Jina....TABASAMU LA UCHUNGU
Mtunzi...... Official Dully
Mkasa....wa...kusisismua

            Sehemu Ya {04}

ILIPOISHIA..

Stephan taratibu aliendelea na safari yake lakini akiwa njiani simu yake iliingia message hivyo aliichukua na kuitazama lakini aligundua ni message za mtandao hivyo aliirudisha simu mahali ilipokuwa lakini alipoinua macho kutazama mbele ghafla alimuona mwanamke akikatiza mbele yake na mwanamke huo alikuwa akitembea kwa kuchechemea hivyo alijikuta akikanyaga mbreki kwa nguvu ili kukwepa kumgonga...ENDELEA..

   Kilikuwa ni kitendo cha ghafla sana ambacho kilimchanganya Stephan hivyo alibaki ameduwaa kumtazama yule binti lakini mwisho alimuona akianguka chini mbele ya gari lake na hii ilimfanya azidi kichanganyikiwa.

"Mungu wangu au huenda nimemgonga nini.!?"
      Stephan alijiongelesha mwenyewe huku akifungua mrango wake wa gari na  kushuka kwenda kumuona binti huyo, hakujua alikuwa ni Tresha.

Alifka mpaka alipo yule binti na kumtazama vizuri ndipo alishtuka kumuona Tresha, alimtikisa ili kumumasha lakini juhudi zake ziligongwa mwamba Tresha alikuwa tayari amepoteza fahamu hajitambui.
     Alitazama kushoto na kulia hakukuwa na mtu yeyote aliekuwa akimuangalia, alimchukua Tresha na kumpakia kwenye gari yake na safari ilianza kuelekea kwake, hakutaka kumpeleka hospital.

"Huyu binti nimemgonga mimi au huenda ni matatizo yake mwenyewe, mh hapana mimi sijamgonga bhana maana kama nimemgoga basi ningesikia kishindo.!!"
       Stephan bado alikuwa na hofu huku safari ikiendelea kumpeleka Tresha kwake ili ampatie huduma ya kwanza arudi kwenye hali yake ya kawaida.

Yapata majira ya saa nne usiku ndipo Stephan aliwasili kwake na wakati huo bado mvua kubwa iliendelea kunyesha na ngurumo za radi zikichukua nafasi yake huku baridi likitanda kila kona ya jiji.

Baada ya kuwasili alipiga honi na bila kuchelewa mlinzi alifungua geti na Stephan kwa mwendo wa taratibu sana aliingiza gari ndani kisha kupaki sehemu husika.

"Hey Mayunga hebu njoo ushushe hii mizigo kwanza"
       Stephan alizungumza kumwambia mlinzi wake na bila kuchelewa mlinzi alisogea mpaka nyuma ya buti la gari na kuanza kutoa baadhi ya zawadi alizorudi nazo Stephan ila alipomtazama bosi wake alimuona akihangaika kumshusha mtu na hii ilimshangaza sana.

"Sa..samahani bosi, huyo ni nani na amepatwa na nini mbona amelegea kiasi hicho.!?"
     Mayunga uvumilivu ulimshinda na kuamua kumshushia swali Stephan ambae alimkata jicho kali mpaka aliogopa.

"Kwani mpaka lazima ujue, au mdio unataka kupeleka taarifa kwa mama, haya peleka basi nimeleta mwanamke ndani maana wewe umeletwa hapa na mama sio kwaajili ya ulinzi ila kwaajili ya kunichunguza mimi na kupeleka umbea kwa mama.!!"

"Hapana bosi sina maana hiyo ila nilitaka kujua tu lakini samahani sana kama nimekuudhi"
      Mayunga ilibidi aombe radhi, alichukua baadhi ya mozigo na kupeleka ndani lakini alipofika store ya kuweka mizigo alitoa simu yake na kumpigia mama Stephan.

Simu haikuita sana iliita kidogo na mwisho ilipokelewa na ndipo Mayunga alianza kumwaga umbea kwa mama Stephan kumueleza nini kinaendelea.

"Yaani mama huwezi amini, Stephan tayari ame....."
      Mayunga kabla hajamaliza kuongea simu yake ilichukuliwa na kuzimwa kabisa na aliefanya hivyo alikuwa ni Stephan alikuwa akimfuatilia nyuma kwa nyuma maana alijua lazima atapiga simu kwa mama yake.

