Jina....TABASAMU LA UCHUNGU
Mtunzi....... Official Dully
Mkasa....wa...kusisismua

            Sehemu Ya {17}

ILIPOISHIA..

Wakati story zimepamba moto walisikia honi ya gari nnje hivyo Sasha alijua tu atakuwa Stephan, alitoka haraka kwenda kufungua gati na taratibu gari iliingia ndani lakini iliposimama na kushuka Stephan ilimfanya Sasha afurahi sana lakini alistaajabu mrango wa pili ukifunguliwa na kusubiri kumuona nani atashuka.....ENDELEA...

Macho ya Sasha yaliganda kumtazama mtu ambae atashuka kwenye gari la Stephan lakini alikuja kupigwa na butwaa baada ya kumuona Tresha, alibaki haamini na kitendo hicho kilimuuma sana kumuona Tresha hapo maana alijua tayari hana chake.

"Haya we kenge umefuata nini kwenye hii nyumba, si nimekwambia ukae mbali na Stephan sasa umekuja kufuata nini hapa.!?"
     Sasha aliona amtolee uvivu Tresha maana alijua tayari amepokonywa tonge mdomoni hivyo hata akikaa kimya haitasaidia kitu..

Tresha nae kwa dharau alifanya kama hamsikii, alimsogelea Stephan na kumshika mkono kisha kuingia nae ndani ambapo kulikuwa na wazazi wa Stephan wameketi huku wakiongea mambo yao kama wanandoa.
      Stephan aliingia akiwa amemshika mkono Tresha na hata wazazi wake walipomuona waliacha kuongea walivyokuwa wanaviongea na kumtazama binti ambae aliongozana na kijana wao Stephan.

Kwa upande wa mama Stephan alipomuona Tresha alijikuta akiboeka maana alijua huyo ndiye binti anaeutesa moyo wa mtoto wake ila kwa baba alionekana kutabasamu na kumkaribisha vyema sana.

"Karibu sana binti, karibu sana jisikie upo nyumbani bhana"
     Baba Stephan alimkaribisha Tresha kwa furaha na uchangamfua lakini kwa mke wake akibaki kubinua mdomo.

"Asante baba nimekaribia sh'kamoo"

"Maharaha nwanangu karibu sana bhana maana tulikuwa hatukai kwa raha kila siku Stephan anatusumbua ooh namtaka Tresha arudi ooh sijui nini na nini nitaenda kumtafuta na kweli ametimiza alichokisema hatimae upo hapa karibu sana mwanangu"

Baba Stephan kwa kiasi fulani alionekana kumkubali sana Tresha maana kwa jinsi alivyokuwa akimchangamkia haikuwa hivyo kwa Sasha ambapo muda mwingi alikuwa mkimya akimtazama.

"Sh'kamoo mama"
       Tresha ilibidi atoe salama na upande wa pili kwa mama Stephan ambae alibinua mdomo na kugeuka pembeni kisha aliitikia kwa jeuri sana lakini Tresha hakujali hilo yeye kikubwa amefika hapo na kupokelewa vizuri.

"Baba, mama najua huyu binti mnamfahamu ndiye binti ambae amefanya mpaka mimi nipo hai na kama nilivyosema ndiye mwanamke ninaempenda sana kwahiyo nao........"
     Stephan alizungumza lakini kabla hajamaliza mama yake alimkatisha na kuanza kufoka maana aliona akikaa kimya mwisho Sasha atakuwa hana chake.

"We..we..weeee tena unyamaze, mwanamke mwanamke kwani amekuwa dhahabu huyo, sasa kwa taarufa yako najua umemleta hapa kwa lengo la kumtambulisha lakini mimi nasema simkubali"

"Lakini ma...."

"Hata mimi nina mama yangu na nishasema simtaki kwahiyo kama ambavyo mmeingilia kupitia ule mrango basi mtoke na mrango ule ule sipokei wanawake wa hovyo hapa wasio na maadili"
      Mama Stephan alikuwa kapanic lakini Tresha hakumjibu chochote japo alikuwa anaumia lakini ukimya ndio ulikuwa jibu kwake.

"Mke wangu sasa naona unanipanda kichwani, kila siku nakuangalia tu unavyojiamuliaga mambo kama wewe ndio mume ila sasa nikwambie mimi nafuata maamuzi ya mwanangu na kama huyu binti anampenda basi na mimi nimempenda"

"Lakini mume wangu mbona binti mwenyewe hana maadili huyu, pia anaonekana hata roho ya utu hana alafu bado unamkubali tu hivi....."

