Jina....TABASAMU LA UCHUNGU
Mtunzi....... Official Dully
Mkasa....wa...kusisismua

            Sehemu Ya {14}

ILIPOISHIA..

Tresha alimuachia maagizo Shakira na kuondoka zake lakini kitendo cha yeye kuondoka ilifika gari moja ya kifahari na kusimama ambayo ilimuacha mdomo wazi Shakira, baada ya kusimama gari hiyo mrango ulifunguliwa na alishuka Gidion ambae alivalia samart sana......ENDELEA.....

     Shakira alipomuona Gidion alimshangaa pia hakumfahamu ni nani lakini lengo la Gidion kuja hapo ni kuonana na Tresha ili wazungumze na kuyamaliza ikiwezekana waanzishe mahusioano.

"Hello dada habari za hapa.?"
      Gidion alianza kwa salamu huku taratibu akijongea zaidi alipo Shakira ambae alikuwa busy kuandaa vyombo vya kupikia.

"Salama tu karibu"

"Asante nimekaribia"
      Gidion alijisogeza na kuingia ndani ya mgahawa huo kisha alivuta kiti na kuketi.

"Sasa kakaangu mbona umekuja mda mbaya sana maana chakula tayari kimeisha ila kama itawezekana ungetembea tembea au kama kuna shughuli kafanye alafu baadae uje maana ndio tunataka kupika"

"Ah hapana dadaangu mimi sihitaji chakula ila namsubiri Tresha kwasababu nimeambiwa mgahawa wake huu sasa sijajua atakuja muda gani.?"

"Oh kumbe unamtaka Tresha basi msubiri ameenda dukani hapo kuchukua vitu vya kupikia kwahiyo sasahivi atarudi ila wewe ni nani yake.?"

"Ah mimi ni mpenzi wake, nilipotezana nae kwa takribani miezi sasa kwahiyo nimemtafuta jiji zima lakini bahati nzuri nimejua anapofanyia kazi ndio nimekuja"

"Oh sawa basi msubiri anarudi sasahivi hatokawia sana" 
 
"Ok sawa"

Gidion alijieleza vizuri na kufanya Shakira amuelewa ila hakujua Gidion ndiye mtu aliemfanya Tresha kuja kuishi kwenye mtaa huo kuogopa kwenda jela.

Tresha akiwa hana ili wala lile alinunua bidhaa zake zinazohitajika kwa mapishi na kurudi, lakini alipofika karibu na ngahawa wake aliona kuna gari nyeusi imesimama na gari hiyo ilikuwa ya gharama sana lakini kwa upande mwingine alihisi huenda ni mteja maana alikuwa na wateja wengi sana.

"Mh lakini mteja mwenyewe mbona kaja muda mbaya sasa, muda wote alikuwa wapi mpaka anakuja muda huu watu tunaanza kupika.!"
      Tresha alijiuliza maswali huku akijongea kuukaribia mgahawa wake ila hakujua gari hiyo ilikuwa ya Gidion.

Baada ya sekunde kadhaa aliufikia mgahawa wake lakini wakati anaingia alishtuka kumuona gidion na kujikuta akiangusha kiroba cha mchele kilichokuwa kichwani kwake.

"Gidion...umefuata nini hapa mshenzi wewe.!?"
      Tresha aliuliza lakini bado alikuwa kwenye hali ya mshangao na hakufahamu Gidion amefikaje eneo hilo au amejuaje yeye anapatikana hapo.

"Jamani Tresha ndio nini sasa, umeniona unatakiwa kunikaribisha tukae chini tuongee yaishe ili tuendeleze mapenzi lakini unavyoanza kufoka na kunitukana inakuwa haipendezi.!"

"Sijali na nitaendelea kukutukana mpaka uondoke muuaji mkubwa wewe, wewe ndie chanzo cha mimi kuishi maisha haya na kuniweka mbali na mtu nimpendae kwahiyo sitamani hata kukuona naomba uende"

"Lakini Tre......!"

