Jina....TABASAMU LA UCHUNGU
Present.......Story Za Mapenzi
Mkasa....wa...kusisismua
Sehemu Ya {15}
ILIPOISHIA..
Mama aliita lakini Stephan hakutaka kugeuka wala kumsikiliza kwa chochote, alitoka mpaka nnje lilipo gari lake na kupanda sasa kilichobaki akilini mwake ni kumtafuta Tresha kwa usiku na mchana kumrudisha tena kwenye himaya yake na ikiwezekana amuoe kabisa.....ENDELEA....
Safari ya Stephan ilimfikisha nyumbani kwa Daniel na bahati nzuri alimkuta hivyo alikaribishwa ndani lakini Daniel alimpomtazama Stephan aligundua hayupo sawa.
"Stephan shida nini mbona nimekukaribisha alafu huongei chochote na sio kawaida yako kuwa mkimya au kuna vitu vimekuchanganya.!?"
Daniel ilibidi amuulize Stephan ambae alijikuta akicheka.
"Yaani rafiki yangu hata wewe unanificha, wewe wa kuniambia Sasha ndiye amenitolea figo wakati alienitolea ni Tresha daah hapa naamini maneno ya wahenga ya kwamba rafiki yako ndiye adui yako"
"Ah unajua Stephan sio hivyo mimi nilitaka kukwambia pindi ukiamka lakini siku hiyo ambayo nimewaza hivyo usiku nilipigiwa simu na Sasha akaniomba nisikwamnie sasa unafikiri mimi ningefanya nini"
"Ahaaa kwahiyo wewe unaona wanawake wa maana kuliko mimi mshkaji wako, alafu kama ulikuwa hujui leo kesho wewe ukifa mimi ndiye nitabeba jeneza lako na sio mwanamke lakini aina mbaya"
Stephan siku hiyo alijikuta mnyonge sana na kwa kiasi fulani aliona kama wememtenga, alikaa hapo kwa takribani dakika tano kisha aliinuka na kuondoka zake bila kuaga na safari yake ilikuwa ni kuelekea sheli kujaza mafuta na jukumu la kumtafuta Tresha lianze.
Wakati huo yapata kama saa nne usiku inaelekea saa tano lakini hakujali ila alichoona yeye na alichokuwa anahitaji ni kumpata Tresha na sio kingine.
"Daaah jiji hili ni kubwa sana sasa sijui nianzie wapi niishie wapi mbona ni balaa tena hili jamani.!?"
Stephan alianza kutafakari wakati huo gari tayari ikiwa full tank kwaajili ya kuanza safari kumtafuta Tresha.
"Ila acha kwanza nianzie kaskazini najua atakuwa mitaani tu hana sehemu yeyote ya kwenda"
Stephan baada ya kupata shauri ndani ya kichwa chake basi alikanyaga mafuta na kuingia mitaani kwa mwendo wa taratibu sana kuhakikisha Tresha anampata.
Huku kwa wazazi wake ilikuwa ni huzuni kwa Sasha maana alijua kama tayari siri yake imefichuka kinachofuata ni kukosa ndoa.
"Usijali binti yangu mimi kama mama najua atanisikiliza na atakuoa kwahiyo ondo ashaka kabisa hata usiwe na wasiwawi mamaangu"
Mama Stephan alichukua jukumu la kumbembeleza Sasha ambae alikuwa akilia bila kukoma lakini mume wake alikuwa akimtazama na mara nyingi hua sio mtu wa kuongea sana.
"Mama mimi najua hawezi kunioa kabisa alafu tayari kasema atamuoa huyo Tresha sasa bado unanipa moyo ili iweje wakati mambo yamewekwa wazi.!?"
Tresha masikini alizungumza huku akimwaga machozi na kujikuta akijutia kwanini aliongopa.
"Hapan binti yangu unajua Stephan tumemlea kwenye mazingira ya maadili na adabu kwahiyo anatakiwa kumpata mwanamke mwenye maadili na adabu na mwanamke mwenyewe ni wewe kwahiyo sitaruhusu aoe mwanamke mwingine zaidi yako"
"Kweli mama.!?"
