Jina....TABASAMU LA UCHUNGU
Present.......Story Za Mapenzi
Mkasa....wa...kusisismua

            Sehemu Ya {16}

ILIPOISHIA..

Gidion alijikuta akishikwa na hasira ghafla, hakujali kama anampenda Tresha au laa, alimsukuma mpaka chini huku watu wakishudunia na hakuna hata mmoja alieweza kuingilia ugomvu huo, kipigo kilianza kushuka kwa Tresha lakini wakati Gidion anahitaji kumpiga kofi jingine Tresha kuna mtu alifika na kuushika mkono wake....ENDELEA.....

Kila mmoja alibaki kushangaa na kujiuliza ni nani aliefika hapo kumsaidia Tresha lakini kitendo cha Gidion kushikwa mkono aligeuka haraka ila alijikuta akipata mshtuko baada ya kumuona Stephan ndiye aliefika hapo na alimkumbuka ndiye mtu aliempiga risasi.

Pia hata Stephan alipomuona Gidion alishangaa sana nae alimkumbuka ni mtu aliemsababishia matatizo makubwa sasa ikawa mafahali wawili wamekutana.

"Kumbe ni wewe mshenzi.!?"
        Stephan alizungumza huku bado ameukamata mkono wa Gidion na wakati huo hakutambua kama aliekuwa anapigwa ni Tresha ila yeye alitetea kwakuwa aliona mwanamke akionewa.

"Hebu niache mkono wangu tafadhali kwasababu kama utaendea kuushikilia yatakukuta makubwa sasa ili yasikukute makubwa naomba uachie mkono wangu.!?"

"Ahaaa kama unafikiri unao ubavu juu yangu basi nitakuachia lakini lazima leo uingie mikononi mwa polisi na nitakufungulia kesi muuaji mkubwa wewe"

Stephan alikuwa hatanii, aliukamata mkono wa Gidion ipasavyo lakini alipotupa macho kutazama binti aliekuwa chini alistaajabu kumuona Tresha na ndiye mtu aliekuwa anamfuta hivyo alijikuta akimuachia Gidion na kumkimbilia Tresha ambae nae alikuwa haamini kumuona Stephan hapo.

Gidion aliona hiyo ndio nafasi ya yeye kutimka lakini kabla hajalifika gari lake polisi walikuwa tayari wamewasili eneo hilo na kuziba kila upande kuhakikisha gari ya Gidion aiende sehemu yeyote na aliechukua jukumu la kupigia polisi alikuwa ni Shakira.

"Tresha, umzima kweli kipenzi changu?, oh asante Mungu nimekupata maana nilikuwa nakutafuta usiku na mchana sasa sijui kwaninu ulinikimbia.!?"
      Stephan mpaka machozi yalikuwa yakimtoka na hata Tresha nae alijikuta akitokwa na machozi huku akimtazama Stephan tumboni kwake.

"Mimi nipo salama kabisa sijui wewe oparesion yako imeendaje maana niliondoka na kukuacha hata sijui hali yako.!?"

"Nipo salama pia asante sana kwa kuokoa maisha yangu maana bila wewe nisingekuwa hapa mbele yako lakini kwa ujasiri wako na moyo wa huruma uliojaa upendo umeweza kunisaidia mpaka leo napumua"

"Nakupenda sana Stephan.!"
       Tresha uvumilivua ulimshinda, alimrukia Stephan na kumkumbatia huku akimpiga mabusu mengi yasiyo na idadi ila yote hayo Gidion alikuwa akitazama huku akiwa chini ya ulinzi wa polisi.

Basi Stephan aliinuka na kuwasogelea polisi kisha alimfuata polisi mkuu na kumpa taarifa za matukio aliyofanya Gidion.

"Afande mimi nahitaji kumfungulia kesi huyu mtu kwahiyo nawaomba mfikisheni polisi kesho mapema sana nitakuja na mwanasheria tutafungua kesi"
     Stephan hakutoa maneno tupu, alitoa kitita cha pesa na kumfinyia polisi bila wenzake kujua maana aliona hivihivi bila kumpa hongo hatoweza kufanikisha anachotaka.