"Sasa ulikuwa unataka kusema nini mbona mmbea wewe alafu ujue wewe ni mtoto wa kiume kwahiyo umbea haukupendezi hata kidogo kama ulikuwa hujui"

"Hapana bosi ila mama yako alikuulizia nikamwambia bado hujarudi lakini sasa umerudi nilitaka kumjuza kuwa umerudi ila sikuwa na nia ya kusema chochote!"
     Mayunga alijitetea lakini ukweli alitaka kueleza kile kinacho endelea na aliwekwa hapo na mama Stephan ili kutoa taarifa kwa kila anachofanya Stephan.

"Ahaaa sasa kama ni hivyo sawa ila kesho kukipambazuka uchukue mabegi yako uende mimi sihitaji mlinzi alafu kama ulikuwa hujui mimi nakufuatilia muda sana kwahiyo usijitetee"
      Stephan alikuwa ameshikwa na hasira, aliweka simu ya Mayunga mfukoni kwake na kurudi nnje ambapo alimchukua Tresha na kumuingiza ndani kisha alimuweka chumba cha wageni kwaajili ya kumpatia matibabu.

Alimfikisha na kumlaza kitandani ila alipoutazama mwili wa Tresha alimuonea huruma sana maana ulijaa vidonda, makovu na mguuni kwake alikuwa na jeraha kubwa sana.

"Huyu binti ni mtu wa aina gani mbona kila ninapomuona makovu yanamzidi au kuna mtu anamtendea huu ukatili.!!"
     Stephan alikuwa na maswali ambayo yalikosa majibu ila mwisho alianza kumfanyia huduma ya kwanza Tresha, alimtoa nguo alizovaa na kumvisha nguo zake.

Usiku huo ulikuwa mrefu sana kwa Stephan, maswali mengi yalijaa kichwani kwake na mwisho alipata usingizi saa tisa usiku ila kupopambazuka yeye ndiye alikuwa wa kwanza kuamka na alipotazama simu yake alikua missed call nyingi kitoka kwa mama yake.

Hakuwa na budi kumpigia na ilipopokelewa lawama zilianza

"Habari yako mama?"

"Salama tu ila umefanya nini sasa, kwahiyo sasa umeanza kwenda kinyume na mimi sio?"

"Kwanini mama mbona nashindwa kukuelewa.!?"
      Stephan aliketi vizuri kitandani maana alikuwa bado hajamuelewa mama yake alikuwa anazungumzia ninini.

"Mayunga mbona amekuja asubuhi asubuhi na mabegi yake inamaana imemfukuza eeh.!?"

"Ndio nimemfukuza mama mimi ni mtoto wa kiume sihitaji ulinzi wowote kwahiyo kama unahitaji kuwapata watoto zako ulinzi ni bora upeleke kwa dada Grace ila mimi sihitaji ulinzi na nikutakie asubuhi njema"
     Stephan alikata simu na kuelekea jikoni kuandaa kifungua kinywa ili kama Tresha akiamka basi akute kifungua kinywa tayari.

Wakati anamaliza kuandaa kifungua kinywa huku kwa upande wa Tresha ndio alikuwa anaamka lakini alishangaa kujikuta kwenye kitanda kikubwa cha thamani na hata chumba alichokuwepo kilikuwa ni chumba chenye vito vingi vya tahamani.

"Hapa ni wapi na nani amenileta hapa.!!?"
      Tresha alianza kujiuliza maswali huku macho yake yakitalii kila kona ya chumba hicho na alipoutazama mguu wake ulioumia aliona ukiwa na bandage pia hata nguo alizovaa hazikuwa nguo zake, jambo hili ililimpa hofu sana.

Wakati yupo kwenye mswali yasiyokuwa na majibu ghafla mrango wa chumba alichokuwa ulifunguliwa na kwa hofu aliyokuwa nayo alijiingiza kwenye shuka kisha alizuga kulala ili mtu huyo anaeingia asifahamu kama tayari alikuwa ameamka.

                ****************

Asubuhi na mapema katika kampuni ya Stephan kulikuwa na gari moja ya kifahari imesimama nnje na wakati Daniel anawasili aliiona gari hiyo ila hakufahamu ilikuwa gari ya nani, aliamua kuipotezea na kupaki gari yake sehemu husika kisha aliteremka.

Kwa mwendo wa taratibu alianza kijongea kuingia kwenye jengo la kampuni ila kabla hajazifikia ngazi alisikia akiitwa kwa jina lake na hii ilimpelekea ageuke haraka sana kumtazama nani aliemwita maana sauti ilisikika ya kike.