"Yah kweli wewe ondoa shaka mwanangu kila kitu kitakuwa sawa wala usijali"
Maneno ya mama Stephan yalirudisha matumaini kwa Sasha na kujikuta akitabasamu na kumkumbatia.
Basi taratibu majira yalianza kusonga mpaka inatimu saa sita usiku Stephan bado alikuwa mtaani na usingizi ulikuwa umejaa kichwani kwake ilifika wakati nusu kuingia kwenye mitaro kutokana na kutozingatia anapoenda.
"Ah sasa huu usingizi unaweza kuniingiza kwenye matatizo acha tu nitafute hotel nipumzike alafu asubuhi niingie mitaani kwa mara nyingine.
Stephan aligeuza gari lake na kurudi nyuma kidogo ambapo kuna hotel aliipita na kwenda kuchukua chumba kwaajili ya kupumzika.
Chumba alipata lakini alipoingia chumbani na kujilaza kitandani usingizi uligoma kuja kwa wakati huo maana akili yake ilikuwa ikimuwaza Tresha asijue yupo katika hali gani amekufa au ni mzima.
Hata upande wa Tresha muda huo alikuwa hajalala maana mawazo yake yalikuwa kwa Stephan, hakufahamu kama tayari amepona au bado anaendelea kuuguzwa, atakuwa amekufa au mzima maana mara mwisho aliondoka bila kujua hali yake inaendeleaje kiufupi bado alikuwa anampenda Stephan.
"Lakini kwanini Stephan alitaka niende jela mbona aliempiga risasi ni mwingine na sio mimi.!?"
"Ila sawa kama ameamua hivyo acha niendelee na maisha yangu ila atakuja kunikumbuka naimani hilo siku moja"
Basi Tresha hakuwa na jinsi alivuta shuka na kulala huku pia hotelini Stephan alivuta shuka na kulala mpaka kunapambazuka.
****************
Asubuhi na mapema Stephan alikuwa wa kwanza kuamka mpaka wahudumu walimshangaa maana haikuwa kawaida mteja kuamka mapama hivyo, alipata kifungua kinywa na baada ya kumaliza aliingia mitaani lengo lake lilikuwa lile lile.
Tresha nae aliamka mapema sana na kuelekea kilipo chumba cha shakira maana kila mmoja alikuwa analala kwenye chumba chake.
"Shakira hebu amka muda tayari huu wa kwenda kuanza biashara alafu kumbuka leo ni jumaa tatu pilika ni nyingi kwahiyo tukichelewa tutakosa pesa nyingi sana"
"Aya nakuja tangulia"
Shakira kwa sauti ya uchovu na iliyojaa usingizi alijibu lakini Tresha hakutaka kwenda maana alijua kama atamuacha ataendelea kulala hivyo alimpigia kelele mpaka Shakira aliinuka kitandani na kufungua mrango.
"Yaani Tresha una mikelele jamani.!?"
"Sawa nina mikelele lakini uamke muda tayari huu hakuna kulaza damu mama"
"Ok sawa lakini Tresha jana uliponiacha ukaondoka si yule mkaka alirudi tena"
"Mkaka gani.!?"
"Yule bhana sijui Gidion sijui Godi"
"Gidion yule"
"Eheee basi alikuja tena amenikuta nina wateja kibao wamenijalia, alikuulizia lakini nimemwambia kaenda kulala akaniomba nimlete hapa unapoishi ila nimemwambia nipo busy basi kanunua chakula pale kala kaondoka"
"Yaani usisubutu kumleta hata kidogo maana mtu katili yule tena kama ingewezakana jana hata chakula usingemuuzia simpendi hata kumuona pumbavu zake.!"
"Lakini mbona anaonekana ni mtu mzuri tu, mcheshi na hana shaka yeyote"
"Eheee umefika huko tena, haya naomba kaoge tuingie kazini maana tukianza kumchambua yule mpuuzi mwisho tutakesha ila mimi acha nitangulie nikafagie fagie"
Tresha alichukua vyombo vyake nusu na kutangulia kwenye biashara zake kiufupi alipenda sana biashara hiyo na ilimuingizia kipato kikubwa sana.
