Jina....TABASAMU LA UCHUNGU
Present.......Story Za Mapenzi
Mkasa....wa...kusisismua
Sehemu Ya {11}
ILIPOISHIA..
Maneno ya mama yalimfanya Joyce atabasamu, alimfuata mama yake na kumkumbatia kwa furaha sasa alichokiwaza kwa wakati huo ni harakati za kumpata Stephan, amueleze ukweli kama anampenda na kisha afanye taratibu za kumtambulisha kwa wazazi wake wamtambue na swala la ndoa lipite...ENDELEA.....
Ilikuwa ni pisha njia katika hospital kuu ya taifa na jopo la madaktari lilikuwa kwenye mwendo wa kukimbia huku wakisukuma kitanda cha matairi manne ambacho juu ya kitanda hicho alikuwa amelala Stephan ambae hajitambui na tumbo lake likitapakaa damu nyingi sana.
Kwenye msafara huo wa madktari kusukuma kitanda alikuwepo pia Tresha ila yeye alikuwa ameukamata vyema mkono wa Stephan huku akiangusha kilio ambacho kilimfanya kila mmoja amshangae hapo hospital.
"Staphan hebu tafadhali fumbua macho na useme kitu Tresha wako nipo hapa nitazame japo kidogo.!!"
Tresha alizungumza maneno yaliyojaa majonzi na uchungu lakini maneno yake hayakumfanya Stephan afumbue macho wala kujitikisa.
Safari ya kusukuma kitanda ilikomea kwenye chumba cha oparesion, madaktari walimuamuru Tresha asubiri nnje kisha wao waliingia ndani na Stephan ambae hali yake ilikuwa mbaya sana.
"Daktari naomba tafadhali fanyeni kila liwezekanalo Stephan wangu awe salama nawaomba nipo chini ya miguu yenu"
Tresha masikini alijikuta akipiga magoti lakini daktari alimuinua na kumsogeza mpaka vilipo viti na kumuomba akae kisha alimtoa wasiwasi.
"Usijali dadaangu wa kumponya mgonjwa wako ni wewe na Mungu pekee nikisema wewe namaanisha maombi na dua zako kwahiyo usiache kumuombea naimani Mungu atapokea dua zako na mgonjwa atakuwa salama"
Daktari baada ya kuongea hayo aliweka miwani yake vizuri na kuingia chumba cha opareshioni.
Hali ya utulivu ilikuwa imetawala ndani ya chumba hicho, zilisikika kelele za visu na mikasi tu ambayo ndio ilikuwa na kazi ya kuhakikisha Stephan anakuwa salama.
"Daktari huyu kijana amepigwa risasi mbili alafu hizi risasi zinaonekana zilikuwa na nguvu kwa kiasi kikubwa kwasababu tukimuangalia amepigwa risasi mgongoni ila ajabu zimetokea mbele kwahiyo hii inaweza kuwa hatari sana na anaweza asipone"
"Kwani mashine si zinasema bado anapumua?"
"Yah anapumua lakini kwa mbali sana na ukiangalia figo zake zote zimeharibika kwa risasi sasa hapa awekewe figo nyingine la sivyo tunamkosa kabisa"
"Basi cha kufanya toeni kwanza hizo risasi alafu tutaangalia taratibu za kumuwekea figo ila wakati huo tushamtoa kwenye hatari ya kwanza"
Yalikuwa ni mazungumzo ya madaktari huku wakihangaika kuokoa maisha ya Stephan lakini upande wa nnje Tresha alikuwa mtu wa kulia huku mkononi akiwa na simu ya Stephan.
"Hapa tu niwapigie simu wazazi wake ili wajue maana bila hivyo nitajikuta kwenye wakati mgumu sana!"
Mawazo yaliyopita kichwani kwa Tresha hakutaka kuyapotezea, alipiga simu kwa mama Stephan na kumueleza habari hizo ila alipotaka kupiga na kwa baba yake simu iliisha salio.
Baada ya taarifa hizo kufika kwa wazazi wa Stephan haikuchukua dakika ishirini walikuwa tayari wamefika huku vilio vikichukua nafasi yake na aliekuwa akilia sana alikuwa ni mama wa Stephan akisaidiwa na Sasha.
"Daktari mwanangu yupo chumba gani niambie tafadhali niambie nikamuone jamani Stephan wangu.!?"
