Jina....TABASAMU LA UCHUNGU
Mtunzi.......... Official Dully
Mkasa....wa...kusisismua
Sehemu Ya {07}
ILIPOISHIA..
Siku hiyo shangazi aliipata fresha, basi taratibu alijikokota mpaka kwake, alipatiwa humuduma ya kwanza na mume wake siku hiyo ilipita akiwa na majonzi lakini siku iliyofuata asubuhi na mapema aliamshwa na kelele, alitoka nnje haraka kuangalia nini kimejiri ila alikutana na umati wa wanawake wenzake wakiwa na madalali na hiyo ilimaanisha nyumba yake inatakiwa kuuzwa.....ENDELEA..
Shangazi siku hiyo alishindwa kuelewa aanzie wapi aishie wapi maana kwa nyuso za wana kikundi wenzake waliofika kwake zilionesha dhahiri hawakuja kiutani na hawakuhitani kusikia chochote kutoka kwake zaidi ya kuona nyumba ikipigwa mnada..
"Jamani sikieni niwaambie wana kikundi wenzangu mimi pesa yenu nitawapa sio kama sihitaji kulipa lakini kuna mambo jana yamenitokea na kama mnavyoona hali yangu, nioneeni huruma mimi nitawalipa jamani.!!"
Shangazi aliongea kwa sauti ya upole huku akiweka sura ya huruma lakini hakuna hata aliemuonea huruma.
"Eti tukuonee huruma, hivi hukumbuki kilichomtokea mama Hamisi, vyombo vyake vya ndani vyote vimeuzwa, achilia mbali mama Hamisi uliona kilichonitokea mimi nimefirisiwa biashara mpaka mwanangu Chiku alibaki nyumbani nilikosa pesa ya kumlipia ada ya shule alafu wewe tu kizeme unataka uonewe huruma"
"Lakini mama chiku nisikilize, mimi nitalipa hiyo pesa nipeni siku moja tu naahidi pesa nitawalipa.!!"
Shangazi alijikuta mpaka akipiga magoti na siku hiyo ujanja hakuwa nao kabisa.
"Hebu usituchanganye hapa yaani tukuonee huruma wakati keshokutwa tu hapo harusi alafu mpaka muda huu hatujashona sare, hebu wana kikundi ingieni ndani toeni kila kitu kipigwe bei na nyumba iwekwe mnadani itauzwa kwa bei ya hasara tu"
Amri ilitolewa na mama Chiku ambae ndiye kiongozi wa kikundi, basi wana kikundi walifanya kazi yao ila upande wa shangazi alibaki akilia tu ajui afanye nini na mume wake alikuwa hayupo ameenda kazini.
"Kwahiyo mama chiku leo mmeamua kunifanyia unyama huu hivi hamuoni kama nina watoto wadogo, je watoto wangu wataishi kwenye mazingira gani jamani.!?"
"Hebu usinisemeshe mimi, kipindi nataifishwa wewe ndiye ulikuwa kimbelembele na mibao ulinipiga alafu leo hii eti unasema watoto wako wataishi vipi kwani mimi watoto wangu waliishi vipi..!?"
"Lakini mama chiku watoto wangu ni wadogo sana...!!"
"Bwana weee wataishi hivyo hivyo mbona kuku hana nyumba lakini watoto wake wanaishi kwahiyo na watoto wako wataishi hivyo hivyo"
Shangazi alibaki kimya tu maana kila alichokuwa akimwambia mama chiku alikuwa hamuelewi hivyo alibaki kutazama vitu vyake vya thamani vikitolewa nnje na muda si punde lilifika gari kubwa ambalo ndilo lilitakiwa kuchukua vyombo hivyo na kuvipeleka kwa wateja.
Shangazi akiwa haamini kinachoendelea alifika rafiki yake wa karibu na kumshika bega.
"Nilikwambia mimi shoga yangu lakini ukajifanya eti ooh bora pesa ziende kuliko kulala kituo cha polisi haya ona sasa ujalala kituo cha polisi ila unakwenda kulala nnje"
"Lakini unanishauri, unataka kunisaidia au unanisema maana naona kama unanisema.!?"
"Amna sina cha kukusaidia na kama ilivyo desturi ya kikundi chetu mtu ukimsaidia na wewe unataifishwa kwahiyo mimi msaada wangu ni ushauri tu ukihitaji ila hayo mengine sitaki yanikute mwenzagu"
Vitu vilitolewa vyote na kupakiwa kwenye gari, karatasi za umiliki wa nyumba zote zilikabidhiwa kwa wana kikundi na muda huo huo nyumba iliwekwa mnadani hakukuwa na muda wa kuchelewa, yote hayo yanaendelea shangazi alikuwa akitazama na kuumia.
