Mtunzi...........Official Dully
Mkasa....wa....kusisismua
Sehemu Ya {10}
ILIPOISHIA..
Tresha haraka alitoka nnje mpaka lilipo geti na kufungua lakini alikutana na kijana mdogo wa makamo ambe ameshika box na box hilo lilikuwa na chakula ndani, Tresha alilipokea bila kujua limetokea wapi na kurudi ndani hata Stephan alipoliona box hilo alishangaa na kumuuliza Tresha amepatiwa na nani....ENDELEA...
Baada ya Stephan kumuuliza Tresha chakula hicho amekipata wapi basi Tresha alikifungua ndani na kuangalia lakini alijikuta akitabasamu baada ya kukuta chakula kilichokuwa humo ni chakula alichokuwa akikipenda sana.
"Wow alafu hiki chakula nakipenda sana jamani tangu nikiwa kwa shangazi nilikuwa nakipika sana mh alafu kinanukia vizuri"
Tresha alikisifia kile chakula huku akiingiza mkono na kuchota ili apeleke mdomoni lakini Stephan alimshoka mkono.
"Unataka kula unajua nani amekuletea au ni uroho tu, kama kimewekwa sumu au mtu kaweka mambo yake mabaya utajuaje alafu hata hufikirii hilo kabisa.!!"
Stephan alizungumza kisha alikichukua kile chakula kutoka mikononi mwa Tresha na kuelekea nacho jikoni.
"Stephan unataka kufanya nini mbona sikuelewi, mimi najua chakula hiki atakuwa ameniletea rafiki yangu Gidion.!!"
"Utajua wewe na rafiki yako, kama unataka chakula hiki basi ni ruhusa kwenda supermarket ukanunue au ununue vitu utengeneze mwenyewe ukiweza lakini sio kula hovyo ikiwa hujui aliekuletea anania nzuri na wewe au mbaya"
Stephan hakutaka kuchelewa alikitia kile chakula kwenye dustib ya uchafu na kufunika lakini alipotoka sebuleni hakumkuta Tresha.
"Tresha...Treshaaaa.!!"
Alianza kuita huku akiwa na wasiwasi kidogo, aligonga chumba anacholala Tresha lakini ukimya ulitawala, alifungua mrango na kuingia ila hakumkuta na hiyo ikamuongezea wasiwasi zaidi.
"Sasa huyu Tresha mbona anaanza vibweka tena, atakuwa ameelekea wapi au ndio amekasirika baada ya kutupa kile chakula.!!?"
Stephan alijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu sahihi ila alipotoka nnje alimkuta ameketi barazani huku ameshika tama kuashiria alikuwa na mawazo sana.
"Shiiit inamaana wakati wote nakwita hunisikii au unafanya kusudi alafu Tresha sijui una nini siku hizi ok nambie nini kimekufanya uwe hivyo wakati kama chakula nimekwambia nenda supermarket kanunue"
"Amna sijakasirika pia hata ulivyotupa kile chakula sijali lakini nimewakumbuka tu wazazi wangu ndio maana unaniona nipo kwenye hali"
"Oh pole sana"
"Asante ila nipe hiyo pesa nikanunue kile chakula maana sio kwamba nimekwambia nimekumbuka wazazi wangu ukafikiri nimesahau kuhusu kile chakula haya nipatie pesa niende haraka"
"Ok sawa ngoja nikupe"
Stephan bila ubishi alimpatia Tresha pesa lakini alipomtazama machoni aliona kuna kitu Tresha alitaka kuzungumza.
"Tresha hebu subiri mbona kuna kitu nakiona kwenye macho yako haya hebu niambie ni nini unataka kuniambia kuwa free kabisa mimi ni wako"
Stephan alizungumza huku akimkazia macho Tresha lakini Tresha kwa aibu hakutaka kusema alibaki kutazama chini lakini mwisho uvumilivu ulimshinda, kwa kitendo cha haraka alimkiss Stephan shavuni na kuinuka kuelekea lilipo geti.
