Jina....TABASAMU LA UCHUNGU
Mtunzi......... Official Dully
Mkasa....wa...kusisismua

            Sehemu Ya {05}

ILIPOISHIA..

Tresha alinywea maana alijua hasira za shangazi yake, alifungua mdomo wake ili kujibu lakini aliambulia kofi zito lililomfanya abaki na alama shavuni, haikuishia hapo shangazi alivua kiatu chake ili kumuadhibu Tresha lakini ghafla alishangaa mkono wake umedakwa na aliefanya hivyo alitokea nyuma yake.....ENDELEA...

   Watu walikuwa tayari wamejaa aneo hilo na kila mmoja alikuwa akisubiri kuona ni tukio gani ambalo litatokea hapo lakini Stephan alifika na kuzuia ili Tresha asiendelee kuadhibiwa maana ilikuwa ni aibu kubwa sana kwa binti kama huyo kuadhibiwa tena mbele ya umati wa watu huku wengine wakiwa na simu zao wakichukua kile kinacho endelea.

"Samahani hivi umenishika mkono wewe kama nani au wewe ndiye mwanaume unaemzuzua binti yangu mpaka anashindwa kunisikiliza na kutoroka nyumbani.!?"
      Shangazi aligeuza hasira zake kwa Stephan ambae hakuwa na wasiwasi, alimtazama kwa dharau na kubaki akitabasamu.

"Ok sasa kama nikikwambia mwanaume mwenyewe ni mimi ambae nampotosha binti yako utachukua maamuzi gani.?"
     Stephan alizungumza kwa kujiamini lakini wakati huo Tresha alikuwa kimya hana neno lolote la kuzungumza.

"Yaani vijana wa siku hizi mnajikuta viburi eeh sasa subiri nipige simu polisi"

Shangazi haraka bila kuchelewa alitoa simu kwenye mkoba wake lakini Stephan hakutaka kusubiri upuuzi huo, alimshika mkono Tresha na kuingia nae dukani kununua nguo huku akimuacha sahangazi akihangaika kupiga simu polisi.

Walianza kufanya manunuzi yao kuchagua nguo zilizowafaa lakini wakati zoezi hilo linaendelea Tresha alimtazama Stephan kwa muda na kumuuliza swali ambalo lilimfanya Stephan atabasamu.

"Hivi we kaka huogopi polisi.!?"

"Kwanini niogope sasa kwani nina kosa gani, nimeua au nimeiba cha mtu, kama nimeua sawa nitaogopa lakini siwezi kuogopa chochote hebu fanya haraka pakia nguo tuende zetu"

"Ok sawa"
       Tresha hakuwa na budi kuanza kupakia nguo lakini kwa kiasi fulani alijikuta akimuamini Stephan licha ya kuto kumfahamu kwa jina pia kuto kumfahamu kiundani.

Taratibu walianza kutoka nnje Stephan akiwa mbele na Tresha akimfuata kwa nyuma ila walipotoka walikuta tayari polisi wamefika wakiongozwa na shangazi.

"Afande mwanaume mwenyewe ni yule aliemteka binti yangu nahitaji mumshike mumpeleke kituoni maana hawa watekaji wamekuwa wengi sana mjini hapa"
     Shangazi alikuwa na kiherehere lakini Stephan hakuwa na hofu, polisi walimsogelea na kumuomba anyooshe mikono wamvishe pingu lakini aligoma.

"Kwahiyo nyie maafande mnaijua kazi yenu vizuri au mnakurupuka tu maana naona kama vile hamjasoma sheria na kanuni za upolisi au bado wanafunzi nyie.!?"
       Stephan alitoa maneno hayo kwa kujiamini lakini wakati huo Tresha alikuwa nyuma yake amejificha kwa hofu.

"Kijana unaleta jeuri mbele ya sheria eeh.!?"

"Sheria ipi ambayo unaisemea wewe, ya kumkamata mtu bila ushahidi, hebu tazama binti mwenyewe ni huyu ambae inasemekana nimemteka lakini mbona hajatoroka au kupiga kelele kuomba mumsaidie.?"

"Lakini......"

"Afande hebu tulia hakuna cha lakini hapa, mtazameni huyu binti mwilini mwake alivyo na makovu alafu muulizeni haya makovu ameyapata vipi kisha ndipo mnikamate"
      Stephan alimsogeza Tresha mbele yake ili polisi wamuone vizuri na kweli walipomtazama walimuona na majeraha mengi.