Ok tuachane na huko tuje kwa Joyce, siku hiyo Joyce alichelewa kuamka na alikuja kuamka saa tatu asubuhi baada ya mrango wa chumba chake kugongwa, alijiinua kwa uvivu kutoka kitandani na kwenda kufungua lakini alikutana uso kwa uso na Stellah.
"Haya umefuata nini chumbani kwangu we kijuso si nilikukataza kuja hapa.!?"
"Mimi sijaja kubishana na wewe nimekuja hapa kwasababu mama amenituma nije kukuamsha kwahiyo kama unaona unahamu ya kutukana basi kamtukane mama alienituma na sio mimi"
"Ok haya nitokee mbele yangu nahisi kinyaa"
Stellah bila kubisha wala kupinga aliondoka zake na kumuacha Joyce akijiandaa, baada ya dakika kadhaa Joyce alitoka na kujumika kupata kifungua kinywa na familia yake lakini muda wote alikuwa akimtazama Stellah kwa hasira maana alikuwa ni mtu anaemfuatilia sana kwenye mambo yake.
"Wewe Joyce mbona unamuangalia mdogo wako kama hivyo au tayari mmekorofishana maana hua hamchelewi nyie.!!"
"Hapana mama kawaida lakini......"
Joyce kabla hajamaliza kuongea alichokusudia walisikia honi ya gari ikilia nnje na kumfanya kila mmoja ashangae ila kwa upande mwingine walifikiri huenda baba wa familia ndiye amewasili.
Stellah haraka aliacha kifungua kinywa na kutoka mpaka getini, alifungua geti ila alikutana na gari tofauti na sio gari la baba yake kama ambavyo alifikiria.
"Huyu ni nani.!?"
Stellah alijiuliza na wakati huo mrango wa ile gari ulifunguliwa kisha alishuka Ochu, mwanume ambae alilala na Joyce usiku wa juzi.
"Hello mrembo.?"
Ochu alimsalimia Stellah na bila ajizi Stellah aliitika salamu yake huku bado akiwa na maswali kibao kuhusu mwanaume huyo.
"Samahani najua sijakosea nyumba binti, bila shaka hapa mdipo anaishi Joyce.?"
"Yah ndio hapa kwahiyo nikakuitie au vipi?"
"Yah mwite mwambie kuna mtu anakwitaa anahitaji kuzungumza na wewe akikuuliza jinsia gani usimwambie maana ukimwambia anaweza asije"
"Ok sawa"
Stellah alirudi ndani haraka lakini kwa tabia ya dada yake Joyce alishajua kwamba yule ni mwanaume wa dada yake na sio vingine.
Alifika mpaka sebuleni lakini bahati hakumkuta mama yake mezani ila alimkuta Joyce ameketi mwenyewe akimalizia kupata kifungua kinywa, basi alimfuata na kumwambia kama ambavyo alitumwa.
"Weee nani huyo ananiita, wa kike au wa kiume.!?"
"Ah wewe nenda kwani si ulinimbia nisiingilie mambo yako kwahiyo wewe nenda utajua huko huko nnje"
Joyce mapigo ya moyo yalianza kumuenda kasi, lakini hakutaka kupoteza muda aliinuka na kutoka mpaka nnje, ndipo alipomuona Ochu amesimama akiwa mwingi wa tabasamu.
"Ochu.!!!"
"Yah ni mimi mpenzi lakini mbona juzi uliniambia utanitafuta alafu ukawa kimya au kuna shida mpenzi wangu.!?"
"We hebu usinitanie umepajuaje hapa.!?"
Joyce alimshika mkono Ochu na kumsogeza pembeni ili waongee vizuri maana ilikuwa ni ghafla sana kufika hapo na tangu aanze kutembea na wanaume mbali mbali hakuna hata mmoja aliepajua kwao ila kwa Ochu alibaki na maswali mengi sana je amepajuaje.!.
*****************
Upande wa pili kwa Stephan siku hiyo aliamka asubuhi na mapema, aliandaa kifungua kinywa kisha aliweka mezani na kundoka zake, hakutaka kumuamsha Tresha akiwa na imani atamsumbua hivyo aliondoka lakini alimuachia maagizo kwenye kikaratasi na kuweka mezani.
Mpaka inatimu saa tano asubuhi ndipo Tresha anakuja kuamka lakini alitabasamu baada ya kujikuta juu ya kitanda kikubwa cha kifahari.
Aliinuka na kuvaa gauni lake lile lile jekundu kisha alielekea sebuleni ambapo alikuta meza imesheheni vyakula vilivyopikwa vyema na kufunikwa.
"Inamaana Stephan ndiye amepika hivi au amenunua.!?"
