Jina....TABASAMU LA UCHUNGU
Present.......Story Za Mapenzi
Mkasa....wa...kusisismua

            Sehemu Ya {13}

ILIPOISHIA..

Stephan kitu cha kwanza kuzungumza baada ya kuamka alimuulizia Tresha na hii ilionesha jinsi gani anampenda na kumjali ila kitendi hicho kilimfanya Sasha aumie sana, alijikuta taratibu akiuachia mkono wa Stephan ambao alikuwa ameukamata kwa upendo......ENDELEA....

Stephan alivyotamka jina la Tresha kila mmoja alibaki kuduwaa na kujiuliza Tresha ni nani ila Sasha alimfahamu vyema lakini hakutaka kuonesha kama anamjua zaidi alijifanya kama hamjui.

"Tresha ndio nani mbona hilo jina geni masikioni mwangu.!?"
      Mama Stephan aliuliza lakini Sasha alitamani kutoka nnje kwenda kumfukuza Tresha ila hakupata nafasi hiyo.

"Kuna binti aaaah...."
      Stephan alitaka kuzungumza kuwaelekeza wamtambue lakini alijikuta akipata maumivu makali sana ya tumbo maana kidonda chake alichofanyiwa oparesion bado kilikuwa kibichi.

"Taratibu Stephan kwanza ulitakiwa usizungumze maana ukiongea inaweza kuwa hatari kwako sawa eeh"
     Sasha hapo aliona amjali ili kujichukulia sifa mbele ya wazazi wa Stephan lakini wakati akiwa busy kumliwaza Stephan simu yake ilianza kuita hivyo aliomba aende nnje mara moja kupokea.

Alitoka na kutazama nani alikuwa anapiga lakini alikuwa ni Daniel hivyo alimpokelea na kuongea nae ila cha zaidi alichotaka kujua Danile ni hali ya bosi wake na ndipo Sasha alipomueleza kila kitu kilichokuwa kinaendelea.

"Daaa aisee kwakweli Mungu ni mkubwa lakini wa kumshukuru sana ni yule binti aliemtolea figo kwasababu bila yeye sahizi tungekuwa tunaongea mengine au tayari tumeanza kunsahau Stephan.

" Ah bwana eeh kwani yule binti kafanya kipi cha maana wakati hata asingekuwepo yeye tungetoa milion themanini tukanunua ila wa kushukuriwa ni madaktari ambao walifanya juhudi"
      Sasha aliona apindishe maneno maana hakupenda kanisa kuona sifa zinaenda kwa Tresha.

"Basi sawa kama ameamka ni jambo jema kwahiyo kesho anaruhusiwa kwenda kuuguziwa nyimbani sio?, ok basi nitakuja kumuona ila usiache kumpa salamu zangu"

"Sawa aina shida best"

Baada ya kuongea hayo Sasha taratibu alianza kurudi kwenye chumba alicholazwa Stephan lakini alipokikaribia alimuona Tresha amesimana mrangoni hivyo haraka alimfuata na kumshika mkono kisha alimsogeza pembeni.

"Sa..samahani eti nasikia Stephan tayari ameamka hivi ni kweli au?"
       Tresha alikuwa na shauku kubwa sana lakini Sasha hakutaka kabisa Tresha akutane na Stephan.

"Wewe yaani mimi naona bora uende tena uende mbali sana maana Stephan alivyoamka kawaambia wazazi wake yote uliyofanya mpaka yeye kuwa kwenye hatari kwahiyo kinachofuata ni kukamatwa kwenda polisi"

"Polisi..!!!?"
       Tresha alishtuka na kwa jinsi alivyokuwa akiogopa polisi ndio alizidi kuvurugwa na Sasha alipata nafasi ya kumtisha zaidi baada ya kuona Tresha alikuwa muoga wa polisi.

"Ndio polisi yaani unakwenda kukaa zako miaka therasini kwa kosa la kutaka kuuwa maana aliempiga risasi Stephan wewe unajuana nae kwahiyo yeye akikamatwa atafungwa miaka stini alafu wewe therasini kwahiyo usubiri mama"

"Jamani jamani sasa mimi nitafanya nini mbona sijafanya lolote baya, naomba unisaidie nisikamatwe sitaki kwenda jela mimi nisaidie tafadhali.!!"

"Ok njia ni moja tu kukaa mbali na Stephan yaani asikuone kabisaa sasa nitakupa kama milion tano uende mbali huko tafuta chumba upange fungua biashara uza ishi kwa amani lakini vinginevyo yatakukuta makubwa"

"Sawa nitafanya hivyo"
       Tresha masikini ilibidi akubali maana kama akikataa alihofia kukamatwa na ukiangalia kweli anajuana na Gidion hivyo aliona miaka therasini ni mingi sana kwenda jela.

