Jina....TABASAMU LA UCHUNGU
Mtunzi...... Official Dully
Mkasa....wa...kusisismua

            Sehemu Ya {06}

ILIPOISHIA..

Baada ya sauti hiyo ya muhudumu wa kike kusikika Stephan alishtuka maana alikuwa akiifahamu, hakutaka kuchelewa aliinuka alipokaa ili kusogea aneo la tukio, kweli alipofika alikuta wanaume watatu amemshika Tresha kwa nguvu huku wakimvuta kuelekea nae vilipo vyumba vya kulala wakamalizane nae....ENDELEA...

  Ilikuwa ni vuta nikuvite kwa wanaume wale lakini Tresha hakukubali kwenda maana alijua kama atakubali huenda ukawa ndio mwisho wa maisha yake au kuzoa magonjwa ambayo yatamletea shida maishani mwake.

"Hey tafadhali naomba mumuache huyo binti kama ataki kwenda muacheni mimi nitamchukua kwenda kulala nae"
     Stephan alizungumza kwa kupaza sauti na kupelekea wale wanaume kugeuka ili kumjua nani alieuzungumza kauli hiyo.

Hata Tresha alipogeuka na kumuona Stephan alijikuta akipata amani ya moyo maana aliona tayari mkombozi amefika na hatoweza kufanywa chochote.

Baada ya kauli ya Stephan kusikika bosi wa club hiyo alipiga hatua taratibu mpaka alipo Stephan na kusimama mbele yake kisha alimtazama juu mpaka chini na kumuuliza swali ambalo lilimfanya Stephan atabasamu.

"Hivi kijana unafikiri utatoa kiasi gani ambacho kitanishawishi nimtoe huyu binti kwenye mikono ya hawa wanaume na kukupa wewe kwasababu wamenipa pesa nyingi sana ili kumtumia huyu binti"

"Aijalishi wamekupa kiasi gani ila mimi nitakupa mara mbili yake na nitamnunua kabisa huyu binti"
     Stephan aliongea kwa kujiamini huku akimtazama Tresha ambae bado alikuwa ameshikwa mikono na wale wanaume wakisubiri maamuzi ya mmiliki wa club kama waende nae au wamuache aondoke na Stephan.

"Hongera sana kijana unaonekana una kiburi cha pesa ok sawa nipatie milion tatu nikuachie uende nae"

"Ok aina shida"
      Stephan bila kuchelewa aliingiza mkono mfukoni na kutoa wallet iliyosheheni pesa, alifungua na kutoa milion tatu kisha alimpatia yule mmiliki wa club.

Baada ya kukabidhi pesa amri ilitolewa Tresha aachiwe aende na Stephan na wale wanaume hawakuwa na ajizi walimuacha Tresha ambae kwa mwendo wa kukimbia alimfuata Stepha na kumkumbatia huku machozi yakimshuka.

"Nisamehe sana kakaangu pia naomba msaada wako sihitahi tena kubaki hapa.!!"

"Ulitaka msaada wangu wewe, si uliniona mimi sifai sijui nitaenda kukufanyia mambo mabaya sasa nafikiri umeona dunia ilivyo kwahiyo mimi nimekununua na maisha yako yote utakuwa chini yangu"
       Stephan alimshika mkono Tresha na kutoka nae nnje ila kabla hajafika kwenye gari lake alisikia akiitwa na aliekuwa anamwita alikuwa ni Joyce.

"Oh Joyce samahani sana yaani nilisahau kabisa kama nilikuwa na wewe ila kama unavyoona dharura imetokea kwahiyo naomba tuonane siku nyingine"

"Ok sawa aina shida kipenzi"
         Joyce alikubali kishingo upande na siku hiyo mpango wake ulikuwa tayari umefeli.

"Lakini aina shida Stephan kama leo nimekukosa basi nitakupata siku nyingine lazima unionje joto la mwili wako iwe isiwe"
     Joyce hakuwa na muda wa kupoteza, alienda mahali lilipo gari lake alipanda na kuondoka zake lakini mtego wake ulikuwa umefeli siku hiyo.

Safri kati ya Stephan na Tresha ilianza ila wakiwa njiani Stephan alipeleka gari kando ya barabara na kusimama kisha alifungua mrango upande alipo Tresha na kumtazama mpaka Tresha mwenyewe alishangaa.

"Samahani mbona unanitazama kiasi hicho.!?"