Tresha alijiongelesha huku akifunua kila chombo na kuvuta harufu safi ya vyakula hivyo, alichukua kijiko na kuingiza kwenye bakuli ya supu ila alipotaka kupelekea kinywani alikumbuka kuwa bado hajasafisha kinywa.
Aliacha na kufunika vizuri ila alipotazama pembeni alikuta karatasi na karatasi ile alipoisoma ilikuwa na maelekezo ni nini anatakiwa kufanya pindi akiamka, hii kwake haikuwa ajabu kwasababu alikuwa mtu wa kufanya kazi basi aliona afanyie kazi vitu alivyoambiwa afanye kabla ya kula.
Siku hiyo ilikuwa ni tulivu sana hata kwa upande wa Stephan alipofika kazini kwake aliwaona wafanyakazi wake wakiwa na nyuso za furaha sana na haikuwa kawaida kuwaona wafanyakazi wake wakiwa na furaha kiasi hicho.
"Jamani kuna nini mbona mnanitazama sana alafu mnatabasamu au nimekosea kuvaa leo.!?"
Stephan aliuliza huku akijitazama vizuri lakini ghafla alisikia makofi yakianza kupigwa huku nyimbo ya birthday ikichukua nafasi yake na ndipo alikumbuka siku hiyo ilikuwa siku yake ya kuzaliwa.
Hakukaa sawa mrango wa ofisi ya Daniel ulifunguliwa na walitoka wazazi wake huku wakiongozwa na Daniel pamoja na Sasha ambae alikuwa amebeba keki kubwa ya gharama.
"Wow kumbe leo ni siku yangu ya kuzaliwa daah alafu nilikuwa sijui kabisa na hata mawazo hayo sikuwa nayo.!!"
Stephan alijisemea mwenyewe na nafsi yake lakini macho yake yalitua kwenye mwili wa binti mmoja mrembo mwenye ngozi ya chocolate na hakuwa mwingine ila ni Sasha.
"Inamaana Sasha pia anajua siku yangu ya kuzaliwa au atakuwa ni Daniel amemwambia.!?"
Siku hiyo ilikuwa ni siku muhimu sana kwa Stephan pia ilikuwa ni siku ya furaha kwa kila mmoja lakini si huko tu hata Tresha alipokuwa anasafisha chumbani kwa Stephan aliona sanduku moja ikiwa wazi, aliisogelea ili kuifunga na ndipo aliona card ya Stephan ya kuzaliwa.
Aliichukua na kuitazama vizuri ndipo alistaajabu kuona siku hiyo ilikuwa siku ya Stephan ya kuzaliwa.
"Inamaana leo ni siku yake ya kuzaliwa, mbona sasa hakusema au atakuwa amesahau, sasa kama amesahau basi nitamfanyia surprise"
Tresha aliirudisha ile card na kuendelea kufanya usafi nyumba nzima.
Alikuwa ni mwanamke aliekuwa haraka sana kwenye kazi, huenda kutokana na maisha ya utumwa aliyosihi au laa lakini alipomaliza alifunga safari kwenda kwenye supermarket na huko alinunua kila kitu kilichofaa kutengenezwa keki.
Tuache huko turudi tena kwa Stephan ambapo huku party ndio ilikuwa inaishia ishia, watu walikula keki na kutoa zawadi mbali mbali kwa Stephan ila wakati zawadi zinaendelea kutolewa baba wa Stephan alimvuta kijana wake kando ili kuzungumza.
"Unajua mwanangu nimekuvuta hapa kwa jambo moja na jambo hilo nikisubiri tuongelee nyumbani tunaweza kuchelewa kwahiyo nimeona nikwite hapa tuzungumze kuhusu wewe kuoa"
Baba Stephan alizungumza huku akitabasamu ila Stephan alishtuka kidogo.
"Baba mbona ghafla sana.!?"
"Sio ghafla mwanangu, wewe hapo ulipo una miaka 24 huoni kama umri unaenda na kuna binti tumemuona anafaa pia tumemuuliza nae amesema yupo tayari na anakupenda sana sasa huu ni muda wako mwanangu wa kutoka kwenye ubachela"
"Baba mbona kama unanivuruga na mwanamke mwenyewe ni nani.!?"
"Si yule binti Sasha"
"Sashaaa.!!?"
Stephan aliuliza kwa mshangao maana hakutarajia kama mwanamke mwenyewe angekuwa Sasha na pia hakuwahi kufiria itafika siku awe nae kwenye mahusiano.
"Hapana baba siwezi kumuoa Sasha ila kuna mwanamke nampenda"
"Mwanamke yupi.!!?"
Baba Stephan alishtuka kusikia kijana wake kuna mwanamke anampenda hivyo ilibidi amkazie macho na kuweka umakini ili kujua ni mwanamke gani ambae kijana wake ametoka kumpenda.
