Jina....TABASAMU LA UCHUNGU

Mtunzi........Official Dully

Mkasa....wa...kusisismua

            Sehemu Ya {02}

ILIPOISHIA...

Tresha alijibu na hakutaka kabisa kuendelea kubaki hapo aligeuka na kuondoka zake kwa mwendo wa haraka huku nyuma akimuacha Stephan akimtazama na kuachia tabasamu pana ambalo liliashiria kuna jambo lilikuwa la siri akilini mwake.....ENDELEA...

Stephan alibaki kumsindikiza Tresha kwa macho mpaka alipotokomea nae alipanda kwenye gari yake na kuiwasha tayari kwa safari lakini akilini mwake alijikuta akimfikiria Tresha pasi na kujitambua na jambo hili lilimshangaza sana.

"Ila huyu binti ni mwema sana yaani ameokota wallet yenye pesa nyingi kiasi hiki alafu anarudisha mh hapana huenda huyu ni malaika maana zama za sasa uangushe kitu cha thamani alafu urudishiwe ni bahati sana"

       Stephan alijiongelesha na kukanyaga mafuta kuanza safari lakini upande wa Tresha nae alielekea kwenye supermarket aliyotoka Stephan kwaajili ya kununua mahitaji ya nyumbani na hiyo ilikuwa kawaida yake kila siku.

Alianza kuchagua baadhi ya bidhaa ambazo alihitaji lakini akiwa busy alifika mtu nyuma yake na kumkamata sikio kwa nguvu na kitendo hicho kilimtia maumivu makali sana.

     Hakuwa mwingine ila alikuwa ni shangazi yake aliefika hapo na alikuwa akimfuatilia hatua kwa hatua wakati anakuja kununua mahitaji pasi na Tresha mwenyewe kujua.

"Yaani leo huniambii chochote nimekuona kwa macho yangu mshenzi mkubwa  wewe"

"Shangazi..!! nimefanya nini tena alafu umefika saa ngapi mbona sijakuona wakati unakuja.!?"

      Tresha aliongea huku akiwa amejikunja kwa maumivu ambayo alikuwa akihisi kwa wakati huo.

"Ulitaka unione ili iweje na yule mwanaume uliekuwa nae pale nnje ni nani mliokuwa mnacheka na kukumbatiana, nataka kumjua la sivyo nakurarua vipande vipande.!!"

"Jamani shangazi mbona sijakumbatiana na mtu, yule kaka aliangusha wallet yake sasa nimeokota nikaona nimpelekee lakini sikumkumbatia wala kumshika mkono jamani.!"

"Kwahiyo unanifanya mimi kipofu eeh sasa ngoja nikuoneshe"

Suangazi hakuwa na huruma hata kidogo yaani kiufupi alikuwa akimchukia sana Tresha hivyo alianza kumshushia kipigo kizito hapo hapo na kupelekea watu wajae kutazama kile kilichokuwa kinaendelea hapo.

    Kila aliefika hapo alikuwa na moyo wake, wapo waliodiriki kimtetea Tresha na wapo waliodiriki kuona ni kama maigizo ya filmau, walichukua video kwa simu zao na kutupia mitandaoni ili kupata view na like.

"Hebu jamani dada muache huyo binti, mbona unampiga kiasi hiki alafu umri wake ni mkubwa haifai kupigwa kabisa sasa amekosea nini mpaka unamuadhibu kiasi hiki na hutaki kumsikiliza kabisa.!!"

      Yalikuwa ni maneno ya mama mmoja mtu mzima ambae alifika hapo na kumshika mkono Tresha kisha kumvutia nyuma yake.

Wakati huo tayari Tresha alikuwa ameumia vibaya sana baadhi ya sehemu za mwili wake na watu hawakukoma kumchukua video.

"Dada tafadhali naomba acha nimuadhibu, huyu mtoto ni jeuri sana yaani unamtuma anachelewa kumbe kazi yake akifika huku anasimama na wanaume wanamshika makalio basi anaona raha kabisa sasa acha nimuoneshe"

       Shangazi alikuwa hataki kusikia wala kuambiwa lakini yote hayo alifanya kwa chuki zake binafsi.

Yule mama baada ya kuambiwa hayo alimgeukia Tresha na kumuuliza kama alichokuwa anaongea shangazi yake kina ukweli au laa.

"Hapana mamaangu mimi sina tabia hiyo kabisa ila kuna mkaka aliangusha wallet yake nikaona nimfuate nimpatie lakini sikushikana nae mkono wala kukumbatiana nae"

     Tresha alijitetea lakini shangazi hakutaka kukaa hapo tena alitoka na kuondoka zake lakini bado moyoni aliapa kumfunza adabu kabisa Tresha mpaka dunia aione chungu.

