Jina....TABASAMU LA UCHUNGU
Mtunzi....... Official Dully
Mkasa....wa...kusisismua

            Sehemu Ya {20} FINAL

ILIPOISHIA..

Stephana alikata simu na kujikuta akiwa na maswali mengi kichwani lakini huku upande wa Daniel alikuwa akicheka sana huku akiitazama ile video kwa maana yeye ndie alimtumia mama Stephan na yeye ndiye alirecod bila Sasha kujua, sasa haieleweki kwanini alifanya hivyo ila alikuwa na maana kubwa sana......ENDELEA...

 Stephan alifika kwake akiwa mwingi wa mawazo hasa baada ya kupigiwa simu na mama yake, hakuelewa simu hiyo ilikuwa inahusu aende kufanya nini lakini hakufahamu kama tayari mama yake amebadili mawazo na hii ni baada ya kuona video inayomuhusu Sasha akifanya uchafu.

Alifika kwake lakini alikuta geti lipo wazi na haikuwa kawaida, pia nyumba nzima ilikuwa imetawala kiza, hii kidogo ikampa mashaka Stephan na kuanza kujiuliza maswali huku taratibu akiingiza gari ndani.

Aliifikisha sehemu ya sparking, hakujali kama imepark vizuri au laa, aliteremka na kuanza kujongea ndani kwa mwendo wa haraka huku akimwita Tresha ambae hakuitika kabisa.
     Alipanda ngazi mpaka ulipo mrango wa kuingilia ndani lakini kabla hajaufungua alisita, alitoa simu yake ili kuwasha tochi lakini simu ilikuwa na asilimia chache hivyo isingeweza kuwasha tochi.

Basi ilibidi ajikaze na kuingia ndani lakini kitendo cha kuingia taa ziliwashwa na makofi yalianza kupigwa, sebule nzima ilikuwa imepambwa vyema kwa maua na vitaa lakini mpaka wakati huo Stephan hakuelewa surprise hiyo inahusu nini.

"Woww hongera sana Stephan hongera sanaaa najua hii ni surprise nimeuifanyia lakini hongera sana"
      Tresha alizungumza huku akimsogelea Stephan na mkononi akiwa na karatasi ya majibu ya mimba.

"Hongera ya nini wakati birthday yangu imepita na keki tumekula sasa hiyo surprise imahusu nini mbona unanichanganya jamami.!?"
      Stephan aliuliza huku aikimtazama Tresha ambae bila kuchelewa alimpa majibu ya mimba asomea.

"Inahusu nini hii karatasi.!?"

"Wewe chukua, fungua na usome utaelewa wala usijali na hiyo ndio surprise ambayo nimekufanyia pia hongera sana jamani"

Stephan hakuwa na jinsi kuchukua ile karatasi na kuifungua lakini alivyosoma na kuona majibu yaliyoandikwa mule alijikuta akifurahia na kurukaruka maana hakuamini kama anakwenda kuitwa baba na furaha yake ilipitiliza mpaka aliteleza na kuanguka chini.

"Jamani mpenzi sasa ndio furaha gani hiyo unataka kujiua alafu mwisho mtoto azaliwe asikie baba yake alikufa wakati anasherehekea mimba yake, hebu kwanza kuwa mpole jamani.!!"

"Ok sawa pia hongera sana unakwenda kuitwa mama na nilivyo na furaha hapa nataka kesho twende ukachague gari kazini kwangu hiyo ni maaluma kwa kutembelea mama kijacho wangu"

"Mh lakini nawezaje kuendesha jamani.!?"

"Usijali nitakufundisha alafu pia mama anahitaji kutuona kesho kwahiyo mapema kama saa sita tufike pale alafu tukitoka tutaenda kuchukua gari yako mambo yawe mazuri"

"Mh kwenda kwa mama tena, kuna nini huko maana ninvyomuogopa mpaka najikuta natetemeka hapa.!!"