"Sitakiiiii nimesema uende kwanza jina langu kutamkwa kwenye mdomo wa muuaji kama wewe ni kuniletea nuksi kwahiyo naomba uende tafadhali"
     Tresha alishikilia haswaaa kauli yake ya kumtaka Gidion aondoke kiufupi hakutaka kumuona kabisa machoni mwake.

"Ok sawa naenda ila nitarudi tena kwaajili yako kwahiyo elewa hilo na utambue mimi ni wako na nitakuwa wako"
     Gidion alirudi kwenye gari lake na kupanda kisha alitoka hapo kwa hasira sana huku nyuma akimuacha Tresha akiongea na kutoa maneno machafu.

"Yaani sijui watu wengine wana nini, mtu umeamua kuwaepuka ili ufanye mambo yako kwa amani na uishi viziri lakini ajabu wanakufuata huko huko ili tu kukuvuruga.!!"

"Pole sana Tresha mdogo kwani kipi ambacho kimekukuta huko nyuma maana inaonekana ni mazito sana.!?"
      Shakira sasa ilibidi aulize ili kujua ukweli kuhusu Tresha na Tresha hakuwa na ajizi ilibidi amsimulie kuanzia mwanzo mpaka hapo alipo.

"Duh kweli umepitia magumu pole sana tena sana ila subiri nikwambie kitu, najua atarudi tena tu kesho kwahiyo kama inawezekana tutoe taarifa polisi ili adhibitiwe la sivyo atakuharibia maisha yako"

"Hata mimi hilo ndilo naliona sasa subiri kesho akija tu ataona wala usijali mbona ataenda kulala polisi alafu hata kuendelea kupika tena siwezi wewe pika mimi acha nikalale bhana"
      Tresha alimuaga Shakira na kuondoka zake maana siku yake imeingia doa.

Wakati hayo yanaendelea huku upande wa Joyce siku hiyo kama kawaida yake alimualika Stephan kwenye chakula cha usiku katika hotel moja kubwa huku maongezi yakiendelea.

"Unajua Stephan tangu upone sikuja kabisa kukuona alafu umshukuru sana yule binti kwasababu bila yeye sijui ungekuwa wapi sahizi"

"Ah ndio hivyo ana moyo wa ushujaa sana kama mwili wake ulivyo mnene na moyo wake mnene wenye ujasiri mkubwa"

"Mh mnene, kwani wewe unamzungumzia binti yupi, mimi namzungumzia yule Tresha ambae ametoa figo kwaajili yako sasa wewe unasema mnene, au umenielewa vibaya.!?"

"Hebu kwanza subiri, kwani alienitolea figo mimi ni nani, ni Tresha au Sasha maana mimi najua kanitolea figo Sasha sasa huyo Tresha tena inakuwaje.!?"
       Stephan alijikuta kwenye mshangao na kuna baadhi ya mambo aliona kama yamejificha.

"Hapana bhana mimi najua yule binti anaitwa Tresha maana siku unapigwa risasi tulikuja kukuona lakini hatukupata nafasi ndipo tukaenda chumba alicholazwa huyo binti na kweli tulimuona ametoka kufanyiwa opareshion sasa huyo Sasha tena vipi au ana majina mawili.!?"

"Hebu kwanza subiri, huyu binti mlieenda kumuona yupoje.!?"

"Ni mrefu kiasi alafu ana mwili namba nane ila sio mnene wala mwembamba, sura yake ya duara na ni mweupe"
      Joyce alimuelezea Tresha kama ambavyo alivyo muona na kumfanya Stephan ashangae maana yeye anajua alietoa figo ni Sasha.