Mama Stephan alimvamia daktari mmoja na kumuuliza ila yule daktari hakuwa na taarifa yeyote maana kitengo alichokuwa yeye kingine kabisa na kitengo ambacho kilichompokea Stephan.
"Samahani mama mimi sifahamu labda ukaulizie kwa madaktari wengine pia uwape jina la mgonjwa la sivyo utakesha pasi na kumuona mgonjwa wako"
Yule daktari alimuachia maelekezo mama Stephan na kuondoka zake ila mama Stephan alipotazama kwenye viti wanavyokaa watu kusubiri wangonjwa wao au kusubiri huduma ndipo alimuona binti ameketi akilia huku ameshika simu ya Stephan na nguo zake zikitapakaa.
Alimuendela haraka na alipomfikia alimkunja na kumsimamisha huku akimuhoji maswali ambayo yalimfanya Tresha azidi kuangua kilio pasi na kumjibu.
"Wewe ndie umenipigia simu eeh sasa niambie kijana wangu yuko wapi nataka kwenda kumuona niambie sasahivi.!!"
Mama Stephan hakuacha kulia lakini Tresha mdomo haukuwa na nguvu zaidi ya kuishia kuonesha kidole kwenye chumba ambacho Stephan ameingizwa.
Vilio havikukoma sehemu hiyo na Tresha ilibidi ajikaze kueleza nini kilitokea ila kilichofuata hapo ni lawama na matusi.
"Mshenzi mkubwa wewe yaani wewe ndie chanzo cha yote sasa nakwanbia hivii mwanangu kama akifa basi na wewe nitakuuwa sitakucha uishi kabisa kwenye ulimwengu huu.!!"
Zilikuwa ni lawama tu zilizoshuka kwa Tresha ila yeye hakujali hata kidogo alichowaza ni hali ya Stephan tu hayo mengine aliona kama makelele yasiyo na maana.
Wakati lawama juu ya Tresha zinaendelea alitoka daktari mkuu wa oparesion akiwa na karatasi ya majibu mkononi hivyo ilibidi wote wamfuate kujua hali ya Stephan onaendelea.
"Daktari hebu niambie mwanangu anaendelejae nahitaji kujua niambie tafadhali"
"Mama hebu usipanic maana ukipanic utashindwa kunielewa kwahiyo tulia, shusha pumzi unisikilize"
"Ok daktari ok ok"
Mama Stephan ilibidi awe mpole na hapo ndipo daktari alianza kuwapa majibu ya hali ambayo mgonjwa wao anayo.
"Mgonjwa wenu tumetoa risasi kwenye mwili wake lakini risasi hizo zimeathiri figo zake kwahiyo hii ni hatari kubwa sana kwake sasa ili kupona anatakiwa kupata figo angalau moja na gharama ya figo ni miliona themanini sasa kama inawezekana tuagize kutoka india na ndani ya siku mbili figo zitafika hapa mgonjwa wenu atapatiwa matibabu"
"Daktari kama inawezekana pigeni tu simu iletwe sisi tutatoa hizo miliona themanini ila tunachohitaji ni kijana wetu apone"
Baba Stephan ilibidi azungumze kama kichwa cha familia lakini Tresha ilibidi aingilie kati na kuzungunza.
"Daktari sio kupiga simu ila kama inawezekana kutoa figo mimi nipo tayari kufanyiwa oparesion, figo yangu moja itolewe lakini Stephan awe salama"
"Ok hiyo inawezekana binti kwahiyo kama upo tayari naomba unifuate tuanze upandikizaji"
Daktari alitangulia kuondoka ila wakati Tresha anataka kumfuata Sasha alimshika mkono.
"Fanya ufanyavyo lakini Stephan wangu apone maana wewe ndie chanzo cha matatizo kwahiyo kama akifa ujue utanioa wewe sasa jiangalie.!!"
Vitisho vya Sasha havikumuathiri kwa chochote Tresha na wala hakujali kabisa ila alichowaza yeye ni kuokoa maisha ya Stephan na kumuona akirudi tena mbele ya macho yake.
***************
Usiku huo wakati madaktari wakihangaika kuokoa maisha ya Stephan lakini huku kwa shangazi alirudi tena kwa mganga wake ili kupata mbinu zaidi za kumtesa Tresha.
"Bibi dawa uliyonipa imefeli kabisa yaani mpaka sasa hakuna majibu yeyote niliyopata sasa kama inawezekana tafadhali naomba dawa nyingine bibi"
Shangazi alizungumza huku akiwa ndani ya kilinge yaani kijumba hicho kidogo ambacho ndicho bibi hutoa huduma kwa wateja wake.
"Dawa niliyokupa tayari imeanza kufanya kazi kwahiyo muda si punde majibu utayaona ila yahitaji uvumilivu kidogo mjukuu wangu"
"Kwahiyo unataka kusema bibi kile chakula Tresha alikuwa.!?"
"Hapana hakula ila alikuwa na nia ya kula sasa kama ametia nia kula inamaana ni sawa na kula kwahiyo mateso ndio yatakuwa maisha yake kuanzia sasa, naomba uende na uje hapa baada ya siku saba"
Shangazi kwa furaha aliinuka na kuondoka zake lakini tuje upande wa Joyce ambae siku hiyo alikuwa na furaha sana hasa baada ya wazazi wake kuridhia amlete Stephan kwao lakini hakujua kama Stephan yupo kwenye matatizo makubwa sana.
Kwa hamu na shauku aliyokuwa nayo alipiga simu kwa Stephan ila alipokea mwanamke na sauti ya mwanamke huyo ilimtisha baada ya kisikia akilia kwa kwikwi.
"Hello we nani na kuna nini mbona unalia au kuna jambo limemkuta Stephan wangu jamani.!?"
Joyce nae alijikuta akianza kutokwa na machozi lakini hakuambulia chochote zadi ya simu kukatwa na alipopiga tena namba ilikuwa haipatikani.
Jambo hili lilimtisha sio kidogo na hakufahamu aanzie wapi wala aishie wapi lakini wakati yupo kwenye mawazo simu yake ilianza kuita na aliekuwa anapiga alikuwa ni Ochu.
Hakutaka kuipokea aliona kama anampigia kelele ila alichofanya ni kukata na kutafuta namba ya Daniel kisha alipiga na bahati nzuri alimpata.
"Daniel hebu kwanza niambie nini kimetokea kwa Stephan maana nimepiga simu yake kapokea mwanamke huku akilia kisha akakata bila kusema chochote sasa ukiwa kama mtu wake wa karibu basi naamini utakuwa unafahamu nini kinaendelea.!?"
"Daaah ni kweli kuna taarifa mbaya maana mimi mwenyewe ndio nimepigiwa simu na Sasha hivi naelekea kwenye hospital ya taifa kujua anaendelaje"
"Jamani mbona unanitisa hebu niambie nini kimfika.!?"
Joyce alijikuta na shauku ya kutaka kujua kilichotokea lakini moyoni mwake kulikuwa na hofu iliyokuwa ikisubiri kupokea habari mbaya.
"Inasemekana amepigwa risasi mbili sasa haijulikani amepigwa na nani pia hali yake ni mbaya huko alipo maana figo zake zote zimeharibika kwahiyo acha niende nitakupa taarifa zaidi"
"Sawa na mimi nakuja sasahivi"
Joyce alikata simu na bila kuchelewa alijiandaa na kutoka ila alipofika sebuleni alisimamishwa na mama yake.
"Haya kumekucha tena, usiku huu unaenda wapi.!?"
"Mama yule mwanaume niliesema nitamleta kwenu kumtambulisha amepata matatizo, amepigwa risasi na watu wasio julika kwahiyo hapa nawahi muhimbili nasikia hali yake ni mbaya sana sasa naomba niende mama nikifika nitakujulisha"
Joyce haraka alitoka mpaka nnje na kujipakia kwenye gari yake kisha safari ilianza kuelekea hospital lakini moyoni mwake bado alikuwa na hofu kubwa sana.
****************
Taratibu za utoaje wa figo na upandikizaji zilifanyika na hiyo kidogo iliwafanya wana familia wapumue, hata Tresha akiwa chumba cha oparesion alifurahi sana baada kupata taarifa hizo.