****************
Joyce upande wake bado alikuwa na maswali mengi ya kujiuliza kuhusu Ochu kikubwa alihitaji kujua amefikaje hapo lakini upande mwingine alikuwa hampendi hata kidogo alichokitaka alikipata lakini Ochu bado alimganda.
"Jamani kwani mimi kupajua kwenu kuna tatizo gani kipenzi je kama mataka kuja kuleta barua utajuaje?"
"Achana na barua ila nataka kujua umepajuaje hapa.!?"
"Ah ukweli nilikuwa nakufuatilia usiku ule, najua namba yangu umeitupa lakini tambua mimi nakupenda na nahitaji uwe mke wangu wa milele"
Ochu hakutaka kulaza damu, alichokihisi moyoni mwake ilibidi akiseme.
"Sikia nikwambie bhana ukweli ni kwamba mimi sikupendi na siku ile ilitokea kama ajali, bahati mbaya na usichokijua kuna mwanaume nampenda sana na miezi ijayo tunaweza kufunga ndoa anaitwa Stephan kwahiyo naomba usijichoshe kunipenda pia usije tena hapa"
Joyce alimaliza kuzungumza na kurudi ndani huku nyuma akimuacha Ochu kwenye majonzi makubwa sana ila akilini mwa Ochu alichowaza kwa wakati huo ni kumfahamu huyo Stephan ambae ameuteka moyo ya mwanamke anaempenda.
Ebwana eeeh mambo ni moto sana sasa tuwapishe wenye mapenzi yao tuhamie kwa shangazi ambae alikuwa na wakati mgumu sana siku hiyo, nyumba yake tayari ilikuwa kwenye mnada vitu vyake viliuzwa alibaki yeye kama yeye amaketi chini akijililia.
Wakati huo wana kikundi walikuwa tayari wameondoka na shangazi alikuwa nnje kabisa ya nyumba ila akiwa hapo mwingi wa majonzi alifika mtu na kusimama mbele yake, alipoinua macho kumtazama hakuwa mwingine ila alikuwa ni mume wake.
"Inuka mke wangu najua kila kitu kilichotokea na siwezi kukulaumu kwasababu mimi ndie nimekushawishi kuingia kwenye mambo haya ya vikundi"
Mume alimpatia mke wake mkono na kumuinua.
"Mume wangu gari yako iko wapi.!?"
"Ah ile ni gari ya kampuni na nimepokonywa baada ya huu uvumi wa mali zetu kuuzwa basi bosi aliona huenda gari yake ikauzwa hivyo ameichukua na kwa sasa hata kazi sina"
"Kwanini mume wangu sasa sisi tutaishi vipi na watoto wetu.!?"
"Ah usijali kuhusu watoto kwakuwa ada yako bado aijaisha wataendelea kukaa huko mpaka shule ikifungwa basi tutakuwa tayari tumepata sehemu ya kuishi ila naomba unifuate"
"Tunaenda wapi mume wangu.!?"
"Ah kuna mtoto wa rafiki yangu ambae nimemueleza shida yangu amesema niende kwake atanipa msaada kwahiyo naomba twende huenda tukapata msaada huko maana huyo mtoto mambo yake mazuri sana"
Maneno ya mume yalimfanya shangazi kidogo huzuni imuishe hivyo walifunga safari kuelea huko wakiwa na imani watapata msaada.
Muda taratibu ulianza kusogea huku upande wa Tresha keki ikizidi kutengenezwa maana alikuwa fundi sana kwenye mambo ya kutengeneza keki na siku hiyo alipanga kumfanyia surprise Stephan.
"Yaani hii keki naimani Stephan ataifurahia kabisa"
Tresha alikuwa akiongea mwenyewe wakati huo keki ilikuwa kwenye hatua za mwisho kukamilika.
Baada ya kuikamilisha aliiweka sibuleni na kupamba vizuri lakini wakati huo huo alisikia geti likigongwa nnje, mapigo ya moyo yalimuenda kasi sana, alitoka haraka akiwa na aimani huenda atakuwa Stephan.
Alilifikia geti na bila kuchelewa alifungua mrango huku akiwa na uso uliopambwa na tabasamu lakini tabasamu lake liliyeyuka ghafla baada ya kumuona shangazi yake pamoja na mjomba yake, hata shangazi nae alishangaa kumuona Tresha hapo na kila mmoja alibaki kwenye maswali mengi akijiuliza kuhusu mwenzake....ITAENDELEA...
- Mambo yamepamba moto sasa, huku shangazi uso kwa uso na Tresha kule kwa Joyce Ochu anahitaji kumuona mwanaune alieuteka moyo wa Joyce na huku kwa Stephan baba yake anataka kujua mtoto wake anampenda mwanamke gani....patamu hapooo..!!