Sasha bila kuchelewa alifungua pochi yake na kutoa milion tano na nusu kisha alimkabidhi Tresha na kumtaka aende mbali na Stephan kwa usalama wake.
    Basi Tresha alizipokea na bila kuchelea alitoka nnje akiwa na hofu sana lakini nafsi ilikuwa ikimuuma sana kwa kile ambacho Stephan anataka kufanya kumpeleka polisi kama ambavyo Sasha amemwambia.

Alitoka mpaka nnje ya hospital na kuchukua pikipiki aliombwa apelekwa mbali sana, na kweli dereva alimuamuru apande, aliwasha pikipiki na kuondoka zake huku Sasha akimsindikiza kwa macho na kujiona tayari ameshinda.

"Yaani ni kutumia akili tu na sio nguvu hahaha sasa Stephan ni wangu mimi kwahiyo hakuna matata kabisa"
     Sasha alijisifu na kujingamba kisha taratibu alirudi mpaka alipo Stephan na familia yake lakini ndio alikuta familia inaaga ili kuondoka.

"Mh Sasha kuongea na simu ndio umekawia hivi jamani kama ulikuwa unaongea na dunia nzima.!?"

"Hapana mama nilikuwa naongea na Daniel mfanyakazi wa Stephan alitaka kujua bosi wake anaendeleaje pia amesema kesho anakuja kumuona"

"Ok basi sawa fanya tuende"

"Hapana mama nyie mnaweza kwenda mimi nitakaa hapa mpaka baadae nampa kampani mgonjwa najua atakuwa mpweke sana"

"Kama ni hivyo sawa"

Sasha aliachwa hapo na wazazi wa Stephan waliondoka lakini Stephan hakuacha kumuuliza maswali Sasha kuhusu Tresha na ndipo Sasha aliona ni muda wake wa kumkandamiza Tresha na kujisifia yeye ili apendwe na kuaminika.

"Ahaaa kumbe Tresha ndiye yule binti basi kama ni yule sahau kuonana nae maana ulivyoletwa hapa nimemuona mara moja tu na sijamuona tena pia amekuja na mwanaume flani hivi wamenikuta mimi ndio nasubiri kufanyiwa oparesion wamekaa kidogo wakaondoka"

"Oparision.!!, ya nini tena hiyo.!?"

"Nitoe figo ili kukupandikizia wewe maana baada ya kupigwa risasi figo zako ziliharibika hivyo walinifanyia oparesion na kukupandikizia wewe ndio maana mpaka sasa unaishi"
      Sasha alijipandikiza sifa lakini Stephan hakuamini mpaka pale alipoingia nesi mmoja aliekuwa akimuhudumia na kumuuliza.

"Samahani nesi nataka kufahamu eti ni kweli mimi nimefanyiwa oparesion na kupandikiziwa figo.!?"

"Ni kweli kakaangu kuna binti ametoa figo sasa sijui ni huyu au yupi lakini naamini ni huyu ndiye amekutolea figo kukusaidia"
     Jibu la nesi lilimfanya Stephan aamini kile Sasha alikisema na mwishoe alimshukuru mara kumi kumi bila kujua alietakiwa kupokea sifa ametimuliwa kwa vitisho kama mwizi.

"Usijali Stephan mimi nitafanya chochote kwaajili yako kipenzi hata kutoa moyo wangu ili wewe uishi nipo tayari, uwepo wako ni muhimu sana kwenye maisha yangu"
     Sasha alizungumza kwa hisia mpaka machozi ya unafikiri yalianza kumtoka na kumfanya Stephan amuhurumie.

"Usilie sasa jamani najua una maumivu makali sana na una upendo wa dhati kwangu sasa naomba unitazame alaru futa machozi sawa"
     Stephan alimbembeleza Sasha na kumuona mtu wa muhimu sana lakini alipomfikiria Tresha na alipokumbuka alivyoambiwa alikuja na mwanaume alijikuta akimchukia ghafla pasi na kujua ndie mtu aliempa msaada.

Walikaa hapo huku story za hapa na pale zikichukua nafasi yake pia kwa upande wa Sasha ilikuwa ni burudani sana, alionekana binti mrembo lakini ndani alikuwa amejawa na roho mbaya ambayo ilifichwa na uzuri wake.

