye maswali alisikia honi ikipigwa upande wa nnje.
Haraka alitoka na ndipo alipoona gari ya Stphan imewasili, alifurahi sana tu lakini gari ilipoingia na kusimama ukimya ulitawala hakuna yeyote alieshuka.
"Mh mbona Stephana ashuki tena au kuna jambo limemkuta huko alipokwenda.!?"
Tresha kengele ya hatari iligonga kichwani mwake, aliliendea gari haraka na kufungua ila alimkuta Stephan kwenye hali mbaya sana na hii ilimtisha sio kidogo.
Hakuwa na muda wa kuchelewa alimchukua haraka na kumuingiza ndani kwaajili ya kumpa matibabu maana alikuwa anatokwa na damu nyingi sana kwenye majeraha yake.
***************
Siku iliyofuata Stephan alipata unafuu na alipofungua macho alikutana na sura ya binti mrembo Tresha, aliachia tabasamu mwanana lakini Tresha alikuwa amezira kwa hasira hakutaka hata kumchekea kabisa.
"Jamani kipenzi shida nini mbona unaonekana upo tofauti kabisa.!?"
Stephana aliuliza huku akimtazama Tresha ambae hakuwa hata na dalili ya kutabasamu.
"Unataka mimi nibaki mwenyewe sio, sasa sitaki kujua ulienda wapi na nini kimekukuta usiku wa jana ila sitaki huo ukatili uendelee najua tayari umeua mtu kwahiyo sitaki tena.!!"
"Nimekuelewa kipenzi na nishaacha kabisa hayo mambo kwahiyo usiwe na wasiwasi kuanzia leo nakuapia sitaweza kuuwa tena nahitaji sasa mimi na wewe tuingie kwenye ndoa na kujenga familia"
Stephan alizungumza maneno yaliyorudisha tabasamu la Tresha na kujikuta kila mmoja akifurahi.
Hatimae siku nazo taratibu zilianza kwenda hali ya Stephan ikiwa njema kabisa, lakini siku moja majira ya saa saba mchana Tresha akiwa busy kufanya usafi na wakati huo Stephan alikuwa kazini ila ghfla alianza kuhisi hali tofauti mwilini mwake
Kizunguzungu kilimshika na kujikuta akishindwa kuendelea na kazi hivyo aliacha na kujiandaa kisha alielekea haopital ambapo alipimwa na majibu yalionesha ni mjamzito tena mimba ikiwa na week mbili tu.
Taarifa hizo zilimshtua na kumfurahisha sana, alitamani kumpigia Stephana ampe taarifa lakini alisita na kumsubiri arudi ili amsurprise vizuri.
Tuache huko tuja upande wa Joyce ambae alipata mshtuko baada ya kusikia Ochu amefariki lakini taarifa hizo sio kumshtua tu pia zilimfurahisha maana alikuwa ni mwanaume anaemchukia sana.
"Dada vipi mbona unaonekana upo na furaha leo au tayari Stephan amekukubalia na atakuoa hivi karibuni?"
Lilikuwa ni swali la Stellah akimuuliza dada yake ambae alikuwa na furaha sana siku hiyo lakini..
"Hapana mdogowangu hata hivyo nimemuacha Stephan kama ambavyo mama alivyotaka kwahiyo kwa sasa namtakia maisha mema naamini na mimi nitapata wa kunipenda kwa dhati sana".
"Hayo ndiyo maneno sasa yaani ni kumuomba Mungu akupe wako kwahiyo mimi nipo upande wako kila kitu kitakuwa sawa dada"
Basi ilikuwa ni kutiana moyo mtu na mdogo wake hivyo hata mama yao alipokuwa akiwatazama alibaki kutabasamu na kutikisa kichwa kukubaliana na maamuzi ambayo Joyce aliyachukua.
*****************
Usiku ulipowadia mama Stephan na mume wake sambamba na Sasha walikuwa mezani wakipata kifungua kinywa lakini muda huo huo simu ya mama Stepha iliingia message ya video na namba ilikuwa ngeni hivyo aliifungua lakini video ile ilimuacha mdomo wazi na nusu impe presha.
Ilikuwa ni video ikimuonesha Sasha akifanya mapenzi na Daniel hivyo mama uvumilivu ulimshunda aliiweka ile video mezani na kila mmoja aliiona.
Sasha pozi lilimuisha hata baba Stephan nae alikuwa haamini na ndipo sasa lawama zikageukia kwa Sasha ambae alikuwa akilia bila kujibu chochote.
"Kumbe ni mshenzi hivi, unataka kuolewa na mtoto wangu kumbe humpendi ila kuna mwanaume ambae upo nae, unataka kumpa mwanangu maradhi sio.!?"
"Ni...nisam...."
"Weee tena unyamaze na ukome haya chukua kila kilicho chako na uende sihitaji tena ukae kwenye nyumba yangu naomba uende nisije kukuuwa hapa!!"
Mama Stephana alikuwa serious maana binti aliekuwa anamtegemea sasa amemkosea pakubwa sana.
"Mume wangu ulikuwa sahihi sana kumbe huyu sio binti wa kuolewa na kijana wetu kabisa sasa mimi namuhalalisha Tresha kuwa mkwe wangu na hivi punde aolewe na mwanangu ila huyu simtaki kabisa"
Mama Stephan sasa alibadili uelekeo lakini Sasha alikuwa ni mtu wa kulia na kuomba msamaha kwa madai ilikuwa ni bahati mbaya alikuwa amelewa na kujikuta akifanya hivyo lakini mama Stephana hakutaka kumsikiliza kabisa.
Wakati hayo yanaendelea na haikujulikana nani ametuma hiyo video huku upande wa Sidan alikuwa njiani kurudi kwake lakini akiwa busy kuendesha gari simu yake ilianza kuita na aliekuwa anapiga alikuwa ni mama yake.
"Hello mama.?"
"Hello mwanangu, naomba kama inawezekana kesho usiende kazini uje hapa na Tresha kuna mambo nataka tuongee"
"Sawa mama"
Stephana alikata simu na kujikuta akiwa na maswali mengi kichwani lakini huku upande wa Daniel alikuwa akicheka sana huku akiitazama ile video kwa maana yeye ndie alimtumia mama Stephan na yeye ndiye alirecod bila Sasha kujua, sasa haieleweki kwanini alifanya hivyo ila alikuwa na maana kubwa sana. ....ITAENDELEA...
Unafikiri kwanini Daniel amefanya hivyo, ana lengo gani kufanya hivyo, mimi sifahamu ila majibu utayapata sehemu ya mwisho ya mkasa huu wa kusisimua...20...