"Nimefungua mrango tayari kama unahitaji kushuka uende kwa shangazi yako basi ni ruhusa kwenda"
      Stephan alizungumza lakini alifahamu Tresha asingeweza kwenda, alichokuwa akikiwaza kilikuwa sahihi Tresha hakuweza kushuka ila alifunga mrango kumaanisha waendelee na safari pia alihitaji msaada wa Stephan.

"Sasa kama umefunga mrango inamaanisha umekubali kwenda na mimi kwahiyo sasa nikwambie upo chini yangu"

Stephan hakuwa na maneno mengi aliwasha gari na safari ilianza kuelekea kwake ila akiwa njiani simu yake ilianza kuita na aliekuwa anapiga hakuwa mwingine ila alikuwa ni Joyce.
     Hakutaka kupuuzia simu hiyo, aliipokea na kumsikiliza alitaka kuzungumza nini cha maana.

"Hello Joyce.?"

"Stephan tayari umefika.?"

"Hapana lakini ndio nakaribia kwahiyo kama dakika kumi nitakuwa nimefika"

"Ahaaa sawa lakini nilikuwa nataka kujua yule binti uliemchukua pale club ni nani yako mbona kama mnajuana na ulichosema kuwa unakwenda kulala nae ni kweli au ulikuwa unatania.?"

"Samahani tutaongea vizuri baadae"
       Staphan alikata simu na kujikuta akitabasamu maana alijua nini kilikuwa kinamsumbua Joyce.

Hata upande wa Joyce baada ya simu kukatwa alijikuta mapigo ya moyo yakimuenda mbio sana na haikuwa kawaida mapigo ya moyo kumuenda mbio mbele ya mwanaume.

"Dada nakuona hapo unawaza mbinu mpya kumnasa mwanaume yaani wewe mh sikuwezi.!!"

Wakati Joyce anawaza yake kuhusu Stephan aliingia mdogo wake Stellah huku akiwa na counter book mkononi, alijongea mpaka karibu yake na kuketi kitandani ila Joyce alimkata jicho kali Stellah lakini Stellah hakujali.

"Sasa kwani uwongo dada, mimi najua ukiwa kimya tu ujue unawaza kuhusu mwanaume lakini usijali mimi sijaja kukusema nimekuja unielekeze kuhusu hizi hesabu hapa maana wewe umesoma sana na hesabu unazielewa dadaangu"
     Stellah alizungumza huku akimuwekea Joyce counter book mapajani mwake lakini Joyce alilichukua na kulitupa chini.

"Naomba uende sitaki kukuona chumbani kwangu na sio mara moja wala mbili nimekwambia sihitaji kukuona ila kama hunisikii nitakubutua upeleke kesi kwa mama yako"

"Mh dada nae hutaniwi haya natoka ila ukweli niseme wewe ukikaa unawaza wanaume"
      Stellah aliinuka na kuokota counter book lake huku akizungumza maneno ambayo mpaka mama yake aliyasikia maana alikuwa amefika na kusimama mrangoni baada ya kusikia mzozo.

"Stellah maneno gani hayo unayaongea kwa dada yako, si uliambiwa umuheshimu, umekuwa sasa hayo maziwa kifuani yanakuzuzua eeh.!?"

"Ma...mama...hapana...ni"
       Stellah hakuwa na neno la kujitetea alibaki kuuma maneno lakini mwisho mama yake alimsogelea na kumshika sikio huku akitoka nae nnje.

"Yaani mitoto mingine sijui ipoje, ukiibutua haichelewi kulia sasa subiri muache anizoee dawa yake inacheka"
     Joyce kwa hasira aliinuka na kwenda kufunga mrango ili asiingie mtu yeyote kumletea kero wakati akiwa kwenye mipango yake.

                 ****************

Gari ilifika nnje ya jumba kubwa la kifahari na jumba hilo lilikuwa geni machoni mwa Tresha, ilibidi amgeukie Stephan na kumuuliza hapo ni wapi maana hakuwahi kufika kabla.

"Hapana ni kwangu"
      Jibu la Stephan lilimfanya Tresha atoe kichwa nnje na kulitazama jumba hilo lakini hakupata jibu sahihi kwa alichokiona.

"Hapa ni kwako mbona kama sio pale uliponipeleka jana, hii nyumba ni tofauti kabisa na ile.!?"

