Jina....TABASAMU LA UCHUNGU
Mtunzi....... Official Dully
Mkasa....wa...kusisismua
Sehemu Ya {03}
ILIPOISHIA..
Stephan alijiongelesha mwenyewe lakini aliona haitoshi alipaki gari yake kando ya barabara na kushuka kumfuata Tresha ambae alikuwa busy hana ili wala lile, alijongea mpaka karibu yake na alipomkaribia alimshika mkono ila alipomtazama usoni alimuona akiwa na majeraha mengi aliyoyapata baada ya kushushiwa kipigo kizito na jambo hilo lilimuuma sana Stephan....ENDELEA....
Stephan alimtazama kwa muda Tresha na kujikuta akimuonea huruma sana kwa jinsi alivyo na sehemu kubwa ya mwili wake ilitapakaa makovu yaliyotokana na kipigo kizito kutoka kwa shangazi yake.
"Habari yako dada, wewe si yule ambae ulinipatia wallet yangu mbona una majeraha hivi shida nini.!?"
Stephan alimuuliza Tresha huku amemkamata mkono lakini Tresha alipomtazama Stephan alimkumbuka na alikumbuka huyo ndiye sababu ya yeye kupokea kipigo kikali.
"Hebu niache tafadhali.!!"
Tresha aliutoa mkono wake kwa nguvu kwenye mkono wa Stephan na kuanza kurudi nyuma, hali iliyopelekea Stephan amshangae na taratibu alianza kupiga hatua kumsogelea.
"Shida nini dadaangu, kwani kukuuliza ni kosa au kuna jambo ambalo unaliogopa kutoka kwangu, hebu niambie tafadhali.!?"
Stephan aliendelea kumuhoji Tresha huku akimsogelea lakini Tresha hakutaka kubaki tena hapo, alivuka barabara kwa kukimbia na kutokomea pasipo julikana huku akimuacha Stephan mwenye maswali mengi kichwani.
"Hivi huyu binti kwanini ameniogopa au huenda kuna jambo analiogopa kutoka kwangu, ok sawa kama ameamua muche aende kila mtu na maisha yake mjini hapa"
Stephan alijiongelesha mwenyewe huku taratibu akijongea lilipo gari lake na kuanza safari ila mawazo juu ya Tresha hayakuacha kumuandama.
Hata alipofika ofisini kwake alikuwa tofauti na hii ilifanya wafanyakazi wake wamshangae maana hakuwa na kawaida kufika kazini na kuwapita wafanyakazi wake bila kuwapatia salamu au hata kuwafurahisha kidogo.
"Jamani Daniel kwani leo bosi amepatwa na nini mbona ameingia hata salamu hajatoa na sio kawaida yake kabisa.!?"
Lilikuwa ni swali kutoka kwa dada mmoja ambae nae alikuwa mfanyakazi wa kampuni hiyo huku akiongozana na jopo la wafanyakazi wenzake kutaka kujua bosi wao kapatwa na nini.
"Sikia nikwambie Marry hata mimi sifahamu lakini msijali mimi nitaenda kumuuliza shida nini na nitawapa taarifa kwahiyo endeleeni na majukumu yenu tafadhali"
"Ok sawa"
Wafanayakazi wote hawakuwa na budi kurudi kwenye meza zao huku Daniel taratibu alitoka hapo na kuelekea ilipo ofisi ya Stephan ili kujua nini kimemkuta au kuna jambo gani ambalo limemtatiza.
Stephan aliingia ofisini kwake na kuvua koti lake kisha aliliweka juu ya meza na kuketi kwenye kiti huku bado akimfikira Tresha.
"Au huenda kukutana nae ile jana ndio imekuwa sababu ya kupigwa kama vile, yule aliempiga ni nani mbona hana hata aibu, lazima ni....."
Stephan kabla hajamaliza kuomgea mrango wa ofisi yake ulianza kugongwa na bila kuchelewa alimruhusu mgongaji aingie.
"Daniel eheee niambie kuna mpya gani.!?"
"Ah swali hilo natakiwa kukuuliza wew kuna mpya gani mbona upo tofauti leo mpaka wafanyakazi wako weshindwa kufanya kazi wanahoji nini kimekupata.!!"
"Hahaha amna bhana kawaida ila Danile kusema ukweli kuna jambo linanitatiza sana na jambo hilo hata sielewi nifanye nini kulitatua.!?"
Stephan alizungumza huku akilegeza tai yake vizuri shingoni apate kuzungumza.
"Jambo gani tena hilo ndugu yangu.!?"
Stephan hakuwa na jinsi ilibidi aanze kumsimulia Daniel mwanzo mpaka mwisho na kumfanya aangue kicheko kilichomkera sana.
"Sasa unachocheka wewe ni nini hapo.!?"