              ******************

Safari ilichukua Takribani masaa matatu mwisho walifika sehemu moja iliyokuwa na pilika nyingi Tresha aliomba ashushwe hapo.
     Ilikuwa ni ndani ya jiji hilo hilo lakini alipofika yeye na alipokuwa Stephan au anapoishi Stephan ilikuwa ni mbali sana na hata kuonana kwao ingekuwa ni vigumu sana.

"Kwahiyo ni kiasi gani unadai kakaangu.!?"

"Elfu kumi dada"

Tresha hakutaka maneno mengi alitoa pesa aliyokuwa anadaiwa ya usafiri na kukabidhi kwa dereva kisha aliingia mitaani sasa kuanza maisha na sehemu hiyo aliipenda sana maana ilikuwa imechangamka, pilikapilika zilikuwa nyingi na hata mtu ukifungua biashara yako basi utapata wateja vizuri sana.

Tresha alikuwa ni binti mchapakazi, asiependa kulaza damu hivyo alivyoingia tu mtaani alitafuta sehemu ambayo angefungua biashara, aliongea na mmiliki wa sehemu hiyo walipopatana kulipa kwa mwezi basi siku hiyo hiyo alitafuta vijana na kuomba wamjengee sehemu ya mgahawa.

Ilipendeza sana kuwa na mwanake kama Tresha ambae ni mchapakazi asiepoozesha mwili wake na hata mmiliki wa sehemu hiyo alimsifia sana .

"Yaani binti nimekuvulia kofia, na hivyo ndivyo ambavyo mwanamke anatakiwa awe sio hawa wa kuomba pesa kila siku alafu nguvu wanazo kwahiyo mama nakupongeza sana na hii sehemu utapata wateja wengi sana"

"Asante Babaangu acha nifanye mpango wa kutafuta chumba cha kupanga maana kwenye mitaa hii mimi ni mgeni nimekuja kuanza maisha sasa naimani chumba nitapata"

"Oh kumbe mgeni basi nifuate mimi nitakupeleka sehemu ambayo utapata chumba kizuri wala usijali"

Kiza kilikuwa tayari kimeanza kutanda yapata saa moja kasoro, kwa mwendo wa robo saa walifika kwenye nyumba moja kubwa na ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na vyumba vingi sana vya kupanga pia kulikuwa na baadhi ya wapangaji walikuwa wakiishi humo.

"Tumefika mamaangu alafu sijafahamu unaitwa nani vile?"

"Naitwa Tresha"

"Oh Tresha haya karibu manaa sisi ndio wazee wa mtaa mimi naitwa mzee Magasi karibu sana kwenye mtaa wetu pia ukiwa na shida usisite kuniambia"

"Sawa babaangu shika hiki kiasi kidogo cha pesa kitakusaidia hata kununua sukari"

"Asante mwanangu"

Basi mzee Magasi alimuaga Tresha na kurudi zake kwake, Tresha aliingia kwenye nyumba hiyo alimkuta bibi na bwana wameketi nnje alitambua fika watakuwa wamiliki wa nyumba hiyo, aliwasalimia na kuwaeleza shida yake kuwa anahitaji chumba.

"Ahaa basi umepata mjukuu wangu karibu sana"

"Asante babu kwahiyo itagharimu kiasi gani kwa mwezi.?"

"Ah itagharimu elfu therasini alafu kama unavyoona umeme upo, maji yapo kwahyo kazi kwako tu mjukuu wangu ingia ndani tukuoneshe vyumba ukipenda basi tuandikishane mambo yamalizike"

Basi bila pingamizi Tresha aliingia na kuanza kuangalia chumba hadi chumba kiukweli alivipenda sana na kuamua kulipa kodi ya miezi mitano.
     Hatua hiyo ilimalizika ila kuhusu godoro la kulalia aliona atanunua kesho hivyo siku hiyo alilala chumba kimoja na mtoto wa mwenye nyumba alieitwa Shakira na ni baada ya kuomba, pia hata kula alikula nao, yeye alichangia unga tu mambo yakaenda powa.

Siku iliyofuata asubuhi na mapema alijiandaa lakini kabla hajatoka Shakira yaani mtoto wa mwenye nyumba alimsimamisha.

"Samahani mdogowangu nasikia wewe ni mgeni wa mitaa hii sasa unahitaji kwenda wapi hata nikupe kampani uifahamu mitaa?"
 