Shangazi wakati huo sasa aliona kibao kinageukia upande wake, taratibu alianza kurudi nyuma ili kama likitokea la kutokea aanze kukimbia.

"Eti binti nataka kufahamu huyu mwanaume amekuteka au na vipi haya majeraha yamesababishwa na nini.!?"
    Afande mkuu ambae alikuwa ndiye kiongozi wa oparesion alimtupia swali Tresha huku akimkagua kila sehemu lakini Tresha macho yake yalibaki kumtazama shangazi yake ambae kijasho cha meno kilianza kumtoka.

"Afande hakuna lolote hivi vidonda na haya makovu nilikuwa naumwa na huyu kaka ndie kanisaidia kwahiyo hakuna kesi"
     Tresha aliona amtetee shangazi yake maana kama angesema alikuwa anamtesa basi alikuwa anaenda kulala kituoni.

"Afande nafikiri mmemsikia binti mwenyewe kwahiyo huyo mama aliewaita ndio mdeal nae sisi acha tuende maana tuna mambo mengi ya kufanya"
 
Stephan alimshika mkono Tresha na kuliendelea gari lao ambapo walipanda na kulitoa kwa kasi huku nyuma wakimuacha shangazi kwenye msala.

"Sasa mama umeamua kusumbua jeshi la polisi sio, haya sasa tuelewane ukalale kituoni au tukupe adhabu hapa hapa kisha uende nyumbani kwako?"

"A...af..afande hebu sikia nikwambie mimi sio kama nimewasumbua lakini ukweli yule kijana mtekaji na pale binti yangu kashindwa kuongea kwasababu yule kijana alikuwa na bastora lakini ni mtekaji yule.!!"

Shangazi masikini kigugumizi kilimshika huku kijasho chembamba kikimtoka lakini polisi hawakutaka kumsikiliza walimtaka apige magoti na kutoa pesa kidogo ya usumbufu.

"Sawa afande nitafanya hivyo"
       Shangazi bila ubishi alifungua mkoba wake na kuwapatia pesa zote mapolisi lakini moyoni mwake alijikuta akijenga kisasi kizito juu ya Tresha.

Polisi baada ya kuondoka aliinuka huku akipokea lawama kutoka kwa shoga yake maana pesa alizotoa kuwapa polisi hazikuwa pesa zake bali zilikuwa ni pesa za kikundi.

"Sasa shogaangu pesa zote tulizokuja kununulia kitambaa kwaajili ya shughuli umewapa mapolisi sasa kitambaa tutanunulia na nini.!?"

"Kwahiyo ulitaka mimi nikalale sentro kisa tu pesa za sare, acha ziende lakini bado nipo uraiani hayo mambo memgine tutamalizana"

"Ni sawa unachosema ila si uliona mama Ziada siku ile nyumba yake ilivyouzwa kisa alipoteza pesa za kikundi na sasa naona lile tukio linaenda kujirudia kwako"

Shangazi aliona kama rafikiyake anampigia kelele, alitafuta usafiri na kuondoka zake lakini moyoni alikuwa akimuwaza Tresha maana aibu aliyompa ilikuwa ni kubwa sana ambayo hakutegemea kama angeipata.

                   *************

Safari ya Tresha na Stephan ilikuwa ikisonga huku kila mmoja akiwa kimya lakini baada ya dakika kadhaa kupita Stephana alivunja ukimya na kuamua kumuongelesha Tresha ambae macho yake yalikuwa busy kutazama wanapoenda.

"Hey Tresha si nakuuliza wewe hizo nguo ulivyojaribisha zinakutosha mbona upo mbali sana kimawazo au ndio unamfikiria yule mama sijui mama yako?"

"Nguo zinanitosha lakini yule sio mama yangu yule ni shangazi yangu tu"
      Tresha alijibu lakini bado alionekana yupo mbali sana kimawazo na Stephan hakuelewa alikuwa anawaza nini

"Ahaaa sawa kwahiyo unachowaza hapo ni nini au unamuonea huruma shangazi yako ila nikutoe hofu hawezi kukamatwa ila atahojiwa tu alafu ataachiwa ondoa shaka"
      Stephan aliona amtoe hofu Tresha lakini Tresha ghafla aliomba gari isimamishwe.

"Nisimamishe kwanini wakati bado hatujafika.!?"
     Stephan alihoji huku taratibu akisimamisha gari kando ya barabara.