"Basi inatosha sasa unanizoea, haya niambie ni binti yupi ambae hana maadili na utu, kwanza kumbuka huyu unaesema hana utu ndiye katoa figo kumuokoa mwanao ingawa yule unaemuona ana utu alikuwa kimya akimtazama daktari"

"Haya tuachilie hapo huyo unaesema ana maadili hebu tazama nguo anazovaa hata mbele ya wakwe zake ni nguo za ajabu ajabu sana, ukiongea kitu anataka mbishane ilhali huyu amekaa kimya hakutaka hata kukohoa kwahiyo nani mwenye maadili na utu hapo.!?"

Baba Stephan siku hiyo alikaza buti, alishikilia msuli kumtetea Tresha lakini yote hayo yanaendekea Sasha alikuwa mrangoni amesimama akiwasikiliza huku machozi yakimtoka na mwisho aliona sogee na kusema kitu.

"Jamani inatosha hakuna haja ya kuendelea kuzozana ingawa mtu anafanya maamuzi kwa kulingana na moyo wake unasema nini, kama Stephan anampenda huyo mwanamke basi msikilizeni, mpeni haki yake msimbanie"
       Sasha aliongea kwa kujikaza na mwisho aliona aingie chumbani ili kuchukua begi aondoke lakini Tresha alimzuia.

"Hebu subiri kwanza dada Sasha...mimi napingana na maneno yako, najua vijana wa kiume ni wabishi kukubali mara moja ila mimi kama ningekuwa Stephan ningesikiliza maneno ya wazazi wangu kwahiyo mimi nakuachia Stephan wako najua unampenda sana hivyo sina budi kukuachia furaha ambayo uliichagua"

Maneno ya Tresha yalitoka kinywani kwa maumivu lakini hakuwa na budi aliona ampe Sasha alichokuwa anakihitaji kuliko kumvunja moyo.
     Hakutaka tena kuendelea kubaki hapo, aligeuka na kuondoka zake lakini Stephan alimfuata na kumshika mkono.

"Hivi Tresha unaugua uchizi eeh, unajua jinsi gani nakupenda alafu na wewe unafanya nini sasa au....!!"

"Inatosha sasa Stephan unajua sioni haja ya kuwa kwenye nahusiano tena, kama unavyofahamu mama ni mama na mama akichukia hata mapenzi yetu yatakuwa kwenye mgohoro na matatizo kwahiyo sasa nimeona niwaache"
      Tresha masikini alijikaza kuongea huku mchozi yakimshuka na kupelekea hata Stephan amwage machozi lakini mwisho alitoka hapo na kukimbilia nnje.

Stephan kwa hasira alirudi mpaka alipo mama yake na kuanza kufoka maana aliona wanataka kumpanda kichwani ingawa sio lazima kuoa mwanamke wanaomtaka wao.

"Sasa naona mama unahisi furaha sana binti yule akiondoka kwa huzuni ila acha nikwambie mimi sitaruhusu machozi ya Tresha yaanguke mbele yangu, nitakwenda kuishi na Tresha na hutaniona hapa mpaka naingia kabulini"

"Stephan ndio maneno gani hayo....!?"

"Ndio nishasema sasa na sibadili kauli yangu"

Stephan aligeuka na kutoka mpaka nnje ambapo alimkuta Tresha akitoa begi lake kwenye gari ili kuondoka, alimfuata haraka na kumshika mkono kumzuia.

"Tresha nini sasa na unakwenda wapi, inamaana umesahau zile ahadi zako ulizoweka kwangu kwamba utaishi na mimi daima hata itokee mtu wa kututengenisha alafu ni jana tu umeweka iyo ahadi lakini leo ulivyo mkatili unaivunja!"

"Lakini Step....."

"Sitaki kusikia Stephan wala nini, nakuomba urudi kwenye gari twende nyumbani"

Tresha hakuwa na jinsi kurudi kwenye gari na safari ilianza kuelekea nyumbani kwa Stephan lakini siku hiyo Stephan alikuwa amechukia sana sio kidogo.

                 ***************

Ndugu jamaa na marafiki wa karibu walishtushwa na taarifa za shangazi kufa ghafla, haikujulikana kifo chake kimetokana na nini hata walipoenda kupima hospital hawakuona nini kimemuua lakini maswali ya watu yaligeukia kwa mume wake ambae ndiye aliekuwa akiishi nae nyumba moja.