"Hello Daniel mzima wewe.?"
      Ilikuwa ni salamu kutoka kwa binti mmoja mrembo sana mwenye ngozi flani ya chocolate na alikuwa akitembea kwa mikogo kumsogelea Daniel.

Daniel alipomuona mwanamke huyo alijikuta akitabasamu maana alikuwa akimfahamu tena kwa kitambo sana.

"Ah Sasha weee daah siamini kama ni wewe yaani aumebadilika sana alafu na hiyo gari nilipoiona hapo nikajua huenda ni tajiri flani amefika kumbe ni wewe ila umependeza sana.!!"

"Asante sana lakini siku hizi mnachelewa kufungua ofisi maana nimefika hapa tangu saa kumi na mbili, nimekaa mpaka nimechoka bado kidogo niondoke nilifikiri leo hamfungui.!"

"Ah kufungua lazima ila funguo ninazo mimi lakini si unajua tena hatuwezi kufungua muda huo wa saa kumi na mbili hua kuna muda maalum wa kufungua lakini niambie maana leo umependeza hatari au ndio umekuja kumtega Stephan"
      Daniel alizungumza kama utani lakini jambo hilo lilikuwa na ukweli, Sasha alifika hapo kwaajili ya Stephan na ndie mwanaume alikuwa akimpenda kwa muda mrefu sana.

Miaka miwili iliyopita Sasha alikuwa ni mfanyakazi wa kampuni hiyo kitengo cha meneja masoko pia Sasha alikuwa akimpenda sana Stephan lakini Stephan hakumpatia nafasi ya kuwa nae hata kidogo na ndipo Sasha alichukua jukumu la kuacha kazi kwenye kampuni hiyo ili awe mbali na Stephan lakini baada ya miaka miwili sasa amerudi na kasi mpya kuhakikisha anapata penzi la Stephan kwa hali na mali.

"Jamani hapana sikuja kufuata penzi la Stephana kwanza nina mtu wangu tunapendana sana ila nimekuja kumsalimia tu alafu niende zangu"

"Ahaaa ok sawa ila leo sijui kama atakuja maana jana ameondoka hapa muda mbaya sana na ameniambia leo anaweza kuja au asije ila kwa nimavyomjua leo hawezi kuja kwahiyo nenda uje kesho au nipatie salamu nitafikisha"

"Mh hapana nilitaka nionane nae mwenyewe ila basi kesho mida ya saa nne nitakuja"
     Sasha aligeuka na kurudi lilipo gari lake lakini Daniel alibaki kumsindikiza kwa macho na udenda ulikuwa ukimtoka kwa jinsi Sasha alivyo fungasha.

"Yaani wahenga wanasema kweli bahati wanapata wajinga, kama mimi ningekuwa Stephan unafikiri ningeachaje zigo kama hili, daaah ila ipo siku na mimi Mungu ataniona tu"

Daniel hakuwa na jinsi kula kwa macho na mwisho gari ya Sasha ilipotokomea kwenye upeo wa macho yake aliendelea na safari yake kuelekea ofisini kuanza majukumu.

Tuachane na Sasha tuje kwa Joyce binti kiwembe anaewapanga wanaume kwenye foleni na asubuhi ya siku hiyo aliamka na mwanaume mwingine wakiwa hotelini.

"Jamani mpenzi mbona mapema hivi unataka kuondoka wakati bado nina hamu na wewe jamani.!!"
       Mwanaume ambae alilala na Joyce siku hiyo alizungumza baada ya mumuona Joyce akijiandaa kuondoka zake.

"Unajua Ochu muda umeenda sana natakiwa niwahi nyumbani ila usiku wa leo nitakupigia tukutane tena maana show yako nimeipenda sana"

"Basi mama usiniangushe chukua namba yangu hii utanicall"
     Ochu alitoa namba na kumpatia Joyce ambae aliiweka kwenye mkoba wake kisha alimuaga Ochu na kuondoka zake.

Alifika nnje na kuchukua tax ila alipopanda alifungua mkoba wake na kuchukua namba ya Ochu kisha aliichana na kuitupa haikuwa na thamani tena kwasababu alichotaka tayari alikipata na akili yake ilihamia kwa Stephan.