"Mh hapana siwezi kuambatana tena na wewe maana sikufahamu hata chembe lakini umekuwa mwema sana kwangu mpaka unanipa hofu.!!"

"Tresha unajua......"
       Stephan kabla hajamaliza kuongea Tresha alishuka akiwa na mfuko wake wa nguo tayari kuondoka lakini Stephan nae alishuka kisha amlishika mkono.

"Amna mimi nimekusaidia sio kwa nia mbaya lakini ni ubinaadamu tu umefanya nikusaidie kwahiyo ondoa shaka panda gari tuelekee nyumbani"

"Hapana siwezi, hata mimi nina nyumbani kwetu kwa shangazi yangu hivyo naomba niende"
      Tresha hakuwa na neno jingine la kuongea wala kumsikiliza Stephan, alivuka barabara na kuelekea upande wa pili ambapo kulikuwa na kituo cha gari, kwakua usafiri ulikuwa mwepesi kupatikana basi hakuchukua muda mrefu daladala ilifika, alipanda na kuondoka zake.

"Hivi huyu binti ananichukuliaje huyu kwani ananiona mimi muhuni au nitakwenda kumuuza.!?, ok sio mbaya kwakua ana kwao basi acha aende mimi nishampa msaada inatoaha"
    Stephan hakuwa na maneno mengi alirudi kwenye gari yake kwa unyonge na safari ilianza kurudi wake.

Muda ulikwenda na ilipotimu saa saba chana Tresha aliwasili nyumbani kwa shangazi yake, aligonga geti na muda haukupita geti lilifunguliwa na mjomba yake ambae alipomuona Tresha alitabasamu sana lakini Tresha alishtuka na hofu ilimtawala.

"Karibu mwanangu karibu ndani mbona unaogopa hebu ingia tafadhali sisi tumekusamehe"
      Mjomba alimkaribisha Tresha lakini Tresha alisita na mwisho aliingia ila kwa tahadhari kubwa sana maana kwa kilichotokea jana hakukisahau.

Aliingia mpaka sebuleni na kuketi kwenye sofa lakini alipomuulizia shangazi yake aliambiwa ametoka na hii ilimfanya aingiwe na hofu maana aliona lile tukio la jana linaenda kijirudia.

"Lakini usijali hatochelea kurudi acha mimi nikajipumzishe chumbani kwangu ila akirudi uje kuniamshe"
      Mjomba hakutaka maneno mengi alielekea chumbani kwake na hiyo ikawa nafuu kidogo kwa Tresha maana alishakuwa na hofu ya kubakwa tayari.

Dakika kadhaa zilisogea na ndipo lilisikika geti likigongwa, Tresha aliinuka na kwenda kufungua ndipo alikutana uso kwa uso na shangazi yake akiongozana na wanawake wenzake wapatao watatu.
       Kitendo cha shangazi kutupa macho mbele na kumuona Tresha alishtuka ila hakutaka kuonesha mshtuko wake wazi aliamua kupotezea na kuendelea kupiga soga na wenzake.

"Lakini shoga nawe umezidi kuogopa polisi yaani ningekuwa mimi nisingetoa hata senti kumi ona sasa umepewa siku tatu na zisipolipwa hizo pesa nyumba yako inauzwa na wana kikundi"

Maneno hayo wakati yanaendelea Tresha alikuwa akiyasikia na mwisho shangazi yake aliwaaga wenzake alipohakikisha wameenda alielekea ndani na hii ilimshangaza sana Tresha kwasababu shangazi hakusema chochote kumuhusu.

Hakuwa na budi nae kuelekea ndani ila alipofika sebuleni mrango ulifungwa kwa ndani na shangazi alimgeukia Tresha ambae alishaingiwa na hufu akijua lazima kipogo kitafuata..

                ***************

"Shangazi nisamehe sana sikuwa na nia ya kukuaibisha pale lakini nimerudi kuishi na wewe shangazi yangu maana mama kabla hajafa alisema nisije kukaa mbali na wewe"
     Tresha machozi ya hofu yalianza kumtoka lakini shangazi siku hiyo hakutaka kumpiga, alipiga simu shemu na baada ya dakika kama kumi walifika wanaume watatu wakiwa na gari nyeusi kuanzia matairi mpaka vioo.

Walikaribishwa ndani vizuri na baada ya kuingia shangazi alimtazama Tresha na kuwauliza wale wanaume.

"Mnamuoane huyu binti si anafaa kabisa.?"