"Nataka nikatafute masufuria na vyombo vingine si kama nilivyokwambia jana nataka kufungua mgahawa dadaangu"

"Ok basi sawa nitakupeleka alafu una bahati leo kuna mnada vitu mbali mbali used vinauzwa kwa bei rahisi kwahiyo utapata vingi ukihitaji"
       Shakira hakuwa na roho nyeusi ilibidi amuunge mkono Teresha na kumpeleka mpaka ulipo mnada ambapo huko kulikuwa na vitu vingi vya kila aina vinauzwa, kweli bhana Tresha alirudi na vitu vingi sana, alipata vyombo vya kutosha, kitanda na goro lake pia alipata sofa moja na kabati dogo.

Alikodi gari ambayo ilimpelekea mpaka kwake kisha alivipanga vizuri na chumba sasa kilikuwa kimavutia sana.

"Shakira dadaangu asante sana ila wewe unajishughulisha na biashara gani.?"
      Lilikuwa ni swali kutoka kwa Tresha wakiwa wameketi nnje na Shakira baada ya kazi nzito ya kupanga vyombo ndani.

"Ah mimi nilikuwa nashona nguo lakini kwa sasa nipo tu maana nilipokuwa nafanya kazi nimefukuzwa basi tunaangalia tu na wazazi wangu"

"Ahaa pole lakini mimi naona sasa tusaidiane kwenye kazi hii ya mgahawa maana mwenyewe sitaweza kwahiyo tutafanya usiku tunapiga hesabu nakupa hata robo ya mapato basi maisha yanasonga mwisho wa siku unajikuta unamiliki cherehani yako mambo yanakuwa powa"

Wazo la Tresha lilikuwa zuri sana ambalo Shakira alilipokea kwa mikono miwili na kuanzia hapo wakajikuta wanaanza kufanya kazi pamoja na kwa bidii mpaka mwezi mmoja unakatika walikuwa tayari wamezoeleka na wateja na maisha yalianza kuwa laini sana.

                ******************

Hali ya Sidan ilikuwa nzuri kabisa na kazini alikuwa akienda kama zamani ila usumbufu wa Joyce bado alikuwa akikutana nao lakini hakuwahi kumpa nafasi kuwa karibu yake, pia hata Sasha licha ya kipindi hicho kuishi nyumba moja na Stephan lakini hakuambulia chochote.

"Sasha unajua kipindi kile naumwa mama na baba walikutaka uje kuishi na mimi hapa ili kuniangalia na kunihudumia lakini sasa nimepona ila nashangaa bado upo hapa.!!"

Ilikuwa ni usiku mmoja Sasha na Stephan wakiwa wanapata chakula cha usiku Stephan aliamua kumtolea uvivu Sasha na kuzungumza maneno hayo yaliyomuuma sana Sasha.

"Jamani sasa ndio maneno gani hayo unaongea et alafu kumbuka wazazi wako wamekuambia mimi ni mke wako mtatajiwa".

"Ni sawa mke mtarajiwa lakini ndio tugandane kama ndizi jamani.!?"

"Ok kama unataka niende sawa nitaenda ila siku za mimi na wewe kufunga ndoa zimakaribia kwahiyo muda si mrefu nitarudi tena hapa"

"Sawa"

Stephan hakuwa na pingamizi pia hata kumuoa Sasha amekubali kwasababu wazazi wake wamemfosi pia ukiangalia Sasha ametoa figo kwaajili yake hivyo hakuona sababu za kumvunja moyo lakini ukweli alikuwa hampendi hata kidogo.

Ok tuache huko tuje kwa Tresha ambae kwa sasa ni mama ntilie na alikuwa na wateja wengi sana kiasi kwamba mpaka wengine walikuwa wanakosa chakula.

"Daaah Shakira shoga yangu yaani leo chakula kimeisha mapema sana natamani hata kupika tena najua wateja bado wapo"

"Kama inawezekana basi tupike hata mimi naimani tutauza ila tununue mchele kilo kumi na unga kilo tano naamini chakula kitaisha"

"Basi sawa acha nikanunue mchele wewe subiri hapa andaa vyombo mimi nakuja sasahivi"

Tresha alimuachia maagizo Shakira na kuondoka zake lakini kitendo cha yeye kuondoka ilifika gari moja ya kifahari na kusimama ambayo ilimuacha mdomo wazi Shakira, baada ya kusimama gari hiyo mrango ulifunguliwa na alishuka Gidion ambae alivalia samart sana......ITAENDELEA.....

Unafikiri ninu kitafuata hapo je Stephan atakubali kumuoa Sasha na vipi kwa Tresha atafanya nini endapo akimuona Gidion...mimi na wewe hatujui ila tukutane sehemu ya 14....