"Wewe usijali bhana hapa cha kufanya jiandae kesho twende kwani si nipo upande wake akikuletea za kuleta basi nitadeal nae kwahiyo kuwa na imani na naamini kabisa kwamba hakutakuwa na jambo lolote baya"

"Sawa nitaenea kwaajili yako"

Basi siku hiyo ilikuwa ni furaha tu kwa wawili hao lakini huku kwa Sasha alikusanya mabegi yake na kuondoka akisindikizwa na maneno juu maana alikuwa amefanya ujinga mwenyewe ambao ulipelekea kubadili akili ya mama Stephan.

"Ila nikwambie tu hata kwenye harusi ya mwanangu sitaki kukuona maana utaleta nuksi mshenzi mkubwa wewe, unajua jinsi gani umenivunja moyo, nilikuamini sana lakini hukutaka kulinda imani yangu kwako"

"Sawa mama naenda najua mimi nimekosa aina haja ya kulalamika sana nimekuelewa"
     Sasha masikini alitoka na mabegi yake usiku usiku kama mkimbizi, alichukua gari yake na kuondoka lakini akiwa njiani alipigiwa simu na aliepiga alikuwa ni Daniel.

Alipoona lile jina alipaki gari pembeni ili kumshushia maneno vizuri maana yeye ndiye chanzo cha yote mpaka kumkosa Stephan na kufukuzwa usiku usiku kama mwizi.

"Hello Sasha mambo natumai upo njiani kuna sehemu unaelekea ila niambie unaenda wapi nije kukufuata kipenzi"
      Daniel alianza kuzungumza na alijua tu lazima Sasha atakuwa amefukuzwa.

"Ukaona fahari sana kurecod na kusambaza video sijui ni mwanaume wa aina gani wewe yaani nakuchukia sana kaa ukijua hilo lakini sasa nikwambie tu kile alichotakiwa kupata Stephan sasa umekipata wewe"

"Kipi tena.!?"
     Daniel alishtuka kidogo kusikia kauli hiyo lakini Sasha alianza kucheka.

"Unajua niliwahi kukwambia muda sana kwamba nina kisasi na Stephan na ipo siku nitalipiza, mimi kutaka anioe sio kwamba nampenda hapa lakini nilitaka nilale nae hata kwa usiku mmoja ili kumteketeza lakini nashangaa umemsaidia ama kweli wewe ni rafiki bora"

"Una....unasema nini wewe mwanamke kwahiyo unataka kusema wewe ni muathirika wa ukimwi.!!!?"

"Ndiyo ni muathirika, unafikiri siku naondoka baada ya kuacha kazi kwa Stephan nilikuwa na maisha gani, nilikuwa sina kitu alafu baadae ulikuja kuniona tena ukaniona namilki gari la kifahari pesa ninazo kwahiyo hata hukujiuliza.!?"

"Hebu kwanza tuache utani Sasha niambie ukweli wewe ni muathirika au unanitisha tu ili kunirusha roho.!?"

"Ukweli ni huo baada ya kutoka hapa nilijiunga na makundi wa wadada wanaojiuza na ndipo nimeupata huu ugonjwa kwahiyo nakushauri nenda kapime kisha uanze kutumia dozi haraka"

Sasha alimaliza kuzungumza na kukata simu, alitoa line na kuitupa kisha aliwasha gari na kutokomea pasipo julikana huku nyuma akimuacha Daniel akipiga simu lakini jibu alilopata namba anayopiga ilikuwa haipatikani.

               ****************

Siku iliyofuata kama ambavyo Stephan alivyoitwa ndivyo alivyofika na siku hiyo walipoingia yeye na Tresha walipokelewa na vigelegele vilivyopigwa na ndugu wengi waliokuwa wamefika hapo na hii ilimfanya Stephan pamoja na Tresha watambue kwamba uchumba wao umekubalika.