****************
Muda nao haukuacha kusonga, ilipotimua majira ya mchana Tresha akiwa amejaliwa na wateja ghafla aliona gari imefika na alipoitazama aliifahamu ilikuwa ni gari ya Gidion.
"Jamani samahanini wateja nakuja sasahivi"
Tresha ilibidi awaage wateja na kusogea mpaka lilipo lile gari na muda huo huo Gidion alishuka akiwa mwingi wa tabasamu na mkononi alibeba maua mekundu.
"Habari yako mrambo yaani umependeza sana leo"
Gidion alianza mbwembwe zake lakini Tresha alimsubiri afike karibu yake ili afungulie maneno.
Gidion alifika mpaka karibu na Tresha kisha alimpatia maua lakini Tresha aliyapokea, aliyakunja na kumtupia kisha alionesha kidole sehemu anayotoka Gidion ishara ya kumtaka aondoke.
"Kwahiyo unielewi au mpaka niseme kwa mdomo.!?"
"Lakini Tresha mbona unakuwa mkatili hivyo, tukae chini tumalize tofauti zetu lakini wewe unapenda ukoroni tu"
"Ahaaa mimi katili, unaujua ukatili wewe, sasa nenda tu kabla sijapiga kelele za mwizi watu wakupige mawe ufe"
Wakati hayo mabishano yanaendelea Stephan alikuwa hana ili wala lile, njaa ilikuwa imemshika maaa tangu apate kifungua kinywa asubuhi hakutia tena kitu tumboni hivyo alijikuta akipita sehemu kutafuta hotel lakini hakukuwa na hotel.
"Mh mitaa hii mbona hakuna mahotel makubwa, ok basi acha nitafute hata mgahawa ilimradi tu hii njaa niliyo nayo ikate"
Stephan alijisemea na kupaki gari yake kando ya barabara kisha alishuka na kuanza kuuliza watu wa mtaa huo kama kuna sehemu yeyote anaweza kupata chakula.
"Ah inaonekana ni mgeni mtaa huu humjui Sister T"
"Sister T ndio nani.!?"
"Kuna dada flani mzuri mzuri yupo hapo mtaa wa nyuma anauza chakula ana mgahawa mkubwa sana kwahiyo wewe pita na hii njia hapa utatokea sehemu ya wazi ukitazama mbele utaona mgahawa mkubwa umendikwa Sister T Cafe na pia utaona wateja wengi basi ndio hapo"
"Ok shukrani kakaangu "
Stephan alishukuru baada ya kupata maelekezo hiyo taratibu alianza kufuata njia kama alivyoelekezwa na mwisho kweli aliuona huo mgahawa.
Hakutaka kuchelewa taratibu alianza kujongea ulipo huo mgahawa ili kupata chakula.
Wakati huo mzozo kati ya Gidion na Tresha ulikuwa unaendelea na Gidion bado alikuwa mbishi kuondoka licha ya Tresha kumfokea sana.
"Unajua Tresha hapo ulipo unapiga kelele tu, mimi sitaenda popote na acha niseme kwamba nakupenda"
"Hahaha eti kunipenda basi kampende mamaako kama unaona kupenda ni deal, nishasema sikutaki mbona hivyo wewe"
Tresha alitoa kuli ambayo ilimgusa na kumuuma sana Gidion hasa alipoambiwa ampende mama yake.
"Tresha unasemaje wewe, eti nimpende nani.!?"
"Mamaako"
Gidion alijikuta akishikwa na hasira ghafla, hakujali kama anampenda Tresha au laa, alimsukuma mpaka chini huku watu wakishudunia na hakuna hata mmoja alieweza kuingilia ugomvu huo, kipigo kilianza kushuka kwa Tresha lakini wakati Gidion anahitaji kumpiga kofi jingine Tresha kuna mtu alifika na kuushika mkono wake....ITAENDELEA.....
JE unafikiri ni nani aliefika kumtetea Tresha, vipi Stephan atampata Tresha kwenye harakati zake za kumtafuta....mimi sijui ila majibu utayapata kesho sehemu ya 15.
