Jina....TABASAMU LA UCHUNGU
Present.......Story Za Mapenzi
Mkasa....wa...kusisismua
Sehemu Ya {01}
Utangulizi.....
Tabasamu la uchungu ni simulizi ya kusisimua ambayo itakufanya uburudike uelimike na pia ujifunze mengi kuhusu maisha pia simulizi hii imebeba uhalisia wa maisha ambayo watu wengi hukutana nayo au huenda wamekutana nayo lakini simulizi hii naimani utaifurahia na kuipenda kwahiyo tuazime macho na akili yako kusoma mkasa huu mpaka tamati naamini utajifunza kitu katika maisha....Songa»»»
Tresha ni binti wa miaka 23 binti ambae maisha yake hapo awali yalikuwa kijijini kwa wazazi wake lakini baada ya wazazi wake kufariki alichukuliwa na dada wa baba yake yaani shangazi yake na kwenda kuishi ndani ya jiji la Dar es salaam, jiji zuri ambalo liligeuka ghafla na kuwa shubiri kwa upande wake.
Tresha alikuwa ni binti mpole sana asiependa kuongea sana lakini upole wake huenda ndio ulipelekea kuyaona maisha ni kama shubiri.
Ilikuwa ni siku moja ya jumaatatu tulivu sana Tresha alikukurupuka kutoka usingizini baada ya kumwagiwa maji ya baridi na shangazi yake na hiyo ilikuwa kawaida kwake maana mara nyingi jambo hilo hutokea japo hua linamkera sana ila hua hana jinsi ya kufanya.
"We mshenzi yaani tayari umefanya nyumba ya wazazi wako eeeh haya inuka haraka kama umesahau wajibu wako wa kila siku basi leo nitakukumbusha"
Shangazi alizungumza kwa hasira huku ameshika kiuno akimtazama Tresha ambae taratibu alijivuta kutoka kitandani na kupiga magoti mbele yake.
"Yaani una bahati sana mjomba yako leo yupo lakini kama asingekuwepo basi ningekuchakaza mpaka dunia ungeiona chungu mshenzi wewe"
"Nisamehe sana Shangazi lakini jana nilichelewa kulala kazi zilikuwa nyingi"
Tresha alizungumza kwa sauti yake ya upole lakini alichoambulia ni kofi matata lililopelekea ayumbe kama mtu aliekunywa pombe kali.
"Mshenzi kabisa wewe, umeanza lini tabia yako ya kunijibi pindi nikiongea, umeanza ujeuri eeh au tayarii umepata bwana ambae anakupa jeuri huko mtaani.!?"
"Hapana Shangazi nisamehe.!"
"Sasa inuka uwaandae wanangu waende shule, uandae kifungua kinywa na adhabu yako hutakula mpaka usiku kwahiyo nikifumba macho na kufumbua naomba nikukute jikoni"
Tresha bila kuchelewa aliinuka na kuelekea jikoni lakini alikuwa na majonzi sana kiasi kwamba alijikuta machozi ya uchungu yakimtoka na hiyo ilikuwa kawaida yake kila siku kumwaga machozi.
"Mama..Baba najua mnahuzunika sana mkiangalia haya maisha ninayopitia lakini acha niwaambie Mungu yupo na kuna siku mtaona tabasamu langu maana Mungu alieumba mdomo basi lazima atakupa na tabasamu kwahiyo msihuzunike sana naamini ipo siku na mimi nitatabasamu na kucheka"
Maneno ya uchungu yaliyoambatana na machozi yalimtoka Tresha huku akiwa busy kuandaa kifungua kinywa.
Wakati akiendelea na zoezi hilo Shangazi yake alifika na kusimama mbele yake huku akiwa na beseni ndogo iliyosheheni unga wa ngano.
"Alafu nilisahau kama leo rafiki yangu na mume wake wanakuja kunisalimia kwahiyo shika hii ngano utengeneze chapati nyingi ila olewako uziharibu yaani nitakupiga na hapa utahama"
Shangazi alizungumza kwa vitisho na kuondoka huku Tresha akimsindikiza kwa macho yaliyojaa hofu na woga.