"Hey Tresha mbona unakimbia sasa ok basi subiri nikupeleke kwa gari maana huu ni usiku alafu wewe ni mtoto wa kike inaweza kuwa hatari kwako"
"Hapana nitaenda mwenyewe sio mbali sana dakika kumi tu zitatosha kwenda na kurudi kwahiyo usiwe na wasisi kabisa"
"Ok"
Stephan ilibidi akubaliane na maamuzi ya Tresha lakini hakutaka kumuacha aende mwenyewe alianza kumfuatilia kwa nyuma ili kumpa ulinzi bila Tresha mwenyewe kutambua.
Tuache huko kwanza tuje kwa Joyce ambae alikuwa na mawazo sana hasa juu ya Stephan na kumbuka alikuwa akimpenda kweli sio kama wanaume wengine alikuwa akiwatamani lakini Stephan alimpenda kweli kutoka moyoni na aliona ndiye mwanaume anaefaa kwenye maisha yake kujenga nae familia.
"Yaani huyu mwanamke aliepokea simu ya Stephan ni nani mbona kama anataka kunipanda kichwani jamani daaah.!!"
Joyce masikini alikuwa akiteseka kwa mawazo ila akiwa hapo aliingia mdogo wake Stellah na kama kawaida yake aliingia kwa lengo la kunchunguza Joyce.
"Eheeee haya wewe kijuso umefuata nini hapa.!?"
Joyce baada ya kumuona Stellah alimuuliza lakini Stellah hakujibu kitu, macho yake yalikuwa yakitazama simu ya dada yake iliyokuwa kitandani.
Simu ya Joyce ilikuwa imeseviwa picha ya Stephan kwenye screen saver na Stellah aliiona ile picha hivyo alijikuta akitabasamu mpaka Joyce alishtuka na kuichukua simu yake.
"Mh dada huyo mwanaume mbona handsome hivyo yaani nimempenda haswaaa na kama huyo ndie mwanaume aliekuwa kwenye mipango yako basi umefanikiwa kupata mtu wa type yako kwa hilo nakuunga mkono kabisa nataka siku moja nikutane nae"
Siku hiyo maneno ya Stellah yalimkosha Joyce, alimwita karibu yake na kumkumbatia maana aliongea vitu vya maana ila wakiwa wamekumbatiana aliingia mama yao na kuliona pozi hilo.
"Mh leo maajabu paka na panya kukaa sehemu moja lakini sio mbaya inapendeza ila Joyce baba yako anahitaji kuongea na wewe"
"Mama kuna nini.!?"
"Mimi sifahamu ila anahitaji kuongea na wewe kwahiyo njoo utajua amekuitia nini"
Mama alimaliza kuongea na kutoka nnje akimuacha Joyce kwenye wasiwasi mkubwa sana.
Basi ilibidi wote watoke Joyce akiwa katangulia na Stellah akiwa nyuma, walifika mpaka sebuleni lakini walimkuta baba yao ameketi huku akiwa mwingi wa hasira na hapo Joyce akajua tayari kimenuka, zile habari Stellah alizozitoa na kumwambia mama yake huenda zimefika kwa baba.
"Abee baba nasikia umeniita.!?"
Joyce alizungumza huku akiwa mwenye hofu sana.
"Sasa nimekwita ndio ukae mbali hivyo, hebu sogea hapa karibu nina maswali nataka kukuuliza"
Sauti nzito iliyomtetemesha na kumpa hofu Joyce ilisikika kutoka kwa baba yake.
Joyce taratibu akiwa mwenye hofu alisogea mpaka alipo baba yake lakini kilichofuata hapo alipigwa kofi moja zito lililompata vyema sikioni na kumuangusha mpaka chini huku sikio la upande aliopigwa likipoteza uwezo wa kusikia kwa muda.
**************
Upande wa Stephan alikuwa taratibu kumfuatilia Tresha kwa nyuma bila mwenyewe kujua lakini Tresha alipofika njiani kuna mwanaume alifika na kumzibia njia na alipomtazama usoni alikuwa ni Gidion.
"Gidion.!?"