                *****************

Sasa turudi kwa Stephan na Tresha baada ya kufungua mrango na kuingia aligundua Tresha hakulala hivyo alikuwa amebeba kifungua kinywa, aliweka mezani na kutoka nnje kisha alielekea bafuni kuoga ila huku nyuma taratibu Tresha alifunua shuka na kukuta ameandaliwa kifungua kinywa.

Jambo hilo lilikuwa geni kwake maana alizoea asubuhi anaamshwa kwa kumwagiwa maji baridi au kupigwa mangumi na kifungua kinywa anaweza asipate lakini siku hiyo ilikuwa tofauti sana kwake.

Hakufahamu mpaka wakati huo ni nani ambae amempa msaada ila kwa akili yake ya haraka alifikiri huenda ni mwanamke.
     Basi alijongea mpaka ilipo ile sahani na bila kuchelewa alianza kufakamia kile chakula na kukimwagia sifa nyingi.

"Huyu dada anajua sana kutengeneza brakefast, tangu niishi na shangazi sijawahi pata chakula kizuri kama hiki.!!"
     Tresha mpaka alianza kuramba vidole ila alipomaliza alibeba ile sahani taratibu na kutoka nnje lakini alipofika sebuleni na kutazama ukutani alikuta kuna picha na picha ile ilikuwa ya Stephan.

"Inamaa hapa ni nyumbani kwa yule mpuuzi.!?"
      Tresha alibaki ameduwaa lakini akiwa kwenye mshangao ghafla alisikia sauti ambayo ilimshtua na kupelekea aangushe vile vyombo chini.

"Tafadhali vyombo peleka jikoni nitavisafisha"
     Kauli hiyo ndio ilimshtua Tresha na alipotazama alieuzungumza alikuwa ni Stephan tena alikuwa kifua wazi na chini alivaa tauro baada ya kutoka kuoga.

Kilikuwa ni kitendo kilichomuogopesha sana Tresha, alitoka mbio na kurudi chumbani huku akimuacha Stephan akicheka na kuelekea chumbani kwake.

Muda ulikwenda na ilipotimu saa nne Tresha akiwa chumbani aliingia Stephan na bila kuuliza alimshika mkono na kumtoa nnje mpaka lilipo gari lake na kumpakia.

"Nakuomba utulie tafadhali tunaenda kununua nguo najua huna nguo za kuvaa"

"La...lakini"

"Sitaki kujua, utanieleza baadae tukirudi kwahiyo kwanza unisikilize mimi alafu baadae utanieleza kila kitu kuhusu maisha yako"
      Stephan aliwasha gari yake na safari ilianza huku Tresha akibaki kumtazama Stephan na kujiuliza ni mwanaume wa aina gani ila hakupata jibu.

Walifika katika duka moja maarufu la nguo na waliposhuka Stephan alimuomba Tresha amsubiri kisha alielekea ATM kwenda kutoa pesa lakini bahati mbaya shangazi yake tresha nae siku hiyo akiwa na shoga yake walifika kwenye duka hilo hilo kufanya manunuzi ya nguo.

"Shoga hivi yule sio Tresha wangu kweli"
     Shangazi alizungumza huku akitazama vizuri na rafiki yake alipomtazama alihakikisha ni yeye Tresha.

"Kumbe mtoto ni malaya hivi, sasa kweli gari ile anafanya nini, ngoja nimuoneshe"

Shangazi kwa hasira alitembea haraka mpaka alipo Tresha na alipomfikia hakutaka kuuliza mara mbili alimshika mkono na mumvuta pemben.

"Shangazi.!!?"
       Tresha alishangaa kumuona shangazi yake lakini shangazi hakutaka kuongea kitu, alimfikisha mpaka karibu na umati wa watu na kuanza kumuhoji.

"Ulikuwa unafanya nini pale kwenye lile gari, umeanza umalaya eeh, ulitaka kipi mimi sijakupa au unataka kunitia aibu"
      Shangazi alihoji kwa jazba na wakati huo tayaari alijiandaa kumpiga Tresha.

Tresha alinywea maana alijua hasira za shangazi yake, alifungua mdomo wake ili kujibu lakini aliambulia kofi zito lililomfanya abaki na alama shavuni, haikuishia hapo shangazi alivua kiatu chake ili kumuadhibu Tresha lakini ghafla alishangaa mkono wake umedakwa na aliefanya hivyo alitokea nyuma yake.....ITAENDELEA...

- Unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo yameanza kuwa moto lakini nisikuchoshe niseme tukutane sehemu ya tano ya mkasa huu wa kisisimia na kuelimisha..