Hakuwa na jinsi kuchukua ile ngano na kuanza kutengeneza ila yote alifanya kwa tahadhari maana alijua kama atakosea hata kidogo basi kifuatacho ni kipigo na kunyimwa chakula.
Muda ulikwenda hatimae wageni waliosubiriwa kwa hamu walifika, Tresha aliwapokea na kuwakaribisha vizuri pia aliwakaribisha mezani na kuanza kuandaa kifungua kinywa.
"Hivi Catherine huyu binti ni nani mbona amechangamka hivi alafu anajua kupika sana, nimependa mapishi yake kwakweli.!?"
Lilikuwa ni swali kutoka kwa rafiki wa Shangazi yake Tresha ambae walikuwa wakijuana kwa kipindi kirefu sana.
"Ah huyo ni mfanyakazi wangu yaani hata mimi nampendea hapo anajua sana kupika yaani akipata mume basi mume wake ataenjoy sana hahaha.!?"
Sifa kibao zilimiminika kwa Tresha lakini Tresha mwenyewe hakuwa na wasiwasi kabisa wala kufurahia sifa hizo maana alijua baada ya hapo kinachofuata ni kipigo na kusemwa.
*************
Tuache kwa Tresha tuje kwenye ofisi ya kampuni kubwa ambayo inajishughulisa na uuzaji wa magari pia kampuni hiyo licha ya ukubwa wake na umaarufu wa uuzaji wa magari lakini ilikuwa ikiongozwa na kijana mmoja mdogo sana aliefahamika kwa jina la Stephan kijana aliekuwa na akili nyingi ya biashara.
Stephan alikuwa ni kijana wa miaka 24 kijana alieanza kushika pesa nyingi akiwa na umri mdogo na hii ilichangiwa na wazazi wake ambao walikuwa ni matajiri wakubwa sana ndani ya jiji.
Stephan alikuwa ni kijana mtanashati na aliechanganya akili za wanawake wengi lakini yeye licha ya kupendwa na wanawake wengi hakuna hata mmoja aliempa nafasi kwenye moyo yake wala kuthubutu fungua kinywa chake na kumtamkia neno nakupenda.
"Hivi Stephan unajua sikuelewi kabisa jamaa yangu yaani wanawake wote hawa wanaokushobokea tena wazuri na pesa zao lakini huwataki mh kweli bahati hupata watu wajinga ila kama ningekuwa mimi basi wote nishapita nao"
Yalikuwa ni maneno ya Daniel msaidizi wa Stephan katika kampuni hiyo lakini licha ya kuwa msaidi wake pia ni rafiki yake mkubwa sana ambae vitu vingi huwa wanashirikishana.
"Daniel hebu niache bhana kwanza unafikiri mimi ni mwanaume wa kununuliwa kwa pesa, kama pesa ninazo kwahiyo niache sijaona mwanamke wa kuninyima usingizi mimi"
Stephan alizungumza kwa kujiamini huku akiwa kwenye kiti chake amekunja nne lakini wakati wapo busy kuzungumza yao mrango wa ofisi uligongwa na Stephan alimuamuru Daniel afungue.
Mrango ulifunguliwa na kuingia binti ambae alikuwa mfanyakazi wa kampuni hiyo, alisogea mpaka alipo Stephan na kuweka baadhi ya karatasi juu ya meza.
"Bosi kuna mteja amekuja anahitaji kununua magari sasa nilitaka kumuuzia lakini amesema anahitaji magari kumi na tano kwahiyo nikaona ni vyema ungeenda kumsikiliza"
"Ok sawa nakuja"
Yule binti baada ya kupata mrejesho alitoka nnje na kumuacha Stephan akivaa koti lake ili kutoka kwenda kumsikiliza mteja huyo ambae hakumfahamu na haikuwa kawaida kwenye kampuni hiyo kufika mteja na kuhitaji gari nyingi kiasi hicho.
Baada ya kumaliza kuvaa koti alitoka mpaka ilipo store ya magari lakini macho yake yaligongana na binti mmoja mrembo sana na binti huyo ndiye aliekuwa mnunuzi wa magari hayo.