"Yah ni mimi kipenzi chako, nilikuwa nakusubiri hapa tangu saa kumi na mbili utoke nnje lakini kimya ila nashukuru umetoka sasa niazime muda wako japo kidogo tuongee"
Gidion alizungumza kwa kujiamini lakini wakati huo hakujua Stephan alikuwa nyuma akiwatazama.
"Lakini Gidion muda hauruhusu bhana kuna sehemu naenda nataka niwahi kurudi si unajua mtu ninaeishi nae ni mkorofi sana sasa kama nitachelewa hatonielewa"
"Amna bhana nipe dakika mbili tu"
"Ok sema"
"Unajua Tresha wewe ni binti mrembo sana ambae kila mwanaume kamili atakaekutazama basi lazima ataingiwa na hamu ya kuwa na wewe na mimi ni mmoja wapo ambae natamani nafasi hiyo niipate, najua unaweza kushangaa haya ninayosema au unaweza usielewe lakini ukweli nimetokea kukupenda"
"Mh.!!"
"Kweli yaani amini maneno yangu nakupenda sana na nipo tayari kufanya chochote kwaajili yako, nitakuvisha pete na mwishoe kukuoa uwe mke wangu"
Gidion alitupia swaga ambazo zilimfanya Tresha awe kimya lakini mwisho alizungumza.
"Hapana Gidion utanisamehe maana kuna mtu tayari yupo kwenye hisia zangu na tayari hata yeye ameweka wazi kuwa ananipenda kwahiyo samahani sana"
Tresha ilibidi ajikaze kutoa jibu hilo lakini kwa upande fulani alihisi huruna.
Alipiga hatua kadhaa ili kuondoka lakini ghafla Gidion alimshika mkono na kumvuta kisha kumkumbati kwa nguvu kitendo kilichomfanya Stephan ashikwe na hasira sana.
"Gidion hebu niache tafadhali mbona hivyo jamani.!!"
Tresha sasa ilibidi atumie nguvu kujinasua kwenye mwili wa Gidion ila wakati huo huo Stephan alifika na kumshika mkono Tresha kisha alimvuta upande wake.
"Wewe ni mwanaume au, mbona unashindwa kuwa muelewa ukiwambiwa kitu!"
"Unaongea hivyo ukiwa kama nani hebu acha kuingilia mahusiano yetu nisije kukuharibu, unajua huyu demu nimetoka nae wapi hebu pita na mambo yako bro"
Gidion ilibidi aje juu akidhani huenda Stephan ni mpita mjia ila hakujua ndie mwanaume aliekuwa kwenye hisia za Tresha.
"Ok sawa umetoka nae mbali lakini sitaki kukuona ukimsogelea tena la sivyo nitakuchafua ujute kumfahamu"
Stephan ilibidi aongee kiume, alimshika mkono Tresha na kuondoka nae lakini kitendo cha kumpa ngongo Gidion lilikuwa ni kosa kubwa sana.
Kilichofuata hapo ni mishindo miwili ya risasi kusikika na mwisho ilionekana gari ya Gidion ikitoka eneo hilo kwa kasi sana huku kwa mbali sana sauti ya Tresha ilisikika ikilia huku ikitaja jina la Stephan.
Masikini sijui nini kimetokea hapo lakini tuje moja kwa moja kwenye nyumbani kwa wazazi wa Stephan na usiku huo walikuwa wamemualika Sasha kwaajili ya kuzungumza nae ila kikubwa walichotaka kuongea nae ni kuhusu kuolewa na Stephan.
"Mama na Baba kama ambavyo mlivyoanza kusema na kuniomba niolewe na kijana wenu ila na mimi nawaambia kwa hilo msijali kwasababu kabla hata hamjapanga hili mimi nilishampenda kijana wenu zamani sana"
"Wow basi vizuri ni habari nzuri sana"
Mama Stephan alijikuta akifurahi lakini mume wake alikuwa kimya na ndipo alimuuliza nini kimemfanya awe kimya.