Polisi walifanya kazi yao, walimchukua Gidion na kuondoka nae, Stephan alimrudia tena Tresha na kumshika mkono maana alimmiss sana.

"Tresha unajua nipo na njaa sana hapa na nimekuja hapa baada ya kuelekezwa kwahiyo kamata hii pesa niwekee chakula cha kushiba"

"Mh hapana bhana mpaka wewe nikuuzie si nitakuwa kichaa, wewe njoo uketi hapa, chochote unachotaka nitakupa hata sahani kumi utakula lakini sio kupokea pesa yako kipenzi"
       Tresha alijongea na Stephan mpaka ndani ya mgahawa wake, alimtafutia sehemu nzuri na kumuoba aketi kisha alimuandalia chakula na kumpatia.

Wakati Stephan anakula alisogea na kuketi kando yake akimtazama maana alikua kammiss sana pia alikuwa akimpenda sio kidogo.

"Shakira hebu njoo nikutambulishe kwa shemeji yako maana nisije kuzubaa alafu kesho na keshokutwa nikakuta nae uchochoroni"
     Tresha alizungumza huku akiwa mtu wa furaha tele, Shakira alisogea na kutambulishwa kisha story hapa na pale zilianza.

"Ila shemeji yangu ni handsome sana mpaka natamani nikuibe Tresha asikuone"

"Hahaha Shakira mimi sipendi bhana, ujue nina wivu sana kwahiyo niache tafadhali niache na Stephan wangu wewe nenda kaendelee kupika na kuhudumia wateja"

"Ok sawa"

Basi siku hiyo ilikuwa ni furaha kwa wapendanao wawili hata usiku ulipowadia Stephan hakutaka kurudi kwake, alichukua gari yake na kwenda kuiweka kwenye parking za kulipia kisha alilala kwa Tresha na siku hiyo walilala kitanda kimoja kwa mara ya kwanza.

"Stephan unajua mimi sikukukimbia au kukutelekeza lakini yule mwanamke mweusi aliekuwa na wazazi wako amesema unataka kunipeleka jela kwahiyo akaniambia kwa usalama wangu niondoke kwenda mbali na wewe sasa unafikiri ningefanyaje.?"

"Yaani yule mwanamke simpendi hata kidogo na mbaya zaidi kasema yeye ndie kanitolea figo kumbe ni wewe kipenzi changu daah hawajakufanyia wema kabisa"

"Ah usijali lakini kaniambia wazazi wako wamemuhalalisha kuwa mchumba yako na hivi punde mtafunga ndoa"

"Mh hapana bhana mimi nakupenda wewe na kesho nahitaji turudi nyumbani kwahiyo kama kukuoa nitakuoa wewe pia hii biashara hutafanya tena umuachie Shakira wewe nitakwenda kukufungulia duka kubwa la nguo na urembo"

"Wow basi itapendeza lakini sihitaji kumuona yule mwanamke"

"Kwa hilo usijali mpenzi"

Basi story za wapenzi hao zilikuwa nyingi sana lakini baadae walijikuta wakianza kuchombezana na mwisho wakiingia kwenye ulimwengi wa mahaba mazito ambayo yalifanya kila mmoja afurahie na kuburudika.

                 ***************

Wakati usiku huo wapenzi wawili wakiwa kwenye kisiwa cha huba huku shangazi alikuwa amejifunika shuka na kuwasha moto kwenye chungu kisha alianza kuweka vitu huku akilitaja jina la Tresha.
     Alifanya hivyo kwa takribani dakika mbili lakini ghafla alianza kukohoa na kujikuta akiishindwa kupumua vizuri.

Kilikuwa ni kitendo cha ghafla sana, alifunua shuka akiwa na imani huenda akapumua vizuri lakini mambo baado mambo yalikuwa vile vile na mwisho alianza kupika kelele kumwita mume wake ambae alifika na kumkuta mke wake kwenye hali mbaya sana.

"Na...nakufa mume wangu nisaidie.!!"

"Shida nini mke wangu hebu niambie mbona nashindwa kukuelewa.!?"

Shangazi kila dakika zilivyozidi kwenda ndivyo alizidi kukosa pumzi na mwisho kabisa alijikuta akianza kulegea na mwisho alizima hapo hapo.

"Mke wangu...mke wangu..!!?"

Shangazi aliamshwa na kuamshwa lakini alikuwa kimya na mwisho mapigo yake ya moyo yalisimama kuashiria tayari roho ilikuwa imeachwa mwili.

Kilikuwa ni kitendo cha ghafla sana ambacho kilitokea hapo pia kilikuwa ni kigumu kuaminika lakini ukweli shangazi alikuwa amekufa na huo ukawa mwisho wake ambao ulisindikizwa na kilio kizito kutoka kwa mume wake.

Mambo yalikuwa magumu kwa mume wa marehemu pia hata Sasha alikuwa na wakati mgumu maana usingizi hakupata kabisa, alipiga namba ya Stephan ili kujua yupo wapo lakini namba ilikuwa haipatikani.
     Hakuchoka alipiga tena na tena ila mwisho aliona ampigie mama mkwe wake mtarajiwa ili kumjuza kile kinachoendele.

"Kwahiyo mpaka sasa hajarudi.!?"

"Ndio mama alafu nikipiga namba yake haipatikani sasa sijui yupo kwenye hali gani ananipa wasiwasi sana jamani.!"

"Usijali mwanangu atarudi tu maana jiji zima analijua vizuri pia ni mtu mzima yule kwahiyo hatoweza kupotea atarudi sawa eeh.?

"Sawa mama"
         Sasha kishingo upande aliitika lakini alijua hana chake tena ila alifanya kufosi huenda Stephan au wazazi wake wakamfosi akakubali kumuoa.

               *****************

Siku iliyofuata mapema sana Tresha alimuamsha Stephan ajiweke safi na baada ya kumaliza alipakia nguo zake kwenye begi kisha walitoka na kuanza kuaga baadhi ya majirani lakini kwa upande wa Shakira ilikuwa ni kilio maana alimzoea sana Tresha.

"Usilie sasa dadaangu unajua ukilia hupendezi, mimi sio kwamba nakufa au naenda nje ya mchi lakini mimi naenda kwa mpenzi wangu tena ndani ya jiji hii hii kwahiyo ipo siku nitakuja kukutembelea alafu simu tunazo tutakuwa tunawasiliana na nitakuomba uje ninapoishi kwahiyo usilie sana pia kuhusu ule mgahawa wewe chukua na hiki chumba pia chukua kila kitu chako sasa"

"Asante sana Tresha"

"Basi kwaheri"

Tresha aliaga huku nae roho ikiwa inamuuma sana lakini hakuwa na jinsi ilibidi aondoke kurudi kwa mtu ampendae.
     Walifika kwenye parking na kuchukua gari lakini walipopanda kitu cha kwanza Stepha alimuomba Tresha waende kwao kwa wazazi wake ili wamtambue.

"Jamanj mbona mapema sana eti.!?"

"Wewe usijali kila kitu nataka kiende haraka bhana kwahiyo hapa safari ni nyumbani kwa wazazi wangu wakutambue mengine yatafuta"

Basi safari ilianza kuelekea nyumbani kwa wazazi wake na gari ilitumia takribani masaa mawili kufika nyumbani kwa wazazi wa Stephan ambao walikuwa busy kuongea na Sasha..

Wakati story zimepamba moto walisikia honi ya gari nnje hivyo Sasha alijua tu atakuwa Stephan, alitoka haraka kwenda kufungua gati na taratibu gari iliingia ndani lakini iliposimama na kushuka Stephan ilimfanya Sasha afurahi sana lakini alistaajabu mrango wa pili ukifunguliwa na kusubiri kumuona nani atashuka.....ITAENDELEA...

Unafikiri nini kitafuata hapo, mimi na wewe hatujui lakini majibu utayapata sehemu ya 17 ya mkasa huu wa kusisimua na mpenzi...