Mume wake hakutaka kuficha kitu alieleza nini kimemuua na ndipo ikawa gumzo kwa watu lakini hawakutaka kuchelewa kufanya mazishi yalifanya haraka bila Tresha na ilipotimu majira ya jioni ndipo Tresha alipelekewa taarifa.

Siku hiyo Tresha alikuwa busy jikoni kuandaa chakula na Stephan alikuwa busy akitazama runinga lakini muda huo huo Stephan alisikia geti likigongwa, aliinuka na kwenea kufungua ila alikutana uso kwa uso na mume wa shangazi.

"Eheee umerudi tena wakati nilikuonya usikanyage hapa haya umefuata nini.!?"

"Ah sijaja hapa kukukwaza wala kuomba chochote kutoka kwako ila nilitaka kuonana na Tresha kuna habari nilitaka kumpa"

"Tresha yupo busy hawezi kuonana na wewe"
       Stephan alijibu short na kutaka kufunga geti lakini mjomba alizuia.

"Basi subiri kama haiwezekani kumuona mpe hizi taarifa ya kwamba shangazi yake amefariki na tayari tumezika kwahiyo shangazi yake hatunae tena duniani"
      Mjomba alitoa taarifa hizo kwa majonzi ambazo zilimgusa kiasi fulani Stephan akiwa kama mwanadamu lakini mwisho alitoa pole, alifunga gati na kurudi zake ndani ili kumpa taarifa Tresha.

Tresha alikuwa hana ili wala lile, alifanya kazi kwa furaha zote lakini wakati anaandaa chakula mezani alimuona Stephan amepoa sana na sio kawaida yake hivyo alihisi kuna jambo linaendelea sio la kawaida na kuamua kumuuliza.

"Unaweza kuniambia nini kinakusumbua.?"
      Tresha alimtupia swali Stephan lakini Stephan alikuwa mbali sana kimawazo alikuwa akiwaza kama atampa taarifa hizo Tresha atakuwa kwenye hali gani.

"Stephan mpenzi.!?"

"Eeeeh ah una...unajua ni am amna ila mjomba yako alikuja na kuniletea taarifa mbaya ambayo najifikiria kama nitakwambia utakuwa katika hali gani"
     Maneno ya Stephan yalimfanya Tresha ashtuke kidogo na kuketi chini ili kusikia vizuri ni taarifa gani.

"Taarifa gani hizo amekueletea hebu niambie kwanza maana unanipa wasiwasi unajua.!?"

"Ah ni kwamba shangazi yako amefariki usiku wa kuamkia leo na tayari wamefanya mazishi hivyo ukiwa kama mtoto aliona afikishe taarifa hizi kwako"

Taarifa hizo zilimshtua Tresha kwa kiasi fulani lakini baadae alinyoosha mikono juu kushukuru Mungu huku akitabasamu.

"Nashukuru Mungu kwa kumuondoa huyu kiumbe maana bila hivyo ningepata dhambi kwa kumuua kama ambavyo aliua wazazi wangu"
        Maneno yaliyomuacha Stephan mdomo wazi yalitoka kinywani kwa Tresha na kuamua kumuuliza.

"Unataka kusema shangazi yako ndie kaua wazazi wako, sasa kwanini muda wote hukuenda kufungua kesi polisi ulikaa kimya?"

"Nilikuwa nakusanya nguvu kwanza maana mwanamke ni mshenzi sana yule, amewekea wazazi wangu sumu kwenye chakula kwa tamaa ya mali alafu kipindi kile nilikuwa mdogo miaka kumi lakini sasa nilisubiri kupata pesa nimmalize lakini Mungu amemchukua hapa sasa nitaishi kwa amani"

"Pole sana Tresha ndio maisha hayo na maisha ni changamoto so usijali kila kitu kipo sawa kipenzi"

Stephan ilibidi amtulize Tresha lakini wakati huo huku kwa Joyce alikuwa tayari amekata tamaa ya kumpata Stephan baada ya taarifa kutoka kwa Daniel kumjia na kumjulisha kwamba Stephan anataka kuoa.

Hakutaka kukubali alipiga tena simu kwa Daniel kuhakikisha huenda alikuwa anamtania lakini jibu lilikuwa ni lile lile kwamba Stephan anaenda kioa.

"Kwahiyo mimi niliekuwa nampenda inamaana ndio nimeachwa njia panda au, mbona kama sielewi jamani.!?"