"Ndio nyumba tofauti lakini hapa ndio kwangu ninapopenda kuishi kule nilipokupeleka jana hua naenda kukaa mara moja moja sana"

"Ahaaa kwahiyo una nyumba mbili.!?"

"Hapana nina nyumba nne ila huko kwingine nimepangisha lakini sioni sababu ya kuongelea nyumba kwanza tuingie ndani najua umechoka sana"
       Stepahan alikanyaga mafuta na taratibu alianza kulisogelea geti ila kilichomuacha mdomo wazi Tresha ni baada ya kuona geti la nyumba hiyo linafunguka lenyewe.

Gari iliingia mpaka ndani na kupakiwa sehemu husika kisha walishuka lakini Stephan alipomtazama Tresha alimuona mwenye aibu sana na aibu ya tresha ilitokana na mavazi aliyovaa.

Stephan hakutaka kumfuatilia sana aliongoza ndani na nyuma Tresha alifuata, walipofika sebuleni ndipo Tresha alibaki mdomo wazi zaidi maana sebule ilikuwa kubwa na ilipendeza kwa vito vingi vya tahamni.

 "Tresha wewe shangaa shangaa alafu ukimaliza utaingia kwenye chumba hicho na utakuwa unakitumia muda wote unaokuwa hapa pia kuna nguo ambazo nimekuandalia muda sana sasa itavaa hizo kama huzipendi utaniambia"

Stephan hakutaka maneno mengi aliingia chumbani kwake huku nyuma akimuacha Tresha akishangaa lakini mwisho nae aliingia chumbani kwake ila huko ndipo kulimuacha na mshangao zaidi maana chumba kilikuwa kikubwa na kila kilichokuwa humo kilivutia sana.

"Wowo kumbe kuna watu wanaishi sehemu nzuri hivi, kitanda kikubwa, kabati zuri yaani kila kitu kinavutia mpaka dressing table sio kama ile ya shangazi ndogo.!!"

Wakati Tresha anashangazwa na nyumba ya Stephan tuje kwa shangazi yake mama mwenye roho mbaya kupita kiasi na siku hiyo alikua mwenye hasira sana baada ya kupata taarifa Tresha amechukuliwa.

"Hebu msinivuruge kichwa kaka zangu mnajua nimetoka kwangu usiku huu nimemuacha mume wangu nimekuja kuangalia maendeleo ya Tresha alafu mnaniambia amechukuliwa.!!"

"Sasa dada si pesa nimekupa unachotaka wewe ni nini wakati hizo pesa tumezipata baada ya kumuuza mtoto wako"

"Ahaaa sasa naona mnanipanda kichwani.!!"
     Shangazi alikuwa mtata haswaa na mwili wake mnene aliokuwa nao ndio ulimfanya ajiamini zaidi bila kujua alikuwa anabishana na mwanaume ambae anaweza kumfanya chochote.

"Sio kukupanda kichwani dadaangu lakini....."
     Mmiliki wa club hiyo kabla hajajitetea shangazi alimkunja shati na kuanza kumpa vitisho huku akimtikisa.

"Sikia nikwambie we kaka mimi nakupa siku mbili binti yangu arudi kufanya kazi hapa, sikumleta hapa mumuuze kama mchele ila nimemleta auze mwili wake na kila usiku nije kuchukua mapato sasa kama mmemuuza basi namtaka la sivyo mtajua mimi nani"

Shangazi alitoa vitisho na pesa alizopatiwa milion mbili alizichukua na kuziweka kwenye mkoba wake ili kwenda kulipa pesa aliyopoteza ya kikundi.

"Oya mwanangu umeona bwenge lile yaani linaweka pesa kizembe sasa huyu sio wa kumuacha yaani tunakwapua mkoba wenyewe kesho tunaamka wanene"

"Aina noma mwanangu kesho kwa mama Kimbo tunakunywa supu ya nguvu"

Yaalikuwa ni maongezi ya vijana wawili wa kihuni waliokuwa kwenye club hiyo kama wateja na walikuwa wakimuongelea shangazi baada ya kumuona akiweka pesa kwenye mkoba.

Shangazi bila kujua amepangiwa kuibiwa basi taratibu alianza safari kuelekea kituoni na wale wahuni pia hawakutaka kulaza damu waliinuka na kuanza kumfutilia nyuma ili kufanya yao.

                *****************

Stephan kwakuwa ndie alikuwa mwenye nyumba hiyo na kila kitu alikijua basi aliingia jikoni na kupika chakula kizuri kisha alikiweka mezani na kwenda mpaka kwenye mrango wa chumba cha Tresha kisha alianza kumgongea.