Alimsogelea karibu na kumpatia mkono kama ishara ya kusalimiana lakini binti yule hakuhitaji kupokea mkono wake na hii ilimfanya Stephan achukie sana.
"Hivi mbona huyu binti ana dharau sana yaani kumpatia mkono amekataa na sikuwahi kuoneshwa dharau kama hizi sasa subiri nimuoneshe!!"
Stephan alijiongelesha moyoni mwake kisha alimgeukia msaidizi wake Daniel na kumtaka amuhudumie dada huyo.
"Sasa bosi mbona unanipa jukumu hilo wakati wewe ndiye ulitakiwa kuongea nae.!!"
"Nimesema elewana nae mimi siwezi kuhudumia wateja wenye dharau na tayari nimeharabiwa siku pumbavu sana!!"
Stephan alitoka hapo hakutaka tena kuelekea ofisini kwake aliliendea gari lake na kupanda kurudi kwake huku nyuma akimuacha yule binti akimsindikiza kwa macho na kubaki kwenye mshangao.
***************
Stephan safari yake ilimfikisha kwenye supermarket moja kubwa ambayo hua kila jumaatatu lazima afike hapo na kununua mahitaji yake ya kila siku na ilifika kipindi wahudumu wa supermarket hiyo walimzoea na kutaniana nae.
Alielekea zilipo bidhaa na kuanza kuchagua anachohitaji lakini akili yake bado ilikuwa busy kumuwaza mwanamke ambae alimuharibia siku yake.
"Yaani mabinti wengine sijui kwao hua hawafunzi heshima yaani tena acha niongee na Daniel asimuuzie hata hayo magari huenda akaniletea nuksi sasa.!!"
Stephan alitoa simu yake na kutafuta namba ya Daniel kisha alipiga na hazikupita sekunde nyingi simu ilipokelewa.
"Hello bosi?"
"Hey Dani huyo binti tayari amenunua hizo gari, na kama hajanunua mwambie hatuuzi maana siwezi kumuuzia mtu ambae hana utu anaweza kuleta nuksi kwenye kampuni yangu"
"Bosi mbona tayari amenunua na tayari ameondoka ila aliniomba namba yako ya simu ya private"
"Weeee.!! kwahiyo umempa.!?"
"Sasa unafikiri nalemba mimi, tayari nimempa kwahiyo muda wowote namba ngeni itaingia kwenye simu yako ila bosi samahani kuna mteja mwingine amefika nitakupigia baadae"
Daniel alikata simu na kumuacha Stephan kwenye maswali mengi sana pia hakupenda kabisa kitendo alichofanya Daniel cha kumpatia binti huyo namba zake za simu.
Hakuwa na namna aliendelea kufanya manunuzi yake na baada ya kumaliza alilipa na kutoka nnje mpaka lilipo gari lake kisha alianza kupakia vitu alivyonunua lakini akiwa kwenye zoezi hilo alihisi mtu akimshika kwa nyuma.
Alieguka haraka na kumtazama lakini hakuamini kukutana na binti mmoja mzuri sana ila mavazi ya binti huyo yalikuwa ya kawaida sana ambayo yalificha uzuri wake kwa asilimia kubwa.
"Kaka wallet yako hii uliangusha"
Binti huyo alizungumza huku akimpatia Stephan wallet yake na kweli Stephan alipojikagua hakuona wallet yake hivyo aliipokea na kumshukuru sana binti yule.
"Samahani dada unaitwa nani.?"
"Naitwa Tresha"
Tresha alijibu na hakutaka kabisa kuendelea kubaki hapo aligeuka na kuondoka zake kwa mwendo wa haraka huku nyuma akimuacha Stephan akimtazama na kuachia tabasamu pana ambalo liliashiria kuna jambo lilikuwa la siri akilini mwake.....ITAENDELEA...
Story ni mpya na imeanza na moto wake sasa nikusihi tukutane sehemu ya pili kujua nini kitafuata katika mkasa huu wa kusisimua..