Baada ya shangazi kuondoka yule mama alimchukua Tresha na kumpeleka lilipo duka la dawa kwaajili ya kumfanyia matibabu sehemu zote alizoumia kutokana na kipigo kikali alichopatiwa.

"Pole sana binti lakini siku nyingine ukitumwa kwanza wahi nyumbani alatu hayo mengine baadae, wewe ni binti mkubwa una haki ya kuwa na mpenzi lakini unapotumwa usiweke mambo mengine mbele fanya ulichotumwa"

"Ni sawa lakini sojafanya chochote kibaya na hua kawaida yake sana kunipiga kila siku, tazama haya makovu ni kwaajili yake kwahiyo nimezoea"

"Oh pole sana sasa mama na baba wako wapi.!?"

     Swali hilo lilikuwa kama mkuki uliolengwa kwenye kidonda cha Tresha na kumfanya ahisi maumivu makali sana yaliyomkumbusha mbali.

"Mama na Baba yangu kama wangekuwa hai naamini haya yote yasingetokea na ningeishi kwa amami lakini kwakua hawapo basi nakubaliana na yote ila naamini ipo siku yatakwisha kabisa haya"

     Tresha aliongea maneno ambayo yalimfanya yule mama kulengwa na machozi ila hakuwa na jinsi ya kufanya zaidi ya kumfariji na kumtaka arudi kwao.

"Sawa mwanangu nenda pia nakuombea kwa Mungu akupatia tabasamu la milele"

"Sawa mama kwaheri"

       Tresha alimuaga yule mama kisha alirudi mpaka supermarket kuchukua bidhaa zake alizoacha na kuondoka zake ila moyoni alikuwa na hofu sana akiwa anajua huko anapokwenda kutakwenda kuwa balaa kwake na hakutakuwa na mtetezi.

                 ****************

Stephan alikuwa hana ili wala lile, alikuwa busy barabarani akiendesha gari kurudi kwake lakini muda huo huo simu yake ilianza kuita na namba iliyokuwa inapiga haikuwa na jina hivyo akaamini kabisa lazima atakuwa mwanamke ambae alinunua magari kwenye kampuni yake.

      Hakutaka kuipokea aliacha ikiita mpaka ilipokata na haukupita muda iliita tena ila safari hii aliipokea na kumsikiliza.

"Hello?"

      Sauti ya kike ilisikika na ilikuwa laini sana ambayo ilipenya vyema masikioni mwa Stephan na kusisimua ngome za masikia yake.

"Hello mbona huongei.!?"

"Hey we binti mbona una fujo kiasi hicho si useme shida yako alafu ukate simu kwani lazima mpaka na mimi nizungunze ok sawa Hello, Hello, Hello"

       Stephan hakutaka kabisa mazoea na huyo binti lakini kuongea kwake kulikuwa kama kunatekenya mbavu za binti huyo na kufanya aangue kicheko lakini mwisho Stephan alikata simu na kuizima kabisa.

"Yaani mabinti wengine sijui wapoje, mtu unapiga simu basi sema la maana lakini yeye hallo hallo kama muuza sumu ya panya alafu yote kataka Daniel haya kumpatia namba yangu sasa subiri kesho nitamchana ukweli aache kutoa namba yangu hovyo.!!"

Stephan alikuwa mtu wa kulalamika njia nzima lakini upande wa huyo binti alikuwa kitandani amekumbatia mto na kuketi huku akijaribu kupiga namba ya Stephan kila wakati lakini jibu lilirudi namba haipatikani.

"Mh ndio kaamua kuzima simu kabisa ok nitampata tuu najua lazima atawasha tena"

    Binti huyo alijisemea na kutupa simu yake pembeni ila wakati huo huo mrango wa chumba alichokuwa yeye ulifunguliwa na aliingia binti mdogo anapata kama miaka 17 au 18.

"Dada Joyce mbona unaonekana una mawazo sana au ndio huyo kaka uliesema umekutana nae anakudatisha maana wewe ukikutana na mwanamke mtanashati basi unadata nae sasa sijui utatembea na wangapi"

"Hey Stellah hebu niache kwanza maana ukijaga wewe hapa sikai hata kwa amani kwahiyo nakuomba uende chumbani kwako kabla sijamwambia mama"

"Ok sawa ila sikuwezi wewe dada penda penda"

      Stellah alitoka kwenye chumba hicho akisindikizwa na tusi zito ambalo lilitoka kinywani kwa Joyce.

