Jina....TABASAMU LA UCHUNGU
Mtunzi...... Official Dully
Mkasa....wa...kusisismua

            Sehemu Ya {09}

ILIPOISHIA..

Ochu alikuwa tayari amepanic, alitazama mezani aliona kuna chupa tatu za bia hivyo alichukua chupa moja iliyokuwa tupu na bila kuchelewa alimpiga nayo Stephan kichwani, hali iliyopekea maumivu makali sana kwa Stephan na damu zilianza kumtoka kwa wingi sana....ENDELEA....

Hali ilikuwa tayari imechafuka katika club hiyo, kila mmoja alihamaki kwa tukio hilo la Stephan kupigwa na chupa kakini upande wa Ochu baada ya kufanya tukio hilo alimshika mkono Joyce na kumtoa nnje kwa nguvu lakini walipofika kwenye gari Joyce aligoma kupanda.

"Hebu niachie mkono wangu kwani lazima kwenda na wewe, alafu ujue mimi sio mke wako, umeona ulichomfanya Stephan ni kizuri eeh.!?"
     Joyce alipanic na kumshushia Ochu matusi mazito lakini Ochu hakujali kutukanwa alimuingiza Joyce kwenye gari kwa nguvu kisha nae alipanda na kutoka eneo hili.

"Yaani sitaki tena kukuona karibu na yule mwanaume la sivyo utamponza naweza hata kumuuwa kwahiyo kwa usalama wake naomba kaa mbali nae"
      Wakiwa njiani Ochu alianza kumpa vitisho Joyce lakini Joyce mawazo yake yalikuwa kwa Stephan, hakufahamu anaendeleaje maana alimuacha damu nyingi sana zikimvuja.

Upande wa Stephan baada ya kupigwa na kuona watu wanazidi kumjalia bila kumpa msaada alitoka nnje na kuchukua gari yake kisha safari ilianza kuelekea kwake hakutaka kwenda hospital kwasababu ya umbali hivyo aliona awahi kwake kupata huduma ya kwanza.

"Ila huyu mshenzi lazima nitamtafuta asijione mashinda kabisa kama alikuwa hanijui mimi ni nani basi nitamfuza adabu alafu atambue kuna watu sio wa kuwaingilia kizembe"
      Yalikuwa ni mawazo ya hasira yaliyopita kichwani kwa Stephan, mkono mmoja alishika jeraha lake lisiendee kutoa damu na mkono mwingine ulikuwa na jukumu la kuongoza usukani.

Upande wa Tresha akiwa ametulia akimsubiri mwanaume aliekutana nae ufukweni afike mara alisikia honi ya gari nnje, hakutaka kupoteza muda alitoka haraka na kwenda kufungua geti ndipo alikutana na gari ndogo nyekundu ikiwa imesimama.

"Itakuwa ni yeye huyu.?"
        Tresha alijisemea huku akisogelea lile gari na muda huo huo mrango wa gari ulifunguliwa na kushuka mwanaume, alipomtazama alikuwa ni yeye aliekuwa akimsubiri.

"Nimechelewa sana eeh dadaangu.?"
     Yule mwanaume baada ya kushuka alijongea mpaka karibu na Tresha kisha alisimama mbele yake na kumtazama usoni, kitendo kilichopelekea Tresha atazame chini kwa aibu.

"Hapana hujachelewa"

"Ahaaa ok ila hata hivyo siwezi kukaa sana hapa nimekuja kukuona na kukwambia machache ambayo yamekuwa yakininyima amani kabisa ndani ya moyo wangu"

"Ni yapo hayo.!?"
      Tresha aliuliza lakini mpaka wakati huo alikuwa bado hajaelewa mwanaume huyo alikuwa na dhamira gani kwake.

"Kwanza nataka kulifahamu jina lako, mimi naitwa Gidion sijafahamu wewe unaitwa nani?"

"Ah mimi naitwa Tresha"
      Tresha alijitambulisha na kumfanya Gidion atabasamu huku akilimwagia sifa kedekede jina la Tresha ambae mwenyewe alibaki kucheka kwa aibu.

"Mbona la kawaida tu jamani halina uzuri wowote"

"Ah kwako wewe halina uzuri ila kwangu naliona zuri sana pia hata wewe ni mrembo yaani sijawahi kufikiri kama nitakutana na mwanamke mrembo kama wewe kwenye ulimwengu huu jamani"
     Gidion alianza kumlainisha Tresha taratibu huku akimsogelea zaidi karibu na taratibu alianza kupeleka mdomo ili kumkiss.