"Amna ila umefanya nifurahi sana yaani machokoraa tu wa mitaani wanakuumiza kichwa, hebu achana nao huenda huyo binti amepigwa kwasababu ni mwizi, sasa wewe hushangai binti kama huyo anaenda supermarket kufanya nini kama sio kuiba.!!"
"Hapana mimi nakataa hilo maana nilipoenda supermarket kununua baadhi ya mahitaji niliangusha wallet yangu lakini aliokota na kunirudishia sasa kama angekuwa mwizi angenirudisha kweli.!?"
Swali hilo lilimfanya Daniel akae kimya lakini mwisho aliona apotezee na kuingiza mada ya mwanamke ambae alimpatia namba ya Stephan jana.
"Alafu mwanangu unajua yule demu leo alikuja hapa nikampa namba yangu baada ya muda alinipigia na kuniuliza kwanini namba yako haipatikani na kweli hata mimi nipokupigia ilikuwa haipatikani sasa sijui nini tatizo.!?"
"Ah nimebadilisha namba hua sipendi usumbufu na wanawake na namba hii hata wewe sikupi kwahiyo ukitaka kunitafuta utanitafuta kwa namba yangu ya nyumbani kwenye simu ya mezani lakini hii siwezi kukupa"
"Mh sasa unaogopa nini, mimi siwezi kumpa tena namba yako nitamwambia tu umebadili line ila nikwambie ukweli yule demu ametokea kukupenda yaani upendo wake hata haujifichi"
Daniel alizunguza na kumfanya Stephan ainuke na kumsogelea karibu.
"Naona sasa umechoka kuzungumza na mimi haya nenda nnje haraka sana sitaki kukuona hapa, wewe kama unamtaka utajua wewe lakini usiniambie habari za kijinga hapa"
Stephan alikuja juu na kumfanya hata Daniel aingiwe na hofu, hakutaka kuendelea kukaa humo alitoka na Stephan alifunga mrango kwa ndani hakuhitaji mtu yeyote kuingia tena.
**************
Tukiachana na Stephana tuje upande wa Joyce, binti ambae ni kiwembe mjini, hua akihitaji mwanaume basi ndani ya siku mbili lazima ampate ila kwa Stephan alidunda na hii hata yeye ilimshangaza sana.
Siku hiyo alienda kwa rafiki yake ambae alijulikana kwa jina la Pendo na kilichompeleka hapo ni kuzungumza juu ya mwanaume anaesumbua akili yake.
"Lakini Pendo we nae umezidi yaani kila mwanaume anaepita mbele ya macho yako basi unamtamani hivi utatembea na wangapi shoga yangu, ona mimi nimetulia na huyu wangu yaani raha mustarehe"
"Kwahiyo unanisema au?"
"Hapana sio nakusema ila nakushangaa shoga yangu hebu badilika ila kama hutaki basi mimi nitakushauri unachotaka"
"Sawa ila leo nimekuja hapa nahitaji kuna mambo umishauri maana kila mwanaume ninaemtaka nampata lakini kuna huyu Stephan yaani ananiumiza kichwa sana sasa sijui nifanye nini.!?"
Joyce alizungumza huku akitoa simu yake na kuingia mtandaoni kisha alimuonesha Pendo picha ya Stephan.
"Mh shoga yangu yaani wanaume wote unaowafuatilia wa kawaida ila huyu anavutia jamani lakini acha nikwambie, kama unamtaka usisumbuke kumtafuta kwa simu wewe funga safari mpaka kazini kwake, onana nae alafu muombe kama ana muda basi mtafute sehemu muongee naamini atajiongeza"
"Eti eeeh.!?"
"Ndio ila si hana mpenzi au.?"
"Hana"
"Mh we ulijuaje.!?"
"Jamani si ameniambia mfanyakazi wake kwani unafikiri mimi namfuata mwanaume kijinga bila kumchunguza, kwanza namfanyia utafiti alatu namfuatilia kwahiyo ulichonishauri nitakifanyia kazi"
"Ila ukienda sio unaenda kama unaenda kwenye matanga yaani vaa vinguo vya kumtega naamini hawezi kuchomoa jino moja"
"Ok basi sawa acha nikuache ila ipo siku nitapanga muda nitaenda"
Joyce alimuaga Pendo na kuondoka zake lakini Pendo alimshauri kama rafiki ila hakupenda kabisa tabia ambazo anafanya Joyce aliona ipo siku ataingia matatizoni.
Tutoke huko tuje kwa Tresha, binti anaepitia wakati mgumu sana lakini yote ni baada ya kufiwa na wazazi wake ambao ndio walikuwa nguzo ya maisha yake.
Tresha alikuwa chumbani kwake amepumzika lakini ghafla mrango wa chumba chake ulifunguliwa na alieingia alikuwa ni mjomba yake maana shangazi yake alikuwa ametoka na nyumba nzima alibaki yeye na mjomba yake tu.
"Mjombaa mbona unaingia chumbani kwangu pasi na kugonga mrango hivi huoni kama sio adabu nzuri.!?"