Walikaribishwa kama wageni na siku hiyo mama Stephan alikuwa akimnyenyekea Tresha kama dhahabu maana ndio chaguo la kijana wake japo yeye alimpendekeza Sasha lakini Sasha alipoteza bahati.

"Karibuni sana wapendanao na mjisikie huru kabisaa sio kwasababu mmeona wageni mkajifanya mnaogopa sasa nataka muwe na furaha na muwe huru"

"Usijali mama"
      Stephana alijibu kisha walitoa salamu kwa wageni hao na walikuwa ni ndugu wa wazazi ambao hakuwafahamu maana alichukuliwa na kulelewa tu.

"Mkwe wangu Tresha pia karibu sana alafu umepoa sana au unaumwa jamani.!?"
        Mama Stephan alizungumza ila kuna bibi mmoja alisogea na kumtazama vizuri Tresha na baadae alimuuliza swali ambalo Tresha hakutaka kulificha.

"Wewe ni mjamzito binti.?"

"N...ndiyo mimi mjamzito"
        Tresha alijibu kwa hofu lakini jibu lake lilizua furaha zaidi na kumfanya hata Baba Stephan aliekuwa pembeni atabasamu maana zilikuwa ni habari njema.

"Lakini kwa kiasi fulani hiyo ni aibu kubwa sana kuzaa nnje ya ndoa kwahiyo kesho mapema maandalizi ya ndoa yafanyike, kadi zitengenezwe na kusambazwa mpaka week hii ikiisha basi inayokuja harusi ifanyike"
      Baba Stephan alizungumza na kufanya Tresha ashangae maana hakuamini kama swala hilo lingesikika masikioni mwake.

Ok wakati huko story na mipango ya ndoa inafanyika huku kwa Danjel alikuwa mtu wa kunywa pombe tu, chupa zilikuwa zimemzunguka, alikuwa anakunywa huku akitazama karatasi iliyokuwa na majibu yanayomfahamisha ni muathirika.

"Huyu mwanamke ameniua hivi hivi, ama kweli wanawake hawana roho ya huruma kabisa tena ni washenzi sana"
      Daniel masikini ujanja wake ulikuwa mfukoni, kicheko alichocheka kumkomoa Sasha sasa aliona kimegeuka na kuwa kilio, alijikuta akijutia kitendo alichofanya na ilifika wakati alitamani kujiua kabisa.

              *******************

Taratibu siku zilianza kujongea na hatimae week ya kwanza ilikamilika na week iliyofuata ndio ilikuwa week ya harusi kwa wapendanao wawili ambao walipitia changamoto nyingi kufika hapo.

Harusi ilifana, watu kutoka sehemu mbali mbali walifika kuhudhuria harusi hiyo hata Joyce pia alikuwepo na yeye ndiye alikuwa makeup wa Tresha pia alikuwa ni mpambe wake aliemshikia shera lake refu lililokuwa likiburuzika chini.

Licha ya harusi hiyo kufana lakini haikutakiwa kuchukua muda mwingi ilikuwa na ratiba za haraka sana kutokana na hali ya Tresha kuwa sio nzuri na yote ni sababu ya ujauzito aliokuwa nao ambao ulimfanya ajihisi mchovu sana.

Ilikuwa ni furaha kwa kila mmoja na hata baada ya harusi wakiwa kwenye chumba chao cha kujipumzisha Tresha hakujisikia kufanya chochote.

"Mume wangu najua kama hii ni siku muhimu sana kwetu na ni siku tuliyoisubiria kwa hamu ila nakuomba basi tusifanye chochote kwa leo nahisi nipo mchovu na....."
       Tresha hakumaliza kuogea aliinuka na kukimilia bafuni kutapika kama kawaida ya wajawazito wengi.

Ilibidi Stephan amuelewe lakini akiwa hapo alipigiwa simu na mfanyakazi wake, hakutaka kupuuzia alipokea lakini taarifa alizopata zilimshtua sana.