Tresha alikuwa ametulia hana ujanja na mambo hayo kwake yalikuwa mageni kabisa lakini wakati Gidion anataka kufanya kitendo hicho ghafla walimulikwa na mwanga wa gari ambalo lilikuwa linakuja upande walipo wao.

Kwa taharuki Gidion alijitoa mbele ya Tresha hasa alipoona gari hilo linakaribia walipo wao alitambua huenda ni gari la nyumba hiyo.

"Samahani Tresha tutaonana siku nyingine nachelewa nilipotakiwa kwenda, kwaheri"
     Gidion aliaga na bila kuchelewa alirudi lilipo gari lake na kupanda kisha alilitoa hapo kwa kasi ya ajabu sana.

Gari iliyokuwa inakuja hapo ilikuwa ni gari ya Stephan na tukio lililokuwa linaendelea kati ya Tresha na mwanaume asiemfahamu aliliona ila hakulizingatia sana kutokana na hali yake kuwa mbaya.

Aliingiza gari mpaka ndani na kupaki sehemu husika lakini aliposhuka ndipo Tresha aliona hali aliyokuwa nayo Stephan na ilimchanganya kwa kiasi kikubwa mpaka alijikuta machozi yakimtoka.

"Stephan nini kimekukuta mbona hivyo jamani.!?"
      Tresha ilibidi amuulize Stephan huku akiwa na hofu lakini Stephan hakutaka kumjibu, aliingia ndani kwa mwendo wa kuyumba maana alikuwa ameishiwa nguvu baada ya kupoteza damu nyingi.

Alifika sebuleni lakini hakuweza kuelekea chumbani, alianguka chini na kupoteza fahamu, hali iliyomfanya Tresha achanganyikiwe.

"Stephan....Stephan hebu amka tafadhali uniambie nini kimekukuta mbona umeumia kiasi hicho.!!"

Tresha alikua heelewi afanye nini kwa wakati huo ila alipotuliza akili ndipo alikumbuka kumfayia huduma ya kwanza, alimtazama mapigo ya moyo bado yanadunda na kujihakikisha Stephan bado ni mzima ila alikuwa amepoteza fahamu.

Huku kwa Joyce alifikishwa mpaka kwao na gari ilisimama kwa mbali kidogo, Ochu alishuka na kumfungulia mrango Joyce kisha alimtaka ashuke.

"Sasa kama nilivyokwambia wewe ni wangu pekeyangu sitaki kukuona na mwanaume mwingine ila kama unataka kuhatarisha maisha ya hao wanaume basi kaa karibu nao alafu utajua nafanya nini"

"Hivi Ochu kwani wewe unajiona nani hasa kwangu, umenitolea barua kusema labda ni mchumba wangu, mume wangu au mpenzi wangu.!?"

"Hayo mimi sitaki kujua ila habari ni hiyo wewe ongea lakini mimi nafanya kwa vitendo"
     Ilikuwa ni kauli ya mwisho ya Ochu kisha alirudi kwenye gari yake na kuondoka akimuacha Joyce akimsindikiza kwa macho.

"Yaani wanaume wengine sijui wapoje kama wanyama, sasa sijui Stephan wangu anaendelaje jamani.!!"
      Joyce hakuwa na muda wa kupoteza alitoa simu yake na kumpigia Stephan lakini simu iliita bila kupokewa, alipiga tena na tena mpaka alichoka.

"Najua tu lazima atanikasirikia kwa upuuzi ya yule mjinga ila sawa dawa yake inachemka atajuta kinifuatilia"

Joyce hakutaka kuendelea kubaki hapo, alijongea taratibu kuelekea ilipo nyumba yao huku mawazo yake yakiwa kwa Stephan.

                ****************

Ok tutoke huko tuje pembezoni mwa mji ambapo huku kulikuwa na msitu mkubwa wenye kutisha na ndani ya msitu huo alionekana shangazi na mume wake wakitembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine na shangazi ndiye alikuwa mbele kuongoza safari.

"Jamani mke wangu hivi huoni kama ni hatari usiku huu, sasa huyo mganga ni mganga gani anatoa huduma usiku.!?"

"Yaani ni heri twende sahizi tunapata huduma bila kugasiwa na huduma ya uhakika lakini tukienda mchana anakuwa na wateja wengi sana mwisho unapata huduma haraka haraka isiyo na ubora"

Shangazi alizidi kukatiza msitu huku nyuma mume wake akimfuata na lengo la kwenda kwa mganga ni kumkomesha Tresha ambae yeye ndie chanzo mpaka wao kukosa msaada kwa Stephan.

Kwa mwendo wa takribani masaa mawili walifika katika kijumba kimoja kidogo kilichokuwa msituni na nnje ya kijumba hicho kulikuwa na moto ukiwaka huku pembeni ya moto huo alionekana mtu ameketi huku amejikunja akiota moto.

"Habari yako bibi mjuu wako nimekujaaaa"
      Shangazi alipaza sauti na kumfanya yule mtu aliekuwa akiota moto asimame na kuingia ndani ya kijumba kile bila kuwasemesha.

"Mke wangu una uhakika hapa ni salama kweli mbona naanza kuogopa.!?"

"We usijali ni salama hakuna chochote kibaya ambacho kitatokea"
      Shangazi alimtoa hofu mumewe ambae alionekana kuogopa sana hata mwendo wake alionesha alikuwa ni mtu mwenye hofu sana.

Walijongea mpaka ulipo ule moto kisha shangazi alipiga magoti na mume wake alifanya hivyo hivyo maana alikuwa mgeni na mambo hayo ila shangazi alionekana ni gwiji kila taratibu alikuwa anazijua.

Baada ya kupiga magoti kwa muda walisikia sauti iliyojaa mikwaruzo ikiwaita ndani, waliinuka na kuingia kwenye kijumba hicho ambacho kilikuwa na mwanga hafifu wa kibatari.
     Waliketi chini na sauti hiyo ilisikika tena ikiwataka waeleze shida yao na ndipo shangazi alianza kueleza mwanzo mpaka mwisho hakuficha chochote kuhusu Tresha.

"Kwahiyo mnataka mumfanye nini binti huyo.?"

"Bibi sisi hatutaki kumuuwa ila tunataka ateseke sana sasa sijui utachagua adhabu gani ya kumpatia lakini tunachotaka ateseke mpaka aichukie dunia"
      Shangazi alizungumza lakini mume wake alikuwa kimya akisikiliza kile mke wake anasema.

"Basi hilo limekwisha kabisa, tokeni nnje zungukeni nyumba ya hii nyumba kuna makaburi matatu sasa mnatakiwa mfukue hilo kaburi la kati kuna dawa mtaiona kwenye chupa ndogo nyeusi, dawa hiyo ni unga mweupe ambao mtamuwekea huyo binti kwenye chakula"

"Lakini bibi mbona huyo binti atuishi nae sasa unafikiri tutamuwekeaje hiyo dawa?"

"Akili kichwani mwenu haya muende sasa"

Shangazi na mume wake walitoka na kuzungunza nyuma ya nyuma hiyo, walifanya kama walivyoambiwa na kweli dawa waliipata sasa kazi iliyobaki kwao ni moja tu kuhakikisha wanatumia mbinu zote ili kumuwekea Tresha dawa kwenye chakula.

Wakati hayo yanaendelea Tresha alikuwa hana ili wala lile, alimfanyia Stephan huduma ya kwanza kisha alimpeleka chumbani kwake na baada ya hapo alitoka nnje ili kusafisha damu kwenye gari na ndipo alikuta simu ya Stephan.

Aliichukua ili kuipeleka ndani na ndipo ilianza kuita, jina lilisomeka Joyce juu ya kioo, hakutaka kuipuuza alipokea.

"Jamani Stephan wangu unaendeleaje mbona nilikupigia simu ulikuwa hupokei ujue unanipa wakati mgumu sana.!!"

"Samahani Stephan yupo ndani amepumzika piga baadae akiamka"

"Wewe ni nani unapokea simu ya mpenzi wangu.!?"
     Joyce ilibidi aulize kwa jazba lakini Tresha hakutaka kuendelea kumsikiliza maana alijua kifuatacho ni mzozo na matusi, alikata simu na kuzima kabisa kuepusha shari.

               ****************

Asubuhi kunapambazuka Tresha alikuwa wa kwanza kuamka, aliandaa kifungua kinywa na kupeleka chumbani kwa Stphan, ilimkuta tayari ameamka hivyo aliweka mezani na kumsogelea Staphan.

"Unaendeleaje na hali Stephan.?"

"Hali yangu aikuhusu chukua chai yako utoke nnje sihitaji hata kukuona"
      Stephan alizungumza hayo na kumfanya Tresha asielewe amepatwa na nini mbona amebadilika ghafla.

"Steph......"

"Nimesema tokaaa sihitaji kukuona chumba kwangu au mpaka niongee kingereza, haya chukua chai yako utoke nnje"

Tresha hakuwa na namna alichukua chakula alicholeta na kuelekea nacho jikoni ila kichwani kwake alishindwa kuelewa Stephan amepatwa nini na kuna muda aliwaza huenda ukichaa umemuanza kutokana na jeraha lililokuwa nalo kichwani.

Basi mawazo siku hiyo yalikuwa kwake lakini akiwa kwenye dimbwi la mawazo simu yake ilianza kuita na aliekuwa anapiga alikuwa ni Gidion, alimpokelea na kumsikiliza alikuwa na jambo gani asubuhi hiyo.

"Hello Gidion mambo?"

"Powa kipenzi ila samahani kwa kilichotokea jana nilikuacha kwenye mataa kuna sehemu nilikuwa nawahi lakini leo nitakuja tutaongea vizuri kipenzi"

"Sawa kakaangu"

"Ah jamani kaka tena mbona unaanza kunibania hebu acha zako alafu......."

"Hebu subiri nitakucheki"
        Tresha alikata simu baada ya kusikia kishindo sebuleni, alitoka kwenda kuangalia kishindo hicho kimetokana na nini na ndipo alimkuta Stephan ameanguka chini huku akijaribu kujiinua.

Alimuendea haraka na kumshika ili kumuinua lakini Stephan hakuhitaji msaada wake zaidi alimsukuma..

"Niache na ukae mbali na mimi"

"Lakini Stephan mbona umebadilika ghafla shida nini jamani mbona sio Stephan yule ambae namjua mimi yaani umebadilika sana jamani.!!"

"Nishangae nimebadilika ukimaliza uende zako sitaki kukuona kwenye nyumba yangu tena maana tayari umefanya nyumba yangu kama yako na wanaume tayari umeanza kuwaalika sasa sihitaji kukuona hapa uende tu kwa shangazi yako"

Maneno ya Staphan yalimfanya Tresha awe kimya na ndipo alitambua nini ambacho kimemkera Stephan, ilibidi apige magoti na kumsogelea Stephan alijua amemkosea pakubwa sana..

"Samahani sana Stephan najua nimekukosea ila yule mwanaume sina uhusiano nae wowote tulikutana beach alinipa namba yake ndio tukawa tunawasiliana lakini hakuna chochote kinacho endelea"

"Unajua sana kujitetea eeh alafu kumbuka wewe ni mtu wangu nimekununua kwahiyo sihitaji ufanye vitu bila amri yangu ila kinyume na hapo basi nitakurudisha ulipotoka"
      Stephan alitoa vitisho ila ukweli kwenye nafsi yake alikuwa akimpenda sana Tresha lakini hakuliweka wazi hilo ila aliona aende nae taratibu ipo siku atamueleza ukweli.

Basi furaha ilirudi tena kwa wawili hao lakini Tresha hakuacha kuwasiliana na Gidion kwa siri ila ilipofika kwenye swala la kukutana Tresha alikuwa mgumu akihofia kumkwaza Stephan.

Kadri siku zilivyozidi kwenda mawasiliano yao yalipamba moto pia Stephan alilijua hilo ila aliona akichelewa sana ataambulia manyoya sasa ndipo alipanga usiku mmoja amueleze ukweli Tresha kama anampenda.

Siku hiyo bhana Tresha alikuwa hana ili wala lile, alikuwa zake jikoni akipika lakini ghafla aliingia Stephan na kumkumbatia kwa nyuma, jambo ambalo lilimshangaza sana Tresha na haikuwa kawaida.

"Stephan unafanya nini sasa.!?"
      Tresha ilibidi amtoe Stephan nyuma yake na ndipo Stephan alipiga goti huku mkono akiwa na ua jekundu.

"Nakupenda sana Tresha nahitaji uwe mpenzi wangu"

Stephan sasa alitoa lake la moyoni na upande wa Tresha alibaki ameduwaa maana hakutegemea ingefika siku kama hiyo.
    Wakati wapo kwenye pozi la upendo walisikia geti ikigongwa.

"Sahani Stephan ngoja nimuangalie nani anagonga geti"

Tresha haraka alitoka nnje mpaka lilipo geti na kufungua lakini alikutana na kijana mdogo wa makamo ambe ameshika box na box hilo lilikuwa na chakula ndani, Tresha alilipokea bila kujua limetokea wapi na kurudi ndani hata Stephan alipoliona box hilo alishangaa na kumuuliza Tresha amepatiwa na nani....ITAENDELEA...

- Mambo yameanza kuwa moto ila chakula hicho hajakileta shangazi kweli...mh nina wasi ila sifahamu kama ni kweli au laa lakini majibu utayapata sehemu ya kumi ya mkasa huu wa kusisimua...