Tresha alizungumza huku akijiinua na kuketi.
"Hebu kelele ila leo nataka unisaidie kitu kimoja maana nimekuwa nikikutazama kwa muda na kunitia hamu lakini leo nataka uimalize hamu yangu"
Mjomba alizungumza huku akimsogelea Tresha ambae alijua nini mjomba anataka na hii ilimfanya ajikunje kwa hofu.
"La..la..lakini mjomba ujue wewe ni kama baba yangu hivi huoni unajivunjia heshima.!?"
"Ushasema ni kama baba yako lakini sio baba yako mimi kwahiyo kaa kwa kutulia nimalize hamu yangu"
Mjomba bila aibu alianza kuvua nguo zake na alipobaki mtupu alimrukia Tresha na kuanza kumlazimisha wafanye mapenzi kwa nguvu.
Ilikuwa ni purukushani iliyoanza hapo maana Tresha alijaribu kila awezalo kumzuia mjomba yake lakini alizidiwa nguvu na kuanza kuchaniwa nguo zake.
"Mjomba tafadhali niacheeee.!!"
Tresha alipiga kelele lakini mjomba hakutaka kumsikiliza, ila wakati zoezi hilo linaendelea ghafla shangazi aliingia na kushangaa jinsi mume wake alivyokuwa akilazimisha kufanya mapenzi na Tresha.
Lilikuwa ni tukio la aibu sana kwa mjomba lakini shangazi alijongea mpaka walipo na kitu cha kwanza alimshika Tresha na kuanza kumshushia kipigo pasi na kosa ilhali mume wake ndiye alikuwa mkosaji.
****************
"Yaani mtoto mshenzi sana wewe, kukuhifadhi kwenye nyumba yangu hukuridhika ukaona uanze kutembea na mume wangu, sasa leo nitakufunza adabu na nyumbani kwangu utaondoka..!!"
"Lakini shanga mjomba mwenyewe ndie amekuja chumbani kwangu na kuanza kutaka kunibaka lakini mimi sina kosa lolote shangazi.!!"
Tresha alijitetea lakini hakusikilizwa na kilichofuata hapo ni kipigo mpaka mwili ulianza kumuisha nguvu.
Haikuishia hapo alichukuliwa na kutupwa nnje pamoja na nguo zake huku matusi ya nguoni yakimsindikiza nyuma.
"Shangazi nisamehe sina kosa mimi.!"
"Huna kosa eeh, sasa acha dunia ikifunze malaya mtoto wewe na hapa sitaki kukuona kama unataka usalama nenda kawafuate wazazi wako walipofukiwa maana wao ndio wamekufunza umalaya"
Ilikuwa ni kauli ya mwisho kwa shangazi kisha alifunga geti na kurudi ndani huku akimuacha Tresha akiangua kilio na kuomba msamaha.
Taratibu muda ulianza kusogea na hatimae kiza kiliingia huku Tresha akiwa hapo hapo nnje amekaa akidhani huenda roho ya huruma itampata shangazi na kuja kumsamehe lakini ilikuwa patupu.
Hali ya hewa taratibu ilianza kubadilika, upepo mkali ulivuma na ngurumo za radi zilianza kusikika kuashiria muda wowote mvua kubwa ingeshuka.
Kweli bhana hazikupita dakika nyingi mvua kubwa ilianza kushuka ikiambatana na radi pamoja na upepo mkali uliokaribisha baridi ambalo lilianza kumtesa Tresha.
"Hivi nitakaa hapa nikinyeshewa na mvua mpaka saa ngapi, baridi kali sana ni bora nitafute sehemu nijikinge maana naweza kupata homa nikiendelea kubaki hapa"
Tresha alijiwazia na mwisho alikusanya nguo zake taratibu na kuingia mtaani akitafuta sehemu ambayo itamuwezesha kujikinga na mvua.
Wakati hayo yanaendelea huku Stephan alikuwa njiani kurudi kwake na muda ulisomekaa saa mbili usiku, usiku uliosheheni mvua ya kutisha na baridi kali.
"Mh aisee hii mvua hatari sana!"
Stephan taratibu aliendelea na safari yake lakini akiwa njiani simu yake iliingia message hivyo aliichukua na kuitazama lakini aligundua ni message za mtandao hivyo aliirudisha simu mahali ilipokuwa lakini alipoinua macho kutazama mbele ghafla alimuona mwanamke akikatiza mbele yake na mwanamke huo alikuwa akitembea kwa kuchechemea hivyo alijikuta akikanyaga mbreki kwa nguvu ili kukwepa kumgonga.....ITAENDELEA..
Mh mambo yamekuwa magumu kwa Tresha, unafikiri nini kitafuata, maisha yake yaliyojaa mateso yataisha lini, mimi na wewe hatujui lakini majibu utayapata sehemu ya 04 ya mkasa huu wa kusisimua..