Joyce alikuwa ni binti wa miaka 23, binti ambae amekulia kwenye maisha ya kitajiri na wazazi wake walikuwa na pesa nyingi sana ambazo zilitosha kumpatia kila anachotaka ila Joyce licha ya kupata anachotaka lakini alikuwa kama kiwembe kila mwanaume mtanashati anaepita mbele yake basi lazima alale nae.

Makumi ya wanaume tayari alipita nao wakati huo alikuwa kwenye harakati za kuhakikisha anamnasa Stephan ila kwa upande fulani alianza kuona ugumu kwa mwanaume huyo.

"Yeye si wa kwanza kujifanya mgumu, wapo waliopita walikuwa kama yeye ila mwisho walisalimu amri kwahiyo na yeye lazima atanasa kwenye mtego wangu sina papara na mimi ndiye Joyce og"

Yalikuwa ni mawazo ya Joyce, hakutaka kukata tamaa kabisa kwenye swala la kumpata Stephan alikuwa na aimani ipo siku atamuingiza kwenye mtego wake na kutimiza lengo lake.

                  ***************

Muda uliyoyoma na hatimae usiku uliingia, usikuwa uliokuwa tulivu sana kwa upande wa Stephan lakini kwa Tresha ulikuwa ni usiku wa mateso na kilio tu.

"Shangazi naomba unisamehe nipatie chakula angalau kidogo tangu asubuhi sijala mimi naomba tafadhali shangazi yangu.!!"

      Tresha alikuwa amepiga magoti mbele ya shangazi yake huku akimwaga machozi na kushika tumbo lake lililokuwa likiunguruma kwa njaa kali.

"Ahaaa unataka chakula ok hata usijali mtoto wangu mzuri ila kuna sharti moja tu, kama unataka chakula kwanza nibandike maji ya moto jikoni uje unisafishe miguu yangu alafu nitakupa chakula"

"Sawa shangazi"

      Tresha kwakua alikuwa na njaa sana basi hakuwa na jinsi kufanya kama alivyoambiwa ili kupata chakula.

Alibandika maji jikoni na yalipopata moto aliyapoza kisa alimsafisha miguu shangazi yake na alipomaliza ilibidi amjulishe ili apatiwe kile ambacho aliahidiwa.

"Shangazi tayari"

"Oh tayari ok nisubiri hapo hapo mwanangu mzuri"

     Shangazi alizungumza huku akiinuka na kuelekea jikoni na baada ya dakika kadhaa alirudi akiwa na sufuria iliyosheheni makoko ya wali kisha alimpatia.

Chakula hicho kwa upande wa Tresha kilikuwa kama asali, alikifurahia na kukipokea kwa mikono miwili huku akimshukuru shangazi yake ambae alikuwa akimtazama na kubaki kucheka.

Upande wa Stephan alipanda kitandani kwake na kuchukua laptop yake kutazama mambo yaliyojiri mtandao ila wakati anapita kutazama habari mbali mbali aliona post iliyomuonesha binti akipigwa na post hiyo ilikuwa ni video hivyo aliifungua na kutazama.

"Mh huyu si yule binti ambae amenipatia wallet yangu, why anapigwa kiasi hiki.!?"

      Stephan alibaki mwenye maswali na mawazo lakini aliona apotezee.

"Ok kama nitamuona tena basi nitamuuliza shida ni nini"

Hakutaka kuendelea kuitazama ile video alitoka na kuwasha simu yake na muda huo huo simu yake ilianza kuita na aliekuwa anapiga alikuwa ni Joyce,  hakutaka kumpokelea alimkatia na kuzima kabisa huku kichwani kwake akipanga siku imayofuata abadili laini ya simu.

Kweli siku iliyofuata asubuhi na mapema Stephan alifanya kama alivyokusudia, alisajili laini nyingine alakini wakati anaelekea kazini kwake alimuona mtu ambae sura yake haikuwa ngeni machoni mwake na mtu huyo alikuwa anavuka barabara haraka.

"Tresha..! huyu si ndiye mwanamke wa jana au.!?"

 Stephan alijiongelesha mwenyewe lakini aliona haitoshi alipaki gari yake kando ya barabara na kushuka kumfuata Tresha ambae alikuwa busy hana ili wala lile, alijongea mpaka karibu yake na alipomkaribia alimshika mkono ila alipomtazama usoni alimuona akiwa na majeraha mengi aliyoyapata baada ya kushushiwa kipigo kizito na jambo hilo lilimuuma sana Stephan....ITAENDELEA....

Unafikiri nini kitafuata hapo baada ya wawili hao kukutana, mimi sina mengi ya kuzungumza lakini nakuomba tukutane kesho Mungu akipenda  kwaajili ya kuisoma sehemu ya tatu....