Jina....TABASAMU LA UCHUNGU
Mtunzi........ Official Dully
Mkasa....wa...kusisismua

            Sehemu Ya {18}

ILIPOISHIA..

Stephan kwa ujasiri aliinuka ili kwenda kufungua lakini upande wa nnje aliefika alikuwa ni Gidion kweli tena alikuwa na rungu kubwa ambalo aliona ni silaha tosha kumkabili Stephan, aligonga tena geti na baada ya kusikia hatua za mtu anakuja kufungua alijificha ili akitoka ammalize kama atakuwa Stephan......ENDELEA.....

Stephan alitoka mpaka nnje na kulifikia geti lakini kabla hajafungua Tresha alimwita na alipogeuka alimuona amesimama juu ya ngazi huku akionekana ni mtu mwenye wasiwasi sana.

"Hebu rudi ndani tafadhali"

"Hapana Stephan usifungue tafadhali unaweza kujikuta unaingia matatizoni ila kama hunisikilizi basi sawa lakini ni kwaajili ya usalama wako mpenzi wangu.!!"
      Tresha alizungumza huku akiwa mwingi wa hofu lakini Stephan hakujali alijamini kupika kiasi.

Basi taratibu alishika geti na kulifungua ila alipotazama nnje hakuona mtu yeyote lakini Gidion alikuwa amebana pembeni kwenye kiza akimtazama na kumvutia kasi ili amshushie kipgo.

"Mbona hakuna yeyote hapa au watakuwa wahuni tu wameamua kutusumbua.!!"
      Stephan alizungumza kwa sauti lakini hakuwekea maanani sana kauli yake alikuwa makini kupita maelezo.

"Basi kama hakuna mtu rudi mpenzi maana chakula kinapoa kule jamani mwisho unataka tule cha baridi kama watoto.!"

"Ok sawa nakuja"
       Stephan alipiga hatua kadhaa lakini masikio yake aliyatega nyuma kama kuna mtu anakuja aweze kumsikia.

Kweli bhana Gidion aliona huo ndio muda wa kummaliza Stephan, alitoka kwa kasi lakini Stephan hakuwa na papara japo alishajua kuna mtu anakuja nyuma yake tena kwa kasi sana.
     Stphan hakuwa mikono mitupu kumbe wakati anainuka mezani alichukua kisu kidogo ambacho kilikuwa maalum kwaajili ya kulia na kukiweka kiunoni hivyo alipeleka mkono kiunoni na kukichomoa haraka kisha aligeuka kwa kasi ya ajabu sana.

Alimuona vyema Gidion ambae alikuwa tayari amemfikia na kurusha rungu usawa wa kichwani lakini kwa ushapu aliokuwa nao alibonyea chini kidogo na kupelekea lile rungu kumkosa.

Gidion hakukata tamaa aligeuka na kurusha rungu kwa mara ya pili lakini Stephan alilidaka na bila kuchelewa alipitisha kisu tumboni kwa Gidion ambacho kilimuingia vyema na kupelekea damu nyingi kumtoka.

Tukio lililokuwa likiendelea hapo ilikuwa ni kama filamu ya kina jackie chen ambayo ilimfanya Tresha aogope na kuanza kupiga lele huku akilia na alishuhudia jinsi Stephan alikuwa anafanya unyama huku akijiuliza Stephan ni mtu wa aina gani mbona hakuwa na huruma hata kidogo.

Mdani ya dakika kadhaa Gidion alikuwa amekatwa vibaya sana mwilini mwake na kupelekea damu nyingi sana kumvuja huku hali yake ikiwa mbaya sana lakini Stephan kwa upande wake hakuwa hata na jeraha zaidi ya damu zilizomtapakaa mwilini kutoka kwa Gidion.

"Wewe sio wa kuachwa hai najua utakuja kunisumbua baadae na hata kusumbua watoto wangu kwahiyo huu ni muda wako wa kukuondoka duniani"
     Stephan alizungumza huku akiokota rungu ambalo Gidio alikuja nalo.

"Ni bora iwe hivyo, uniue maana kama ukiniacha leo basi nitakuuwa wewe kwahiyo hii nafasi umepata basi usiichezea itumie kwa usahihi hahaha"
      Gidion licha ya hali mbaya aliyokuwa nayo lakini alionekana kuto kujali kifo ndio kwanza aliongea kwa dharau na kejeli.