"Ndio utaelewa mwaka huu lakini ukweli ni huo Stephan anataka kuoa na hivi punde kadi zitaanza kusambaa kwahiyo jiandae kupokea kadi inayohusu bwana Stephan na bi Sasha"

"Ok sawa acha tuone hiyo ndoa kama itatimia"
      Joyce alikuwa tayari amezira kwa hasira na yote hayo yanaendelea Stellah alikuwa akiyatazama lakini mwisho aliondoka zake kwenda kupeleka umbea kwa mama yake.

                 ****************

Maisha yalianza kusonga taratibu lakini upande wa Gidion aliachiwa huru baada ya polisi kusubiri sana na kuona hakuna dalili yeyote ya Stephan kufika wala kupiga simu hivyo walimuacha na Gidion alivyotoka akili yake ilikuwa ni ile ile.

"Daaah nimekaa ndani week nzima mpaka nimeimiss hewa ya nnje lakini sio mbaya nilienda kupumzika kwa muda sasa mambo yanaanza upya lazima Tresha awe wangu na awamu hii yule mpuuzi akileta kujifanya mwaname wa shoka basi nitamuua"

Yalikuwa ni mawazo ya Gidion wakati huo alikuwa njiani kuelekea mgahawani kwa Tresha bila kujua tayri alikuwa ameondoka.

Alifika na kukuta wateja wamejaa kama kawaida kwenye mgahawa huo, alimuomba Shakira wazungumze kidogo na Shakira hakupinga ilibidi amsikilize.

"Kwahiyo unataka kusema Tresha ameondona na yule mpuuzi.!?"

"Ndio wameondoka kesho yake baada ya lile tukio kwahiyo kama unamuhitaji basi hapa hayupo na hawakuniambia wameenda wapi"

"Ok basi sawa pia sanate kwa msaada wako"

 Gidion aliondoka zake na alijua wapi atampata Tresha lakini alipoondoka tu huku nyuma Shakira alipiga simu kwa Tresha lakini simu ilikuwa haipatikani, kitendo kilichomfanya ogope sana na kukosa amani maana alijua kinachofuata ni balaa.

Majira yalianza kuyoyoma taratibu na ilipofika saa moja siku inaelekea saa mbili ndipo Tresha aliwasha simu na kukuta missed call takribani kumi kutoka kwa Shakira na jambo hilo lilimfanya aingiwe na wasiwasi sana.

"Kuna tatizo gani mbona Shakira amepiga simu kiasi hiki hebu kwanza nimpigie huenda kukawa na tatizo kubwa limetokea"
      Aliingia upande wa contact na kutafuta namba ya Shakira kisha kumpigia na haikuchukua muda ilipokelewa lakini bila salamu Sahkira alianza kuongea.

"Sasha yule mwanaume namaanisha Gidion amekuja kukuulizia na baada ya kukukosa amesema anakutafuta kwahiyo mimi najua yatakukuta matatizo wewe na shemeji sasa cha kufanya mjilinde"

"Laki......."
       Wakati Tresha anataka kuongea alisikia geti likigongwa kwa nguvu na alijua lazima atakuwa Gidion amefika hivyo hakutaka tena kuendekea kuongea na simu alikata na kubaki akiwa ameduwaa.

"Ah nani tena anagonga geti kwa fujo mbona anashindwa kuwa na adabu.!?"
      Stephan alijisemea huku akiinuka lakini Tresha alimshika mkono maana alijua kinachofuata huko ni kifo na sio kingine.

"Stephan usiende kufungua ni Gidion huyo umefika, nimepokea simu kwa Shakira amesema mchana alikuwa anatuulizia kwahiyo naamini atakuwa ni yeye amefika sasa nakuomba usiende kufungua jamani.!!"

"Hebu acha niende nitajua mimi nakabiliana nae vipi."

Stephan kwa ujasiri aliinuka ili kwenda kufungua lakini upande wa nnje aliefika alikuwa ni Gidion kweli tena alikuwa na rungu kubwa ambalo aliona ni silaha tosha kumkabili Stephan, aligonga tena geti na baada ya kusikia hatua za mtu anakuja kufungua alijificha ili akitoka ammalize kama atakuwa Stephan......ITAENDELEA.....

Unafikiri nini kitafuata hapo...Je Gidion atakamilisha alichokusudia au laa...mimi sijui ila majibu ya maswali yako tukutane sehemu ya 18 ya mkasa huu wa kusisimua na kuburudiaha pia simulizi hii imebaki ep 3 kukamilika na kuisha kabisa..