Jina....TABASAMU LA UCHUNGU
Present.......Story Za Mapenzi
Mkasa....wa...kusisismua

            Sehemu Ya {12}

ILIPOISHIA..

Yalikuwa ni maamuzi magumu aliyochukua Sasha na hiyo yote ni kumkomesha Tresha, basi kazi ilifika sehemu husika na ilipotimu saa nne usiku familia yote iliondoka na muda huo ndio yule Nesi aliona autumie kuanza kazi yake huku masikini Tresha hana ili wala lile....ENDELEA......

 Inatimu saa tano usiku ndipo jukumu la kuhakikisha Tresha anakuwa chizi lilianza na yule nesi aliepatiwa pesa na Sasha ndiye aliekuwa kwenye harakati za kwenda kumchoma Tresha sindano ya kumvuruga akili lakini wakati anakikaribia chumba alichokuwa Tresha huku akiwa na sindano mkononi ghafla alisikia akiitwa.

"Nesi tafadhali nahitaji kukuuliza...humu ndipo alipokuwa Tresha maana kuna binti tumeambiwa emelazwa humu anaitwa Tresha sasa kama ni humu tunaomba tuonane nae mara moja"
       Yalikuwa maneno yaliyozungumzwa na Daniel huku akiongozana na Joyce lakini hawakujua walikuwa wamevuruga kabisa mbinu ya nesi huyo.

"Ah sina uhakika lakini huenda ni humu kwahiyo mnaweza kwenda kumuona mkaongea nae wala msijali"

"Ok asante sana"

Nesi aliwaruhusu lakini alikuwa amechukia sana maana tayari alikuwa amevurugiwa mpango wake ila hakukata tamaa aliona kama plan A imeshindikana basi atumie B ili kukamilisha jukumu lake linakamilika.

Tresha akiwa kwenye usingizi mzito aliamshwa na alipowatazama watu waliomuasha aliona sura ngeni hivyo ilimbidi ainuke na kuketi ili kuongea nao vizuri na afahamu walikuwa na shida gani mpaka kumfuata.

"Habari yako dadaangu mimi naitwa Daniel ni mfanyakazi wa Stephan na huyu anaitwa Joyce ni mpenzi wa Stephan ila kuja hapa tulikuwa tunahitaji kujua jambo kuhusu hii ajali iliyomtoke Stephan, chanzo ni nini mpaka kupigwa risasi.!?"
     Daniel aliweka nukta lakini Tresha akili yake ilikuwa mbali sana, alikuwa akiwaza mengi kuhusu Stephan maana kila mwanamke anaekuja hapo lazima awe mpenzi wa Stephan.

"Inamaana yule aliekuja na wazazi wake muda ule ni mpenzi wake, huyu pia ni mpenzi wake na hapo hapo atakuja mwingine ni mpenzi wake mh kumbe Stephan ni hatari namna hii.!?"
       Tresha alijikuta na mawazo ghafla ila hakujua hao wengine walikuwa wapenzi jina lakini yeye pekee ndie aliekuwa kwenye moyo wa Stephan.

"Dada hebu tujibu tafadhali tunahitaji kufahamu nini kimesababisha hivi.!?"

"Ah kakaangu mimi hayo maswali siwezi kuyajibu kamuulizeni mgonjwa wenu mwenyewe maana mimi nimempa msaada wa kumtolea figo tu hayo mengine sifahamu"
    Tresha ilibidi awakatae kiaina ila alifanya hivyo kwa hasira aliyokuwa nayo iliyoambatana na wivu baada ya kuona Stephan ana wanawake wengi tofauti na ambavyo amefikiria yeye.

"Sasa dada tukuelewe wewe au tumuelewe yule daktari maana yeye amesema tuje humu unajua kila kitu alafu wewe unasema uju kwahiyo hujui kweli au ni kusudi ok sema unataka kiasi gani tukupe ili utusimulie.!?"

"Kakaangu mbona unakuwa mbishi na sio muelewa, nimesema sijui sasa nikusimulie nini au unataka nikusimulie mimi nilivyofika hapa na kutoa figo au vipi.!?"
     Tresha alikuwa amepanic lakini muda huo huo aliingia daktar na kuwaomba waende wanamsumbua mgonjwa.

"Dah sawa kama hutaki kutuambia lakini tunashukuru kwa msaada wako uliompa Stephan Mungu akubariki sana na akupe maisha marefu dadaangu"
       Daniel hakuwa na jinsi kutoa shukrani kisha alitoka nnje na Joyce wake lakini huku Tresha alianza kuchomwa sindano ambazo zimgemsaidia kupona haraka majeraha yake.

Alichomwa sindano mbili lakini alipochomwa sindao ya tatu alihisi maumivu makali sana mpaka hata yule daktar alishangaa na ndipo alipoangalia ile dawa iliyokuwa kwenye sindano na kugundua ilikuwa ni sumu.

"Mungu wangu mbona ni sumu hii alafu nakumbuka nimeweka sindano sahihi sasa hii sumu imetokea wapi.!?"

"Etiii sumuuu.!!?"
      Tresha alishtuka kusikia amechomwa sindano ya sumu lakini daktari ili kumtoa hofu alimficha na kumueleza alikuwa anamtania.

"Umenitisha jamani nikajua sumu nilitaka kuanza kulia lakini hayo sio matani mazuri mtakuja kutuuwa kwa presha.!!"

Daktari aliinuka haraka na kutoka nnje lakini ukweli alimchoma Tresha sindano ya sumu na hakufahamu sindano ile imewekwaje wakati alihakikisha kabisa sindano zote zipo sawa, aliingia kwenye ofisi yake na kutafuta antidote ya kuuwa sumu lakini hakukuta zaidi ya kuona madawa mengine.

Lakini kumbe aliefanya hivyo alikuwa ni nesi yule alietumwa na Sasha, alimvizia daktari wakati ametoka aliingia ofisini kwake na kutoa sindano moja kati ya sindano ambazo alitakiwa kwenda kumchuma Tresha kisha aliweka yake yenye sumu na haikuishia hapo alichukua na antidote zote zilizokuwa humo ambazo zilikuwa na uwezo wa kukata sumu na kuondoka nazo.

Kazi ilikuwa nyepesi sana na mpango wa Sasha ulikuwa umetimia lakini upande wa Tresha wakati amelala alianza kuhisi vitu vikitambaa akilini mwake na kumfanya aanze kujikuna kichwa kila wakati.

"Hii ni nini tena mbona sielewi.!?"
        Tresha alijiuliza bila kupata jibu la swali lake lakini hakufahamu kama tayari sumu aliyochomwa inaanza kufanya kazi na muda si punde au siku kadhaa akili yake itabadilika.

Upande wa wazazi wa Stephan familia ilikuwa na huzuni sana siku hiyo na hakuna hata mmoja kati yao aliekuwa na lepe la usingizi kila mmoja alikuwa akimuwaza Stephan lakini wakiwa kwenye hali hiyo ya majonzi ghafla simu ilianza kuita na simu hiyo ilikuwa ya Sasha.

"Samahanini jamani napokea simu"
      Sasha aliaga na kuchukua simu yake kisha alisogea pembeni na kupokea.

"Hello natumai kila kitu kimeenda sawa kabisa.?"

"Kila kitu kimekwisha kesho ukija utakuta tayari mambo yamekamilika ila usisahau kunimalizia pesa yangu kwasababu kazi niliyofanya ni kubwa sana"

"Ok usijali kila kitu kitakamilika kesho nikifika hapo na kumuona huyo mpuuzi yupo kwenye hali gani"

"Ok basi sawa"
     Nesi alikata simu lakini kumbe wakati anaongea na simu yule daktari ambae alikuwa na jukumu la kumuhudumia Tresha alikuwa pembeni akimsikiliza na tangu mwanzo alikuwa akimuhisi hivyo alisubiri amalize kuongea na simu ndipo alimfuata.

"Wow inapendeza sana kuwa na watoa huduma wapumbavu kama wewe kwenye hospital kubwa kama hii, nilijua tu lazima utakuwa ni wewe sasa naomba unipatie antidote haraka nikamuwahi yule binti alafu mimi na wewe tutakuja tuongee vizuri"

 "La...lakini ni..."

"Mimi sitaki kujua cha lakini, nipatie amtidote haraka la sivyo utaikosa kazi yako kama taarifa hizi zitafika kwa daktari mkuu"

"Ok sawa nakupa lakini tafadhali tafadhali nipo chini ya miguu yako naomba usiende kuripoti kwa daktari mkuu nitafukuzwa kazi mimi alafu kama unavyojua nipo na familia inanitegemea"
      Nesi alikuwa mdogo kama sindano maana siri ilikuwa tayari imefichuka, basi ilibidi atoe antidote na daktri bila kuchelewa alipoipata alimuwahi Tresha na kumchoma kisha alimuomba alale.

Ilikuwa ni ponea yake lakini kinyume na hapo habari ya Tresha ilikuwa imeisha kilichobaki na kumzungumzia kama kichaa ila kwa juhudi za daktari zilisaidia.

                 ***************

Siku iliyofuata Tresha aliamka na kujikuta yupo sawa pia alikuta amewekewa kifungua kinywa safi sana lakini hakutaka kukigusa mpaka pale atakapotambua ni nani amemuandalia.

Kweli hakukigusa na zilipopita dakika kadhaa aliingia daktari huku akiwa mwingi wa tabasamu baada ya kumuona Tresha ameamka.

"Oh Mungu mkubwa umeamka shujaa lakini vipi unajisikiaje na hali hasa kichwa chako.!?"
      Swali la daktari lilimfanya Tresha ashangae maana yeye amefanyiwa oparesion tumboni sawa iweje aulizwe kuhusu kichwa.

"Ah salama tu"

"Ok vyema basi fanya upate kifungua kinywa nimekuandalia mimi lakini ninachokuomba uwe makini sana maana unawinda kama mnyama na muda wowote unaweza kujikuta sehemu mbaya"

"Unamaanisha nini daktari kusema hivyo.!!"

"Jana kuna nesi alinichanganyia sindano na kuweka moja yenye sumu ambayo itakufanya uwe kichaa na mimi bila kujua nilikuchoma ndio maana uliona nimeshtuka na pia uliona kichwa chako kama kinawashwa kwahiyo kidogo uwe kichaa kama nisingekuwahi lakini shukuru Mungu upo salama ila jichunge"

Maneno ya Daktari yalimpa hofu Tresha na kutaka kumjua ni nani amemfanyia hivyo ili kama inawezekana ale nae sahani moja.

"Nitakwambia ila uwe mpole sana, unajua baada ya nesi kunichanganyia sindano baadae nilikuja kumgundua na akaniambia kila kitu kwahiyo aliekuwa nyuma ya hili ni yule binti aliekuja jana mweusi ambae aliambatana na wazazi wa mgonjwa"

"Ahaaa ok basi sawa asante dadaangu kwa kuniokoa acha nicheze nae mchezo maana bila hivyo naweza kufa huku najiona"

"Yah kwahiyo kuwa makini"

Tresha sasa alikuwa amefumbuliwa macho na alijua yote anafanyiwa kwasababu gani sasa kilichobaki ni umakini wake kuweza kukabiliana na Sasha.

Ok tutoke huko twende kwa Shangazi na mume wake ambao maisha yao yamekuwa ya tabu lakini bahati nzuri walipanga chumba ili kusogeza siku maisha yaende.

Asubuhi ya siku hiyo wakati mume wa shangazi anaamka alishangaa kumuona mke wake akihema haraka sana huku damu zikimtoka mdomoni na puani, hii ilimuogopesha sana.

"Mke wangu, mke wanguu nini shida tena mbona hivyo.!!?"
      Mume alikuwa tayari amechanganyikiwa lakini shangazi alipotaka kujibu alishindwa damu zilikuwa zikimtoka bila kukoma.

Hakuwa na muda wa kupoteza, alimbeba na kutoka nae nnje ila bahati nzuri kituo cha usafiri hakikuwa mbali, alijongea mpaka kituoni alichukua bajaji na kuomba wawahishwe hospital lakini mpaka wakati huo haikufahamika Shangazi amepatwa na matatizo gani.

Alifikishwa katika hospital ya rufaa lakini walipomcheki hawakuona tatizo lolote na hapo ndipo mjomba akaona ampeleke kwa yule bibi wa kienyeji akapatiwe matibabu maana ilionesha tatizo hilo sio la kutibika kwa matibabu ya kizungu.

Kweli bhana alipompeleka kwa yule bibi alifanyiwa matibabu na kukaa sawa, lakini alipoamka alipatiwa onyo kali sana.

"Kama ambavyo nimekwambia mjukuu wangu hilo ni onyo kutoka kwa wazazi wa yule binti"

"Kwahiyo wanawezaje kunionya wakati wamekufu miaka kumi nyuma.!?"

"Ndio wamekufa lakini nafsi zao zipo kwaajili ya binti yao sasa nakuomba tu muache huyu binti usimfuatulie tena la sivyo utakumbuka maneno yangu"

"Ah mimi siamini kwa hilo bibi kama hutaki kunipa msaada wako ni sawa ila nitamuandama huyu binti mpaka naingia kabulini maana amenifanyia dharau kubwa sana"
     Shangazi kwenye jambo la ubishi alistahili tuzo maana hakutaka kusikia chochote ila alichowaza yeye ni kuhakikisha anamuona Tresha akitaabika.

               ****************

Sasha na wazazi wa Stephan walifika hospital kwaajili ya kumuangalia mgonjwa wao ila upande wa Sasha hamu kubwa aliyokuwa nayo ni kumuona Tresha na hii ni baada ya kupewa taarifa kazi yake imekamilika.

"Hapa nitumie ujanja kuwatoka hawa wazee nikamuone huyo mjinga maana anajifanya mjuaji sana sasa acha maisha yake yawe mtaani"
     Sasha alijisemea na mwisho aliaga, alipopata ruhusa alijongea mpaka kilipo chumba alicholazwa Tresha na kuingia lakini alimkuta ndio anamalizia kupata kifungua kinywa.

"Oh my God umechelewa bhana mke wa Stephana lakini sio mbaya najua umekuja kuniangalia kama tayari nimekuwa chizi au laa ila nikutoe hofu kwamba kazi yako imetimia na hivi punde nakuwa kichaa hahahaha"
      Tresha alizungumza kwa furaha maana alijua jinsi gani Sasha anaumia.

"Unazungumza kuhusu nini mpuuzi wewe.!?"

"Amna hata mimi sijui naongea kuhusu nini au ndio ukichaa umenipanda lakini sio mbaya umejaribu na nimeona jinsi gani ulivyo na roho nyeusi kama ngozi yako lakini yote na yote jaribu mara nyingine kwa sasa umechemsha"

Sasha hakutaka kuendelea kukaa humo maana mineno ya Tresha ilikuwa ikimkera sana alichofanya ni kutoka na kwenda kumuangalia Stephana ambae bado alikuwa hajaamka kabisa lakini kwa taarifa za daktari ingechukua week nzima kuamka.

Basi masiku yalianza kukatika na tarehe zilianza kusogea huku familia ya Stephan haikuacha kwenda kumuona kijana wao wakiongozana na Sasha ila mchana mmoja ilikuwa siku ya ijumaa ndipo Stephan alipata fahamu.

Wakati anapata fahamu familia nzima ilikuwa kwenye chumba ambacho amelazwa ila Tresha alikuwa nnje akiwasubiri maana hakuruhusiwa kuingia pamoja na familia na hii yote ilikuwa ni mipango ya Sasha.

Hali ya mazingira ilimfanya Stephan atambua wapi alipo na alipotazama pembeni aliona familia yake na alimuona Sasha ambae alikuwa na tabasamu mwanana huku ameukamata mkono wake lakini kuna mtu mmoja alimiss.

"Tresha yuko wapi.?"

Stephan kitu cha kwanza kuzungumza baada ya kuamka alimuulizia Tresha na hii ilionesha jinsi gani anampenda na kumjali ila kitendi hicho kilimfanya Sasha aumie sana, alijikuta taratibu akiuachia mkono wa Stephan ambao alikuwa ameukamata kwa upendo......ITAENDELEA....

Unafikiri nini kitafuata hapo maana shangazi amesema hamuachi Tresha atamuandama mpaka kifo na huku vita ya mapenzi kati ya Sasha na Tresha imeanza..nani ataondoka mshindi....tuungane kwenye sehemu ya 13 kujua nini kitafuata..