"Eti.!?"

"Ndiyo bosi Daniel amekutwa chumbani kwake amekunywa sumu sasa sijui nini kimemfanya afanye hivyo.!?"

"Kwahiyo sasa mwili wake uko wapi.!?"

"Umepelekwa hospital maana ulikuwa umeanza kuharibika pia inaonesha hakunywa sumu jana alikuwa juzi kwahiyo uchunguzi unaendelea na sisi tunaenda hospital kufanya taratibu za kuupata mwili ili taratibu za mazishi zianze"

"Ok basi sawa mtakuwa mnanijulisha hatu kwa hatua"

Stephan alijikuta roho ikimuuma sana maana Daniel alikuwa ni mtu wake wa karibu sana pia ni rafiki yake ambae wamesoma wote ila Tresha aliporudi kutoka bafuni alimkuta Stephan ameshika tama huku akiwa mwingi wa mawazo.

"Mume wangu Shida nini tena mbona unaonekana hauko powa kabisa jamani au umekasirika kwakuwa......"

"Hapana bhana nipo kawaida wala usijali mke wangu"

Stephan ilibidi amfiche Tresha hakutaka kabisa kumueleza nini kinamsibu, alionesha tabasamu usoni lakini ndani yake lilikuwa limejaa uchungu wa hali ya juu ila kama mwanaume alijikaza na kuchukua jukumu la kumfurahisha mke wake kipenzi ambae alikuwa ni mjamzito aliehitaji furaha kila wakati.

Basi ziku zilianza kusogea huku wanandoa hao wakiwa na furaha sana hata ilipofika wakati wa mazishi Stephan alifanikisha lakini mwezi ambao Tresha alishika uchungu ulikuwa ni mwezi wa saba majira ya saa mbili usiku wakiwa busy kutazama runinga ndipo uchungu ulimshika Tresha.

Kwakua walikuwa na usafiri wao binafi basi Stephan alitoka nnje akiwa amembeba mke wake kisha kumpakia kwenye gari na safari ya kuelekea hospital ilianza.

Ilikuwa si mbali sana ambapo iliwachukua nusu saa kufika na walipofika walipokelewa vizuri na huduma ya kumsaidia Tresha kijifungua ilianza huku Stephan akiwa nnje kusubiri matokeo pia hakuacha kumuomba Mungu mke wake ajifungue salama.

Baada ya kama dakika kumi alisikia mtoto akilia hivyo alijikuta akitabasamu na muda ulipokwenda Tresha alibadilishwa wodi na ruhusa ilitolewa kwa Stephan kwenda kumuona mke wake pamoja na mtoto wake.

Alikuwa na furaha sana alielekea mpaka kwenye chumba alicho Tresha lakini alipofika alifurahi kumuona mzima na anemkumbatia mtoto kifuani kwake.

"Mke wang....."

"Shiiiii binti yangu amelala kwahiyo usipige kelele maana akiamka sitakuelewa"

"Mh we nae haya sawa lakini hongera sana mke wangu yaani daaah siamini kama leo naitwa baba na nimepata binti kwahiyo acha niwajuze wazee watambue"

Stephan alifanya taratibu za kuwataarifu wazazi wake kisha aliikumbatia famili yake na muda mchache baadae wazazi wa Stephan walifika wakiwa wenye furaha familia yao kuongezena ama kwa hakika kila mmoja alikuwa mwenye tabasamu na amani moyoni mwake...»»»»

              ****MWISHO***

Mpaka kufikia hapa sina la ziada niseme asante sana wewe ulieniazima muda wako kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa mkasa huu ila kikubwa tumshukuru Mungu kwa kutujaalia uzima mpaka hapa na tuombe zaidi atukutanishe kwenye vigongo vinavyofuataa...

SIMULIZI INAYOFUATA *MWISHO WA MATESO* INAKUJA HIVI KARIBUNI...❤❤