"Anafaa kabisa yaani akifika tu ataanza na kazi ndogo ndogo za kuhudumia ila usiku wa saa sita ataanza kazi kubwa kubwa kwahiyo usijali huyu anafaa sana"
       Mwanaume mmoja alijibu na kumfanya shangazi atabasamu lakini Tresha bado alikuwa haelewi anafaa kwenye kazi gani.

Wakati anatafakari wale wanaume walimsogelea na kumshika kwa nguvu kisha kumfunga kamba na hapo Tresha ndipo alianza kuleta vurugu maana alijua huko anapokwenda huenda sio salama.

"Tresha unajua kama nyumba yangu nimepewa siku tatu kulipa pesa ya kikundi na nisipolipa itauzwa alafu uliesababisha yote haya ni wewe kwahiyo nikwambie tu utaenda kufanya kazi club ya kuuza mwili wako naamini ndani ya siku tatu pesa zitarudi"

"Shangaziiiiii....mhhhh.!!"
       Tresha alijaribu kupiga kelele lakini ndomo wake ulizibwa na kitambaa kisha walimbeba juu juu mpaka lilipo gari lao, walimpakia na kuondoka nae tayari kwenda kumfanyisha biashara ya ukahaba.

Siku hiyo ilipita kiivyo na siku iliyofuata asubuhi na mapema Stephan alikuwa wa kwanza kufika kazini mpaka wafanyakazi wake walishangaa, pia siku hiyo alipata ugeni na mgeni mwenyewe alikuwa ni Joyce.

Alimkaribisha ofisini kwake na kuongea mawili matatu lakini Joyce alijifanya yupo na haraka hivyo alimuomba Stephan namba ya simu na kumtaka usiku wa siku hiyo wakutane club akidai yupo na mambo muhimu amataka kuzungumza nae kuhusu kazi.

"Ok sawa nitafika"

"Sawa Stephan"
       Joyce aliondoka kwa furaha na tayari hatua ya kwanza alikuwa ameimaliza sasa alichokuwa akikisubiri ni kukutana club usiku wa siku hiyo ili wamalizane.

Kweli bhana ahadi hakuna alieivuja, wawili hao walikutana huku kila mmoja akipendeza kupita kiasi na mavazi ya Joyce siku hiyo yalimuacha Stephan mdomo wazi.

Walitafuta sehemu na kuketi, waliagiza vinywaji kwa bili ya Joyce na taratibu story zilianza huku Joyce akiwa na lengo moja tu kuhakikisha analala na Stephan usiku huo.

"Hey we binti mgeni njoo hapa, umeanza kazi leo nataka nilale na wewe leo hii hii"

Wakati maongezi ya Stephan na Joyce yanaendelea walisikia kauli hiyo kutoka kwa mlevi mmoja lakini walipogeuka kumtazama alikuwa amekaa sehemu ya kiza hivyo walishindwa kumuona vizuri na waliendelea kuongea zao.

"Unajua Stephan wewe ni mwanaume mzuri sana, unajua kuvaa na unamvutia kila mwanamke lakini sifahamu kwanini upo single.!?"
      Joyce alianza sasa swaga zake na Stephan alishajua nini Joyce anataka kusema au lengo lake kuu ni lipi.

"Nimeamua tu kuwa single"

"Ahaa ila ingependeza kama....."
     Joyce kabla hajamaliza kuongea walisikia muhudumu wa kike akipigwa kwenye club hiyo lakini walipotazama tukio hilo lilikuwa likiendelea sehemu iliyokuwa na mwanga hafifu.

"Mshenzi sana wewe yaani wanaume watatu wanataka kwenda kulala na wewe alafu unakataa, unafikiri shangazi yako amekuleta hapa ukae kama bosi, sasa utaenda kulala na hawa wanaume watatu"

"Lakini kakaangu mimi siwezi hizi kazi nioneeeni huruma"

Baada ya sauti hiyo ya muhudumu wa kike kusikika Stephan alishtuka maana alikuwa akiifahamu, hakutaka kuchelewa aliinuka alipokaa ili kusogea aneo la tukio, kweli alipofika alikuta wanaume watatu amemshika Tresha kwa nguvu huku wakimvuta kuelekea nae vilipo vyumba vya kulala wakamalizane nae....ITAENDELEA...

- Mungu wangu..!!! mambo ni moto mambo ni fire, mimi sijui nini kitafuata hapo lakini nakuomba tu tukutane kesho Mungu akijaalia uzima na afanya kujua yanayojiri kwenye mkasa huu wa kusisimua...