"Hongera sana dada kwa ujasiri wako ama kweli una upendo wa dhati sana kwa mgonjwa wako maana hii ni ngumu sana kutokea kwa watu wengine ila wewe una moyo wa ujasiri"
Daktari alimpongeza Tresha huku alimtoa kwenye chumba hicho na kumpeleka kwenye wodi za kawaida ambapo huko atakaa mpaka hali yake itakapo tengemaa.
"Asante sana daktari lakini hata mimi nampongeza ngonjwa wangu maana amepigwa risasi kwaajili yangu kwahiyo sioni sababu ya kusita kutoa kiungo changu kwaajili yake"
"Oh basi vizuri lakini hapa utakaa kwa siku tatu mpaka pale hali yako itakapokuwa sawa sasa acha nikamuangalie mginjwa wako kwanza"
Daktari alimuacha Tresha humo na kutoka lakini kitendo cha kutoka aliingia Sasha na hakuingia humo kwa wema ila aliingia kwa shari maana alijua chanzo cha Stephan kuwa kwenye matatizo ni yeye Tresha.
"Hapo unahisi amani kabisa kuona Stephan amefumba macho na wajiona shujaa kutoa kifigo chako kumsadia lakini nikwambie tu Stephan ni mchumbaangu hilo wazazi wake wanalitambua sasa kama ulifanya mipango apigwe risasi na umtolee figo ili wazazi wake wakuamini basi sahau mama"
"Samahani dadaangu mbona unafika mbali hivyo na maneno gani hayo unaongea.!?"
"Utajua wewe lakini ukweli ni huo Stephan humpati na nakusihi ukae nae mbali kabisaa la sivyo yatakukuta makubwa"
Sasha alimaliza kuzunguma na kutoka nnje huku akimuacha Tresha akitafakari maneno yake lakini kwa kiasi fulani Tresha ilimuuma maana nae alikuwa akimpenda Stephan.
Basi Sasha alitoka nnje mpaka walipo wazazi wa Stephan ila alisikia baba Stephan akiongea mazuri kimuhusu Tresha.
"Yaani mabinti wenye moyo kama huyu ni wachache sana, amediriki kutoa figo kwaajili ya kijana wangu kweli anastahili pongezi"
Maneno hayo kutoka kwa baba Stephan yalipenya vyema kwenye ngome za masikio ya Sasha na hii kitu ilimuuma sana, alitamani hizo sifa angepata yeye ili kuongeza upendo kwa wakwe zake hao watarajiwa.
"Lakini baba mimi sioni maana ya hizo sifa mnazompa huyo binti kwasababu yeye ndiye kasababisha matatizo alitakiwa hata apelekwe polisi tu"
Sasha sasa aliona amkandamize Tresha na bahati nzuri mama mkwe alikuwa upande wake akimuunga mkono.
"Ni kweli kabisa huyu binti alitakiwa afungwe"
"Unajua mke wangu hii ni ajali kama ajali nyingine sasa sioni sababu ya kufika huko kote hapa cha muhimu ni kushukuru Mungu kijana wetu amepata matibabu"
Basi ilikuwa ni hivyo ila Sasha alijikuta hapendi kabisa kuona Tresha anapata sifa, alichofanya ni kuaga anatoka lakini safari yake ilimfikisha kwenye jopo moja la manesi, alimvuta nesi mmoja pembeni na kupanga nae njama.
"Lakini dada mbona nashindwa kukuelea unamaana gani.!?"
"Sikia nikwambie nesi shika hii laki moja kama kianzio cha kazi sasa ninachotaka umchome sindano huyo binti niliekwambia na hakikisha sindano hiyo ukimchoma anakufa au kuwa kichaaa"
"Basi aina shida mimi kuuwa siwezi ila atakuwa kichaa, kazi yako itafanyika leo leo"
Nesi kwa tamaa ya fedha alichukua na kuichimbilia mfukoni bila wenzake kumuona.
Yalikuwa ni maamuzi magumu aliyochukua Sasha na hiyo yote ni kumkomesha Tresha, basi kazi ilifika sehemu husika na ilipotimu saa nne usiku familia yote iliondoka na muda huo ndio yule Nesi aliona autumie kuanza kazi yake huku masikini Tresha hana ili wala lile....ITAENDELEA......
- Mh ni huzuni sana lakini mimi sijui kama huyo nesi atafanikiwa au laa lakini tukutane sehemu ya 12 kujua nini kitafuata hapo...