"Sasa kwanini wamenificha hawakuniambia ukweli, inamaana kila siku namuona Sasha wa thamani kumbe muongo sasa subiri"

Stephan alijikuta amepanic maana muda wote alikuwa anafichwa na kuaminishwa kwamba Sasha ndie aliemsaidia kumbe aliemsaidia ni mwingine kabisa, hakutaka tena kuendekea kupiga story, aliinuka na kuondoka zake akiwa mwingi wa hasira sana.

               ****************

Shangazi kama kawaida yake alimfuata mganga mwingine ili kumsaidia atimize anachotaka kwa Tresha, alikaribisha vizuri kilingine na kuanza kueleza shida yake ambayo ilimfanya mganga acheke sana.

"Sasa jamani napatiwa msaada au mbona kama hakuna dalili yeyote ya kupata msaada hapa.!?"

"Hapa hua hatukaribishi balaa"

"Unamaanisha nini mganga kusema hivyo mbona nashindwa kukuelewa kabisa jamani.!?"
    Shangazi alikuwa hamuelewi kabisa mganga huyo lakini ilibidi amuulize maswali ili kujua anamaanisha nini.

"Huyo binti unaemfuatilia ni hatari sana na anaweza kukupelekea umauti kwahiyo kama inawezekana achana nae la sivyo yatakukuta makubwa ukajuta baadae"

"Lakini mganga mbona sasa unitisha au kazi umeshindwa, kama umeshindwa niambie niende sasa ataniletea matatizo gani wakati wazazi wake wamenishindwa na mimi mdie nimewaua"

"Sawa niseme tu kazi imenishinda kwahiyo wewe nenda mamaangu aina shida lakini utakuja kunikumbuka wakati huo upo sehemu mbaya"

Shangazi hakujali maneno ya mganga aliinuka na kundoka zake lakini upande wa pili huku Sasha alikuwa mwenye furaha sana akiwa na wakwe zake watarajiwa yaani wazazi wa Stephan.

Story mbali mbali ziliendelea hasa kuhusu ndoa lakini wakati wakiwa busy kuongea yao ghafla aliingia Stephan akiwa mwenye hasira sana na Sasha aliliona hilo.

"Stephan nini shida kipenzi mbona unaonekana mwenye hasira sana au kuna mtu amekukwaza.!?"
      Sasha alizungunza huku akimfuata Stephan lakini alipomkaribia aliambulia kibao kizito kilichompeleka chini.

"Mshenzi mkubwa wewe sasa niambie Tresha yuko wapi najua utakuwa unajua wapi alipo alafu sasa leo nikwambie nimejua kila kitu nani alinitolea figo wakati naumwa kwahiyo wewe uliejipachika uhusika ili upewe sifa basi nikwambie tu umekwama"

"Jamni mwanangu kuna nini tena.!?"
    Mam Stephan ilibidi aingilie lakini Stephan alihamia kwake na kuanza kumshushia lawama.

"Hata wewe mama ulinificha na kuniaminisha Sasha ndie alienisaidia kumbe sio yeye.!!"

"Lakini mwanangu hebu tulia kwanza unisikilize"

"Sitaki kusikia chochote kutoka kwako mama kwanza niwaambie tu Sasha simuoi kuna mtu nampenda na ninaempenda ndiye huyo huyo alienisaidia na huyo huyo nitamuoa kwahiyo mniache na sasa nitazunguka jiji zima kumtafuta, sitalala usiku wala mchana mpaka nimpate.!!"

"Stephan hebu subiri...!!"

Mama aliita lakini Stephan hakutaka kugeuka wala kumsikiliza kwa chochote, alitoka mpaka nnje lilipo gari lake na kupanda sasa kilichobaki akilini mwake ni kumtafuta Tresha kwa usiku na mchana kumrudisha tena kwenye himaya yake na ikiwezekana amuoe kabisa.....ITAENDELEA....

Unafikiri Stephan atampata Tresha na vipi Gidion atafanikiwa kuwa kwenye mahusiano na Tresha kama ambavyo anataka....sasa mambo ni moto ila majibu ya maswali yako tukutane 15..