"Hey we Tresha njoo tupate dinner chakula bado chamoto"

"Nakuja we anza kula tu"

Tresha alijibu kwa sauti ya chini wakati huo alikuwa busy kuchambua nguo kabatini na kuzitupia kitandani akitafuta nguo nzuri ya kuvaa maana kila nguo kwake aliiona mbaya, sio mbaya kwa sababu rangi au muonekano hapana, zilikua nzuri kwa binti wa mjini anaejua kuvaa ila kwa Tresha ambae alizoea kuvaa makanga na vitenge kwake aliona hakuna ya kumfaa.

"Jamani sasa nitavaa nguo gani mimi nguo zote mbaya.!!"
      Tresha alijikuta akiboeka na mwisho aliamua kuketi kitandani huku sura ameikunja kwa hasira.

"Huyu kaka nae hata ajui kuchagua nguo yaani ndio manguo gani sasa haya ni ushamba tu.!!"

Tresha alikua mtu wa kulalamika ila kuna nguo moja aliipenda na nguo hiyo ilikuwa ni gauni ndefu nyekundu iliyokuwa aikimetameta hivyo aliona hiyo itamfaa, aliichukua na kuivaa kisha alitoka kwenda kujumuika na Stephan mezani.

Stephan hakuwa na ili wala lile, alikuwa busy akiendelea kula lakini Tresha alipofika na alipomtazama alijikuta akiangua kicheko kilichomfanya Tresha ashangae na kushindwa kuelewa Stephan anacheka kwanini.

"Unacheka nini.!?"

"Hivi hiyo nguo nani alikwambia ni nguo ya kuvaa nyumbani wakat hiyo ni spericial kwa mtoko.!"

"Bwana hebu niache hata hivyo manguo yote mabaya kwahiyo niliyoona ina unafuu ni hii sasa sitaki unicheke wala kuniongelea"

Tresha alisogea mpaka mezani na kuanza kupata chakula cha usiku lakini huku kwa shangazi alikuwa na kibarua kigumu maana kila alipokuwa anaenda alihisi kufuatiliwa, kwa hofu aliyokuwa nayo aliukumbatia mkoba wake vyema na kuongeza kasi ya kutembea.

Kila alipokuwa akipige hatua na mtu aliekuwa nyuma yake alizidi kuongeza hatua ila ghafla alitokea mwanaume mbele yake huku akiwa na kisu mkononi, alipogeuka kutazama nyuma na yule mtu wa nyuna nae alikuwa na kisu kuashiria lao moja.

"Sa..saa.samahani nyie ni kina nani na mnataka nini kwangu.!?"

"Haina kuuliza ila sisi tunataka hizo pesa la sivyo tunakumwaga utumbo hapa hapa upoteze maisha"
      Mwanaume aliekuwa mbele yake alizungumza na shangazi kwa hofu ya kumwangwa utumbo alitoa pesa zote na kuwapa.

"Lakini kaka zangu nipatieni hata pesa kidogo wanangu wakale"

"We bimkubwa usituletee shida zako hapo, hao watoto wako watakula mawe kwanza hizo hereni ulizovaa mbona kama za dhahabu haya tunaziomba.!!"

Shangazi siku hiyo alipatikana lakini kwenye hereni alikuwa mgumu kidogo kutoa maana alikuwa anazipenda na zilikuwa za thamani sana.
     Ubishi wake ulimponza, wahuni wale hawakuwa na masihara wala muda wa kupoteza, walimshika kwa nguvu na kuvuta zile hereni, kitendo kilichopelekea kumchana masikio na kumuacha kwenye maumivu huku damu zikimvunja.

Siku hiyo shangazi aliipata fresha, basi taratibu alijikokota mpaka kwake, alipatiwa humuduma ya kwanza na mume wake siku hiyo ilipita akiwa na majonzi lakini siku iliyofuata asubuhi na mapema aliamshwa na kelele, alitoka nnje haraka kuangalia nini kimejiri ila alikutana na umati wa wanawake wenzake wakiwa na madalali na hiyo ilimaanisha nyumba yake inatakiwa kuuzwa.....ITAENDELEA..

Unafikiri nini kitafuata hapo, je shangazi kitamkuta nini maana mambo yamegeuka kwake, tukutane sehemu ya 7 kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua.