Jina....TABASAMU LA UCHUNGU
Mtunzi........Official Dully
Mkasa....wa...kusisismua

            Sehemu Ya {08}

ILIPOISHIA..

Alilifikia geti na bila kuchelewa alifungua mrango huku akiwa na uso uliopambwa na tabasamu lakini tabasamu lake liliyeyuka ghafla baada ya kumuona shangazi yake pamoja na mjomba yake, hata shangazi nae alishangaa kumuona Tresha hapo na kila mmoja alibaki kwenye maswali mengi akijiuliza kuhusu mwenzake....ENDELEA...

Tuanzie kwa Stephan ambapo aliulizwa na baba yake kuwa ni mwanamke gani ambae anampenda lakini Stephan alibaki kimya mpaka pale baba yake alipomuuliza tena.

"Kwahiyo inamaana huwezi kunijibu mwanangu, kama una mwanamke unampenda basi tuambie ili maandalizi ya harusi yafanyike"

"Baba hebu acha habari hizi, siku nikiwa tayari kukwambia basi nitakwambia lakini sio kwa sasa alafu kuna mtu amenipigia simu ananisubiri nyumbani kwahiyo naomba nimuwahi"
      Stephan alimuacha baba yake njia panda, alitoka haraka mpaka nnje, alijipakia kwenye gari yake na kuanza safari lakini kichwani kwake alikuwa na mawazo mengi hasa alipokumbuka kauli ya baba yake.

Upande wa Tresha na shangazi yake bado walikuwa wakitazamana kama hawajuani lakini Tresha alivunja ukimya na kumuuliza shangazi yake amefuata nini hapo.

"Tunamuhitaji mwenye nyumba na sio wewe alafu sijui umefikaje hapa na kupokelewa kuishi sehemu nzuri kama hii.!?"
      Shangazi alizungumza kwa kujiamini na dharau lakini Tresha hakujali pia wakati huo hakumuhofia kabisa.

"Kwani ulifikiri kila mtu ana roho mbaya kama wewe na sijui kama utapata unachokitaka ni bora uende tu kuliko kupoteza muda"

"Hebu usinipigie kelele zako malaya mkubwa wewe naomba utuitie mwenye nyumba tuna shida nae na sio kutuwekea msura wako hapa uliokauka kama ngozi ya futi"
      Shangazi alizidi kuongea maneno ambayo yalimkera Tresha ila mume wake alikuwa kimya akiwatazama.

Wakati wanaendelea kuzozana Stephan aliwasili na bila kuchelewa alipaki gari yake kando kisha aliteremka pia mzozo ule uliuona japo hakuweza kusikia walikuwa wanaongea nini mpaka pale alipowakaribia.

"Hey jamani kuna nini hapa mbona naona kama kuna mzozo unaendelea shida nini.!?"
     Stephan aliuliza lakini alipomtazama shangazi alimkumbuka ndiye mwanamke aliemuitiaga polisi.

"Wewe mwanamke umefuata nini hapa kwangu, wewe si ndiye ulieniitia polisi.!?"
      Stephan alibaki na mshangao lakini shangazi hakuwa neno lolote la kuongea zaidi ya kukaa kimya huku kisubiri mume wake aseme kitu.

"Samahani Stephan kijana wangu huyu ni mke wangu nimekuja nae hapa kama tulivyoongea kwenye simu kuhusu swala lile"
    Mjomba ilibidi aingilie kati kumtetea mke wake maana liona akiacha mzozo uendelee wanaweza kukosa msaada.

"Ahaaa sawa kwahiyo wewe ndie mjomba wa Tresha eeh.!?"

"Yah ndiye mimi kabisa yaani huyu binti tumemlea tangu akiwa mdogo kwahiyo mpaka hapa alipofikia, wazazi wake wali......"

"Ok ok ok inatosha aina haja ya kuongea sana lakini ni vyema ukasema na kitendo ulichofanya kwa binti huyu cha kutaka kumbaka"
     Stephan hakutaka kupindisha maneno alianza kufukua ya nyuma ambayo yalishapita.

"Mbona huongei, ok tuachane na hayo mimi hua sisaidii watu wenye roho za wanyama kwahiyo kama mlivyokuja rudini hivyo hivyo na laiti kama ningejua basi nisingekuja kabisa"
     Stephan alimaliza kuonga na hakutaka kusikia chochote kutoka kwao, alirudi kwenye gari yake na taratibu uliingiza ndani kisha geti lilifungwa.

"Sasa mke wangu hapa msaada tumekosa kinachofuata ni nini"

"Mimi siwazi chochote hapa ila aliekuwa kwenye akili yangu ni huyu binti yaani leo wa kutufungia sisi geti, asiee hata kwa mganga nitamuendelea aiwezekani kabisa aoneshe dharau kwetu kiasi hiki"

"Lakini ni sawa mke wagu ana haki ya kufanya hivi maana tuliyokuwa tukimtendea sio madogo"

"Sasa ndio nitamfunza jinsi dunia ilivyo we subiri uone"

Shangazi na mume wake walichukuzana na kuondoka hapo wakiwa mikono mitupu maana walichotegemea hakikuwezekana lakini shangazi kwenye mafsi yake aliweka kisasi kizito kwa Tresha na aliapa kwenda kumfanyia dawa kwa mganga ili ampotezee muelekeo.

Sasa turudi ndani ya nyumba ambapo Stephan alipaki gari na kushuka, aliingia ndani na kukuta kumepambwa kila mahali pia mezani kulikuwa na keki ndogo ikiwa na jina lake..

"Wow umejuaje kama leo ni birthday yangu.!?"
     Stephan alimuuliza Tresha huku akisogelea keki na kuitazama, kiufupi aliipenda sana na ilitengenezwa kwa ustadi wa hali ya juu sana.

"Bwana kula hiyo keki mimi sina hata hamu ya kusherehekea tena maana siku yangu tayari imeingia doa na kwakua shangazi amepajua hapa basi atanisumbua kila siku"

"Usijali hatoweza kuja kukusumbua mimi nipo alafu kama unaona umeboeka sanaa basi jiandae tuelekee baharini tukapunge upepo maana hata mimi nikiboeka napenda sana kwenda sehemu hizo"

"Kweli eeh.!?"

"Yah ukienda huko ukirudi utakuwa sawa kabisa wala usijali niamini"

Maneno ya Stephan yalimtia hamu Tresha ya kwenda huko baharini, walikula keki na baada ya kumaliza walijiandaa na kutoka ila kabla hawajapanda gari Stephan alimtazama Tresha miguuni na kujikuta akiangua kicheko.

"Sasa hayo mandala ya kuendea bafuni ndio umeona yanafaa ya mtoko wakati viatu vipo ndani chumbani kwako kwenye kabati.!!"

"Bwana mimi siwezi ile miatu inaweza kuniangusha kwahiyo niache nimependa hivi na hata haya manguo nimevaa sina jinsi lakini pia ni mabaya kabisa"

"Hebu njoo huku"
       Stephan alimkamata mkono Tresha na kurudi nae ndani mpaka chumbani kwake na kufungua kabati ambalo lilikuwa na viatu vingi vya bei ghali.

Alimtafutia viatu vizuri na kumvalisha kisha alimshika mkono ili asianguke na kutoka nnje.

"Sasa hapo umetokelezea yaani umekuwa mrembo haswaa huitaji hata makeup"

Stephan alimwagia sifa lukuki Tresha ambae alijikuta akitabasamu, walijipakia kwenye gari na safari ilianza kuelekea kwenye fukwe za bahari kupunga upepo na kupoteza mawazo.

                 **************

Upande wa Joyce baada ya kufunga geti na kurudi ndani akimuacha Ochu nnje aliingia moja kwa moja chumbani kwake na kujilaza kitandani lakini muda huo huo aliingia Stellah na kuketi kando yake.

"Eheee kilichokuleta?"

"Amna dada ila nataka kukwambia tu wakati unaongea na yule mwanaume basi mama amekuona na yule mwanaume amemuona sasa subiri kesi ifike kwa baba"

"Kwani unafikiri naogopa sasa alafu ulichokuja kuniambia hata sikielewi hebu nenda zako bhana sitaki watu wambea hapa"

Stellah aliinuka na kuondoka zake na moja kwa moja alielekea chumbani kwa mama yake alimkuta yupo busy akisoma kitabu, alimsogelea na kuketi kando yake.

"Mama hivi mwanao ananionaje mimi yaani nikimsogelea karibu tu kosa, hataki nimwambia ukweli"

"Ukweli gani.!?"

"Kumbe unaishi na mwanao alafu hujui kitu yaani dada ana wanaume kama mvua kila siku anabadilisha na hiyo gari uliyoisikia hapo nnje ilikuwa ya mwanaume wake mwingine amekuja sasa kuwa makini mama la sivyo atawaingiza mpaka ndani"

Stellah siku hiyo aliona amwage umbea maana kukaa kimya alishindwa lakini wakati yote yanaendelea Joyce alikuwa mrangoni akiwasikiliza na baada ya kuridhika alirudi chumbani kwake, alichukua simu na kupiga namba ya Stephan.

Stephan akiwa hana ili wala lile, alikuwa busy kuendesha gari mara simu yake ilianza kuita, aliitoa na kutazama mpigaji jina lilisomeka Joyce juu ya kioo cha simu.
     Hakutaka kuipuuzia aliipokea na kumsikiliza alitaka kuzungumza nini.

"Habari yako?"

"Salama tu za kwako.?"

"Safi ila najua upo kazini nakuharibia pozi ila nilikuwa naomba kama inawezekana usiku wa leo tukutane kwenye ile club nina mengi ya kuzungumza na wewe Stephan"

"Ah nitaangalia muda kama utaruhusu nitakujuza tukutane ondoa shaka"

"Ok sawa"

Simu ilikatwa na safari iliendelea. Nusu saa baadae walikuwa wamefika ufukweni, walipaki gari sehemu husika na kushuka kisha walitafuta sehemu nzuri na kuketi ili kupunga upepo na story zichukue nafasi yake.

"Unajua Tresha kupiga story bila kinywaji inakuwa haipendezi kwahiyo naomba unisubiri hapa nikachukue juice pale ili story ziende vizuri"

"Ok sawa"

Stephan aliinuka na kuelekea mahali ambapo wanauza juice lakini wakati yeye anatoka na kumuacha Tresha kuna mwanaume alifika alipo Tresha na kuketi kando yake, alimsalimia na bila kusita Tresha aliitikia.

"Umependeza sana dada"

"Asante sana jamani"

"Lakini samahani naweza kupata namba yako ya simu kama hutojali maana nipo na haraka kuna sehemu naenda ila nikipata namba yako ya simu itapendeza sana"

"Sina simu mimi"

"Aaah dada hebu acha utani yaani mwanamke mrembo kama wewe unakosaje simu jamani ok fanya hivi chukua namba yangu hii baadae utaomba hata simu unitafute kisha mimi nitafanya mchakato wa kukununulia simu mrembo"

"Ok sawa"
       Tresha alikabidhiwa kikaratasi kidogo kilichokuwa na namba ya simu kisha yule mwanaume aliondoka zake na baada ya dakika kadhaa Stephan alirudi akiwa na glass mbili za juice, alimpatia Tresha moja na kuanza kunywa huku story zinaendelea.

"Unajua Tresha unatakiwa uwe na simu sasa ili hata ukiwa na shida alafu mimi nipo kazini basi unanipigia kwahiyo tukitoka hapa tutapitia duka la simu uchague simu unayoitaka"

"Oh asante sana jamani.!!"

Tresha alijikuta mwenye furaha siku hiyo maana alikuwa na ndoto siku moja amiliki simu, basi siku hiyo walipunga upepo na kucheza michezo mbali mbali ya ufukweni ilipotimu majira ya saa kumi na moja jioni walifunga safari kurudi wanapoishia ila walipitia kabisa kwenye duka la simu na kununua simu nzuri ambayo ingemfaa Tresha kwa matumizi na pia alisajili na line sasa mambo yakawa mazuri kwa Tresha.

                *************** 

Inatimu majira ya saa moja usiku baada ya chakula Stephan alijiandaa na kumuaga Tresha kuna sehemu anaenda lakini safari ilikuwa ni kwenda kuonana na Joyce na mpaka wakati huo hakufahamu kwanini Joyce amemuita.

Wakati yeye ameondoka Tresha alikumbuka kuchukua simu na kumpigia mwanaume aliempa namba, simu ilianza kuita na baada ya dakika kadhaa ilipokelewa.

"Hello"
    Sauti ya kiume ilisikika na kumfanya Tresha atabasamu.

"Hello ni mimi yule binti uliempa namba yako mchana kule baharini"
     Tresha alijitambulisha na yule mwanaume alimkumbuka.

"Ohoo dah nimekukumbuka ila nilifikiri hutanitafuta kumbe wewe ni mkweli na hii namba ni namba ya nani?"

"Namba yangu hii tayari nimepata simu"

"Ahaaa vizuri sasa unaonaje tukakutana sahizi kuna jambo nataka kuzungumza na wewe ni jambo la muhimu sana"

"Mh hapana siwezi kutoka sahizi kabda upange siku nyingine!"

"Sawa ila ni muhimu sana dadaangu au niambie wewe upo wapi nikufuate tunaongea machache alafu nitaondoka sitakaa sana"

Tresha mpaka wakati huo hakujua dhamira ya mwanaume huyo ni nini, basi alimuelekeza sehemu alipo na alihakikishiwa ndani ya dakika therasini gari itawasili hivyo alibaki akiwa na shauku ya kutaka kuona hiyo gari ikifika ataambiwa nini cha maana.

Sasa tutoke huko twende club ambapo tayari Stephan alikuwa amewasili na muda mchache baadae Joyce nae aliwasili ila Joyce asichokijua alikuwa anafuatiliwa nyuma na Ochu ili kujua anaenda wapi.

Alifika na kumkuta Stephan amefika muda mrefu na mpaka vinywaji alikuwa ameagiza.

"Samahani sana Stephan kwa kuchelewa ila kulikuwa na treffic jam lakini natumai hujachukia kipenzi"

"Usijali"

Wakati maongezi yanaendelea Ochu alifika na kutafuta meza kisha aliketi, aliagiza kinywaji na kuanza kunywa taratibu huku akiwatazama Joyce na Stephan.

"Inamaana yule ndiye Stephan mwenyewe au.!?"
    Ochu alijiuliza maswali yaliyokosa majibu lakini wakati anaendelea kuwatazama alimuona Joyce akipeleka mkono taratibu na kuushika mkono wa Stephan, kitendo kilichomuuma na kushindwa kuvumilia.

Aliinuka na kusogea mpaka walipo huku akiwa na hasira sana, Joyce alipomuona Ochu alishtuka sana na kumuuliza alifuata nini hapo.

"Kwahiyo huyu ndiye Stephan ambae anakuzuza akili wewe.!?"

"Hebu Ochu kuwa na adabu kuingilia mazungumzo ya watu kwani Stephan wewe anakuhusu nini kwanza nitokee hapa sikujui wala hunijui"
    Joyce ilibidi aje juu maana aliona atapeperushiwa ndege wake lakini Stephan baada ya ukimywa wa muda nae ilibidi aingilie kati.

"Hey bro kwani shida yako ni nini mbona umekuja ghafla na kuanza kusumbua watu.!?"

"Tena na wewe usiongee kabisa mshenzi mkubwa wewe"

Ochu alikuwa tayari amepanic, alitazama mezani aliona kuna chupa tatu za bia hivyo alichukua chupa moja iliyokuwa tupu na bila kuchelewa alimpiga nayo Stephan kichwani, hali iliyopekea maumivu makali sana kwa Stephan na damu zilianza kumtoka kwa wingi sana....ITAENDELEA....

- Unafikiri nini kitafuata hapo maana kila sehemu mambo ni moto..nakusihi tukutane sehemu ya tisa kujua nini kitafuaa kwenye mkasa huu wa sisimua....