Stephana nae hakutaka kumuacha, alimpiga na rungu moja matata ambalo lilimfanya Gidion aanguke na kupoteza maisha bila hata kuomba maji.

"Sasa wasalimie huko uendapo ikiwezekana niwekee na nafasi ili siku yangu ikifika basi tukutane huko huko mshenzi wewe"
    Stepha alizungumza huku akilitupa lile rungu chini na kuingia ndani, bahati nzuri nyumba yao ilikuwa sehemu ambapo watu ni ngumu kupita hivyo tukio hilo la mauaji hawakuweza kuliona.

Wakati Stephan anaingia ndani Tresha alianza kurudi nyuma kwa hofu maana alichoshudumia hapo kilikuwa ni kitendo cha ukatili sana kilichofanywa na Stephan bila hofu.

"Stephan tafadhali naomba ishia huko huko sitaki unisogelee wala uingie humu ndani muuaji mkubwa wewe tena sitaki hata unitazame.!!"
       Tresha alizungumza huku akitetemeka lakini Stephan hakujali ndio kwanza alikuwa akijongea alipo Tresha.

"Wewe ni nani ambae katili namna hiyo, mbona Stephan ninaemjua mimi sio wewe.!?"

"Yah sio mimi, mimi ni Stephan wa mtaani ambae maisha haya ya kuuwa nimeacha muda sana lakini leo nimeamua kuyarudia ili kutetea penzi letu.!"

"Hapana naomba tu usinisogelee Steph...."
      Tresha hakumaliza kuongea aliyokusudia alianguka chini na kupoteza fahamu maana tukio lililotokea hapo lilikuwa la kikatili sana na tangu kuzaliwa kwake hakuona ukatili wa namna hiyo.

Basi Stephan ilibidi amuwahi na kumchukua kumpelekea ndani kwaajili ya huduma ya kwanza, alipompatia huduma ya kwanza alimuacha na kutoka nnje ambapo alichukua gari lake na kuitoa ile maiti.

Haikujulikana aliipeleka wapi lakini aliporudi alifanya usafi kufuta ushahidi nyumba nzima kisha alirudi ndani ambapo alimkuta tayari Tresha amerejewa na fahamu lakini Tresha alikuwa akimuogopa sana Stephan.

                 ***************

Hata siku iliyofuata asubuhi wakati wa kupata kifungua kinywa kila mmoja alikaa mbali na mwenzie wakati ilizoeleka kukaa pamoja na hata kulishana chakula lakini siku hiyo ilikuwa tofauti kabisa na siku nyingine.

"Sasa ile maiti umeipeleka wapi.!?"
       Wakati wakiwa kimya Tresha aliamua kuvunja ukimya na kumtupia swali Stephan ambae hakutaka kumjibu mpaka pale alipomuuliza tena.

"Kwahiyo hunisikii nauliza ile maiti umeipeleka.!?"

"Kwani ulitaka ulale nayo ndani au?"

"Hapana ila nimeuliza kwahiyo kama unaona huwezi kunijibu basi kaa kimya hata hivyo sijali sana kuhusu dhambi uliyoifanya"

"Ahaa sawa ila maiti imeendwa kuchomwa moto hakuna ushahidi wowote zaidi yako ndie shahidi uliebaki"

"Ahaaa sawa ila nataka kujua Stephan wewe ni mtu wa sampuli gani mbona huna hofu kabisa na ukatili ulioufanya jana au hapo kabla ulikuwa muuaji.!?"
      Tresha alikuwa na maswali mengi siku hiyo lakini maswali yake yalijibiwa kwa uchache na mingine yaliachwa.

"Zamani nilikuwa muuwaji wa kukodi kabla sijachukuliwa na hawa wazazi ambao wameishi na mimi mpaka kufikia hapa, najua kwamba wao wanafahamu mimi sifahamu kuwa sio wazazi wangu lakini nafahamu ila naishi kwa kuwafanya wasifahamu"

"Kwahiyo hawa sio wazazi wako na kwanini sasa ulikuwa muuwaji.!?"

"Kwasababu ya kifo cha wazazi wangu ambao waliuwawa na waliowauwa nimewaua kwa mikono yangu na nilianza kuuwa nikiwa na miaka 18 ila nilipochukuliwa ndipo nikaamua kuacha na kuwa mtu mwingine"

Stephan hakutaka kuficha tena alianza kusimua moja baada ya jingine na kufanya Tresha ajue ukweli kuhusu maisha ya Stephan.