"Amna lakini niliongea na Stephan kuhusu hili ila ameniambia kuna mwanamke anampenda sasa sijui ni mwanamke gani ila Sasha mwanangu sisi kama wazazi wa Stephan tunakuhakikishia lazima utaolewa nae wala usijali"
"Nitafurahi sana jamani maana nampenda sana Stephan mimi"
Sasha sasa kwa upande wake aliona matumaini yamerudi ya kumpata Stephan na kama support tayari anayo kwa maana wazazi wa Stephan wapo upande wake sasa ni muda wake wa kujiongeza ili kuwafurahisha zaidi wakwe zake watarajiwa.
***************
Huku kwa Joyce bado kesi ilikuwa inaendelea baada ya kupigwa kofi aliamuriwa ainuke na kupiga magoti, hakusita alifanya kama alivyoambiwa kisha maswali yalianza juu yake.
"Unajua kuna baadhi ya watu hata majirani walikuwa wakiongea mengi kukuhusu, niliambiwa mwanao malaya anabadilisha wanaume kila siku lakini mimi nikapuuzia na kudharau ila leo hii mama yako na mdogo wako wananiambia tena na mimi kwa macho yangu nashuhudia aisee Joyce umenikosea sana mwanangu..!!!"
"Lakini baba mi......."
"Keleleee tena unyamaze kabisaaa sitaki ufunue domo lako kuongea kabla sijakuruhusu la sivyo nitaukata huo mdomo panya mdogo wewe!!"
Baba Joyce alikuwa mkali haswaa na familia nzima ilikuwa ikimuogopa maana akipandishaga hasira hua hataki kumsikiliza mtu yeyote.
"Haya sasa nataka kukuuliza ninachokisikia kwenye midomo ya watu kukuhusu ni kweli au wanadanganya.!?"
"Ba..baba unajua mimi sifahamu watu wananipenda vipi au wananichukia vipi kwahiyo wanaweza kuzusha ili kuniharibia mimi na kuchafua sifa ya familia yetu lakini ukeli sina hizo tabia kabisa"
"Ahaaa auna eeh ok acha tuone"
Baba Joyce alitoa bahasha ndogo mfukoni mwake na ndani ya bahasha hiyo kulikuwa na picha nyingi zikimuonesha Joyce akiwa na wanaume mbali mbali wakiingia hotelini na kwenye magesti na baada ya kutoa picha hizo alizimwaga chini mbele ya Joyce.
"Sawa ulikuwa unasema wanakusingizia sijui hawakupendi ila nataka kujua hizo picha ni picha za nani na hao wanaume ni wakina nani au wame edit.!?"
Joyce hakuwa na neno la kujibu zaidi ya kukaa kimya maana ukweli tayari ulikuwa wazi hakuwa na uwezo wa kujitetea tena.
"Si nakuuliza wewe.!?"
"Ni kweli baba huyo ni mimi lakini hayo mambo nimeacha kwa sasa sifanyi tena ila kuna mwanaume ambae nampenda sana nahitaji kumleta kwenu mumjue na ndie atakaenioa"
Joyce ilibidi ajikaze kuzungumza ila baba yake hakusema kitu alibaki kimya mpaka pale mama yake alipoingilia.
"Hayi ndio mambo ambayo mzazi yeyote anahitaji kusikio kutoka kwa binti au mtoto wake sasa kama kuna mwanaume unampena basi mlete hapa tumtambue lakini sio kubadili wanaune kama nguo mwisho utuletee maradhi kwenye familia".
Maneno ya mama yalimfanya Joyce atabasamu, alimfuata mama yake na kumkumbatia kwa furaha sasa alichokiwaza kwa wakati huo ni harakati za kumpata Stephan, amueleze ukweli kama anampenda na kisha afanye taratibu za kumtambulisha kwa wazazi wake wamtambue na swala la ndoa lipite...ITAENDELEA.....
Unafikiri nini kitafuata hapo...mambo ni moto ila hatujui upande wa Stephan mambo yapoje maana tumesikia mishindo ya risasi sasa hatujui kimetokea nini....tukutane sehemu ya 11 kujua nini kinafuata...