"Pole sana Stephan kumbe wakati wote ulikuwa na tabasamu la uchungu lakini usijali kikubwa tushukuru Mungu tupo salama maana story za maisha yetu inafanana kabisa"

Tresha sasa alijikuta akisogeza kiti na kuketi kando ya Stephana mbae alikuwa alijikuta akitabasamu na kumkumbatia Tresha wake.

Wakati hayo yanaendelea huku kwa Joyce bado alikuwa anateseka baada ya kupata taarifa kwamba Stephan anaenda kuoa siku zijazo, moja ilikuwa haikai wala mbili kichwani kwake maana haikuwa kawaida yake kumfuatila mwanaume halafu kumkosa ila kwa hii ilimuumiza kichwa sana.

Wakati akiwa mwingu wa mawazo aliingia mama yake na kumtaka aelekee sebuleni kupata kifungua kinywa lakini Joyce alikataa.

"Unajua mwanangu kwenye maisha kuna kupata na kukosa, kama huyo mwanaume anataka kuoa basi ujue sio bahati yako wewe unachotakiwa kufanya ni kutulia huenda ukatapa mwanaume mwingine zaidi ya huyo"

"Mama lakini nampenda sana Stephan na sijui kama nitampenda mwanaume mwingine mimi"
     Joyce mpaka alikuwa akilia na hii ilionesha jinsi gani alivyo na upendo wa dhati juu ya Stephan.

              ******************

Usiku ulipowadia Stephan alimuacha Tresha amelala na kuinuka, alisogea mpaka kwenye kabati lake na kufungua droo ya siri kisha alitoa bastora na kuiweka pembeni.
      Haikujulikana alikuwa na dhumuni gani lakini alipomaliza kuitoa alivaa mavazi vizuri na ile bastora aliichimbilia kiuoni lakini alipotaka kutoka Tresha alimwita.

"Mpenzi unakwenda wapi na hiyo bastora kiunoni ya nini alafu kumbe unamiliki bastora hata mimi sijui ok niambie unaenda wapi.!?"

"Naenda kumfunza mtu adabu alienidhalilisha alafu nikirudi huko nitakuwa nimeacha kila kitu najua hupendi kuniona nafanya haya lakini hili ni la muhimu sana kwangu"
     Stephan hakutaka maneno mengi baada ya kuzungumza hayo alitoka nnje na moja kwa moja alichukua gari yake na kuingia mtaani ila haikujuliakana alikuwa na jukumu gani usiku huo.

Muda ulikuwa ukiyoyoma taratibu lakini inapata saa saba usiku Ochu alikuwa nyumbani kwake kwenye kitanda kikubwa cha sita kwa sita huku pembeni amezungukwa na wanawake wengi waliokuwa utupu.

Chumba hicho kilisheheni mabinti wazuri vinywaji vya kila aina na wimbo laini ulikuwa ukichukua nafasi yake, ama kwa hakika Ochu alijua kula maisha.

Wakati hayo yanaendelea huku nnje Stephan alikuwa tayari amefika na kama ambayo aliwahi kuapa kuwa atamuonyesha na kumfunza adabu Ochu kwa kitendo cha kumpiga na chupa basi leo aliona ni muda muafaka wa kumaliza alichoanza Ochu.

"Sahamani bro huruhusiwi kuingia humu bila appointment yeyote"
      Alizungumza mlinzi wa nyumba hiyo baada ya kufungua geti ambalo lilikuwa limegongwa na Stephan.

Kiza kilikuwa kimetawala eneo hilo hivyo Stephan alishindwa kuonekana sura yake vizuri na hiyo ilimpa ujasiri wa kufanya yake bila kujulikana.

"Naona leo una siku mbaya sana mlinzi kwahiyo nakupa nusu kaputi utaamka baada ya masaa mawili"
      Stephan baada ya kuongea hivyo alirusha ngumi nzito iliyompata vyema mlinzi na kupoteza fahamu.

Alipata njia kuingia ndani na taratibu alianza kujongea huku akiifunga bastora yake kiwambo cha kuzuia sauti pindi akifyatua risasi na siku hiyo naweza kusema ilikuwa siku mbaya kwa Ochu ambae alikuwa busy kunywa na kuwatumia watoto wa kike kadri awezavyo.....ITAENDEIA.....

Je unafikiei nini kitafuata hapo maana mambo ni moto sasa sijui kama Stephan ataweza kweli kumuua Ochu au laa lakini nikusihi tukutane sehemu ya 19 kwa majibu ya maswali yako